Gabo ajadili namna ya kujisalimisha
Umoja wa Mataifa umesema majenerali watatu wanaomtii Rais Laurent Gbagbo aliyezingirwa nchini Ivory Coast wanajadiliana masharti ya kujisalimisha na huku wakitaka wahakikishiwe usalama wao pamoja na wa Bw Gbagbo.
Ufaransa umesema wapatanishi hao wanakaribia kukubaliana kuhusu kuondoka kwake.
Bw Gbagbo amejihifadhi na familia yake kwenye handaki lililopo ndani ya nyumba yake kwenye mji mkuu, Abidjan.
Majeshi yanayomtii mpinzani wa Bw Gbagbo, anayetambuliwa na umoja wa mataifa Alassane Ouattara, yamesema yamezunguka nyumba yake hiyo.
Umoja huo umesema jeshi la Bw Gbagbo na washauri wake wanamkimbia.
Umoja wa Mataifa ulimweleza mwandishi wa BBC Andrew Harding, ambaye yuko nje ya mji wa Abidjan kuwa majenerali watatu wa Bw Gbagbo- mkuu wa majeshi, mkuu wa polisi na mkuu wa walinzi wa Jamhuri-wameanzisha mazungumzo.
Source: BBC
Tuesday, April 5, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment