Mchezaji mahili wa mpira wa kikapu wa timu ya Miami Heat,Lebron James, amesheherekea sikukuu ya mwaka mpya na ile ya kuzaliwa kwake kwa
kumvalisha pete mchumba wake.
James alimvisha pete mchumba wake wa muda mrefu Savannah
Brinson, mama wa watoto zake wawili katika hoteli ya South Beach iliyopo jijini
Miami.
Wawili hao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu tangu James akiwa shuleni huko Akron, katika jimbo la Ohio.
Wiki iliyopita aliyekuwa mchezaji hodari wa mpira wa kikapu
na mmiliki wa timu ya Challote, Michael Jordan, alimvisha pete mchumba wake
Yvette Prieto.
Tunapenda kutoa pongezi kwa ndugu hawa kwa jambo hili muhimu
walilolifanya.
No comments:
Post a Comment