Aliyekua mbuge wa Jimbo la Kalenga,Iringa miaka ya nyuma.mheshimiwa
Galinoma amefariki Dunia leo asubuhi mjini Iringa wakati akiwa garini
akipelekwa hospitalini kutoka kijijini kwake Kalenga,ambako alikokuwa anaishi.
Mheshimiwa
Galinoma ,alikuwa mtumishi wa serikali mstaafu aliyeshika nafasi mbali
mbali katika uhai wake zikiwa Katibu mkuu idara ya ulinzi na jeshi la
kujenga taifa,mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mbuga za
wanyama poli,mwenyekiti wa bodi ya mashirika ya Umma(SCOPO),Katibu wa
tume ya uchunguzi wa viongozi,pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la
Kalenga ,Iringa.
Marehemu Mhe.
Galinoma alikuwa anaugua kwa muda mrefu pia aliwahi kuenda India kwa
matibabu alikua huko wiki 6, na alipata nafuu kwa kiasi fulani lakini
baadae alizidiwa tena.
Marehemu
ameacha wajukuu na watoto ,miongoni mwa watoto wa wake ni
wanamuziki Innocent na Buti Jiwe aka Henry Galinoma. Taaritibu za mazishi
zitatolewa si muda mrefu.
Mungu amlaze mahala pema peponi.
Kwa habari zaidi za msiba wasiliana na Joseph Galinoma kwa namba hii 00255716492048 au Denis Galinoma namba hii 00255784769945
Chanzo: Globu ya Jamii
Thursday, January 26, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment