Bunge lawaka moto
Via Tanzania Daima
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu na ile ya Mashirika ya Umma, zimeibua ufisadi wa kutisha ulioligeuza taifa kuwa shamba la bibi.
Kamati hizo ambazo zinaongozwa na Augustine Mrema (TLP), John Cheyo (UDP) na Zitto Kabwe (CHADEMA), ziliwasilisha taarifa zake za mwaka wa fedha wa 2008/2009 jana bungeni.
Katika halmashauri za wilaya nchini, ufisadi mkubwa umebainika kuwepo katika ununuzi wa spea za magari kwa kuongeza bei isiyo halisi, bei ya kughushi katika ununuzi wa mafuta, matumizi makubwa kwa ajili ya posho kuliko utekelezaji halisi wa miradi kama ya (TASAF), Mazingira na miradi mingine ya maendeleo.
Akiwasilisha taarifa ya kamati yake, Mrema alisema kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha 2008/2009, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga ilitumia sh milioni 2.9 kwa ajili ya kutengeneza pikipiki ya Kichina, iliyonunuliwa kwa bei ya chini kuliko ile iliyotumika kuitengenezea.
Alisema katika Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, kamati yake ilibaini kuwa halmashauri ilitumia sh milioni 15 kwa ajili ya kununua spea ya gari (Injector Pump ya Land cruiser had top).
“Lakini tulipofuatilia kwa kupiga simu kwenye duka lililouza spea hiyo, tuliambiwa bei yake ni sh milioni tatu,” alisema Mrema na kuwaacha wabunge wakibaki na mshangao.
Endelea kusoma habari hii..........................
Wednesday, April 6, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment