Mwanamke wa Kisaudi |
Sheria mpya inayowapiga marufuku wanaume kuuza nguo
za ndani za wanawake kama vile chupi na sidiria inaanza kutekelezwa hii
leo nchini Saudi Arabia.
Ajira kwa wanawake
Hatua hiyo itawapa fursa adimu zaidi ya wanawake 40,000 kuchukua nafasi za kazi zitakazoaachwa wazi.Maafisa wa kidini wasiopendelea mabadiliko wamepinga vikali hatua hiyo ya wanawake kufanya kazi nje ya nyumba zao.
Serikali imepanga kupeleka waangalizi katika vituo vya biashara kote nchini kuhakikisha kwamba wasaidizi wanawake madukani hawabughudhiwi na maafisa wa polisi wa kidini.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment