Tuesday, November 16, 2010

Best Blogger Tips
Waziri Mkuu ni Mizengo Kayanza Peter Pinda



Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua mbunge wa Katavi mkoani Rukwa, Mizengo Kayanza Peter Pinda, kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Spika Anne Makinde alimtangaza Mh. Mizengo Pinda kuwa Waziri Mkuu Mteule jioni ya leo bungeni Dodoma. Baadaye kura za kumdhibitisha zikapigwa na matokeo ni kwamba: kura zilizopigwa: 328 kura za ndio: 277 (85.4%), kura za hapana: 49 (14.9%), kura zilizoharibika 2 (0.2%).

Waziri mkuu anatarajiwa kuapishwa kesho ikulu ndogo ya chamwino, ikiwa ni hatua ya kwanza kabla ya kutangazwa kwa baraza jipya la mawaziri. hatua hii inakamilika baada ya rais kukaa na kushauriana na makamu wa rais na waziri mkuu.

Baraza hilo jipya linatarajiwa kutangazwa ijumaa.


Monday, November 15, 2010

Best Blogger Tips
Mambo ya Kobe Bryant

Sunday, November 14, 2010

Best Blogger Tips
IGP Mwema apangua makamanda

Amng'oa kamishina Nzowa Dawa za kulevya

MKUU wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, amefanya mabadiliko makubwa kwa makamanda wa Polisi wa mikoa na maofisa waandamizi ndani ya jeshi hilo.

Habari za kuaminika zilizopatikana mjini Dar es Salaam jana, zinasema IGP Mwema amefanya mabadiliko hayo ikiwa ni sehemu ya uboreshaji na utendaji kazi wa kila siku wa jeshi hilo.

“Ni kweli IGP Mwema amefanya mabadiliko makubwa yakianzia makao makuu ya jeshi hadi kwa makamanda wa polisi wa mikoa, nadhani nia ni kuboresha utendaji wa chombo hiki,” kilisema chanzo chetu.
Katika mabadiliko hayo, IGP Mwema amemhamisha Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa, kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), pia amemhamisha Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Charles Mkumbo, ambaye sasa anakwenda makao makuu.

Wengine waliokumbwa na uhamisho huo ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, ambaye anahamishiwa makao makuu, wakati nafasi yake inachukuliwa na Charles Kenyela anayetoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Pia IGP Mwema amemhamisha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye, kwenda mkoani Arusha, wakati aliyekuwa kamanda wa mkoa huo, Basilio Matei, amehamishiwa makao makuu.
Taarifa zinasema, nafasi ya Kamanda Andengenye imechukuliwa na ofisa mmoja kutoka makao makuu aliyetajwa kwa jina la Mama Charo.

Rungu hilo limemwangukia pia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi, ambaye amehamishiwa makao makuu, huku nafasi yake ikichukuliwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani.
Endelea kusoma habari hii.................
Source: Tanzania Daima

Friday, November 12, 2010

Best Blogger Tips
Samsung Galaxy Tab: New Information

It seems that a new Samsung Galaxy Tab with a bigger screen will be available in 2011.I am sure that it will have a big succes because the current Samsung Galaxy Tab is great and I am sure that the new one will be even better.

The new Samsung Galaxy Tab with ten-inch screen is assumed that a reality. It would be a Super AMOLED panel and increase its resolution to 1,200 x 600 pixels. So far, the information known so far, which suggested an increase in size and image quality of the tablet of the Korean company.

But recent data from the device that would come in 2011 also point to a decrease in this case, the weight of the screen and, by extension, the entire gadget.Samsung Galaxy Tab is a great tablet.

 As has been told in an exhibition dedicated to ecological vocation held devices in China, the future model of the Samsung Galaxy Tab have a screen built from components derived from the resin, instead of glass. This will get a drastic weight reduction. So much so that, as reported by CNN, a ten-inch screen made of resin would weigh about 28 grams, compared to 130 grams that we would find a glass panel (excluding the backlight system, of course).Current,Samsung Galaxy Tab is the best tablet from the market.

On the other hand, the weight would not be all that would ease if using glass resin screen at Samsung Galaxy Tab . He also noted that the thickness of the panel also would waist, although the reduction in thickness would be minimal, from 0.5 mm to 0.44 mm.Samsung Galaxy Tab is much better than the iPad.
Access the full story..............
Best Blogger Tips
Sugu asiachwe yatima, asaidiwe kuleta mapinduzi

Via Mwananchi

KATIKA matokeo ya wagombea ubunge, sasa tayari wameanza kazi  ya ubunge baada ya kula kiapo jana kule Dodoma, yale ya Joseph Mbilinnyi , maarufu Sugu au Mr II  yalivuta hisia za wengi.Licha ya kuwa mbunge wa Mbeya Mjini lakini Sugu ambaye alishinda kwa kishindo kikubwa dhidi ya mgombea wa CCM, Benson Mwalugala  Mpesya, lakini tunaweza kumweleza kuwa sasa ni mwakilishi wa wasanii wa Tanzania ndani ya chombo cha kutunga sheria.

Mwanzo ilikuwa vigumu kuamini kuwa ilikuwaje hadi Sugu akaamua kuingia katika siasa, tena kugombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hapo ikawa mwanzo wa wasanii mbalimbali nao kuibuka na kutangaza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.  Hata hivyo, wengi walishindwa katika nafasi ya udiwani.

Mbunge huyo mpya licha ya kuchanguliwa na wananchi wa Mbeya Mjini, lakini naamini atawahudumia watu wengi zaidi kwani kila msanii au mdau wa fani au kazi ya zanaa, anaamini kuwa kazi yake kubwa akiwa bungeni atakuwa balozi na mwakilishi wa wasanii wote nchini na si wale wa Mbeya Mjini pekee.

Katika kampeni hizo, ahadi mbalimbali zilitolewa na sasa wananchi wanasubiri utekelezaji wake licha ya kuwa wasipotekeleza  wajue mwaka 2015, mwendo  wao wa kurejea bungeni utakuwa mgumu.

Mwanzo wa kampeni zilizuka tarifa kuwa kuna baadhi ya wasanii walimkacha msanii huyo wakati alipokuwa katika hatua za awali akitangaza kugombea ubunge, sitaki kuamini kuwa wasanii hao wapo na kama wapo watakuwa wachache na labda walifanya hivyo kutokana na kukosa uvumilivu uliotokana na kutokuwa na kutopata mahitaji muhimu ambayo labda yangeweza kuwawezesha kuendelea kuwa bega kwa bega na Sugu kwa muda wote wa kampeni yake.

Ninachoamini ni kwamba kama  kweli  wapo wasanii waliomtenga balozi wao, hawakuwa na nia mbaya naye ya kutaka ashindwe, bali  majukumu ndiyo  yaliyowafanya wafikie hali hiyo.

Naamini walifanya hivyo wakiamini kuwa licha ya kutokuwepo kwao atafanikiwa kuwa mbunge wa Mbeya Mjini na ndiyo maana baada ya kutangazwa kuwa mshindi wamejitokeza kumpongeza.

Nimezungumzia dhana ya kuondoa chuki, imani potofu na visasi ambavyo huenda vikajitokeza kutokana na tuhuma za kutengwa kwa Sugu na baadhi ya wasanii.

Lakini, ninavyoamini mimi ni kwamba kama chuki na visasi vitachukua nafasi katika miaka hii mitano ya uwakilishi  wa Sugu kule bungeni, hakika  hatoweza kurudi tena bungeni na ndoto za kufanikisha kuweka au kuingiza changamoto ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria zitakuwa zimekwama.
Endelea kusoma habari hii.................
Best Blogger Tips
Mh. Anne Makinda: Spika wa Bunge la Tanzania



Hatimaye wabunge leo wameweza kumchagua spika ambaye ataongoza bunge hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

Mheshimiwa  Anne Makinda ndiye spika Mpya wa Bunge baada ya kumshinda Mh. Mabere Nyaucho Marandu katika uchaguzi wa kumpata spika mpya wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mama Makinda kapata kura 265 wakati Mh. Marando kapata kura 53.

Hivi sasa spika huyo mpya anasimamia zoezi la kuapa la wabunge wapya wa bunge hili la 10.

 Bunge la tisa lilimaliza muda wake juai 16, 2010. zoezi la kuapa wabunge wapya linatarajiwa kuchukua siku zaidi ya 2.

Wednesday, November 10, 2010

Best Blogger Tips

FIFA YAMUONGOZEA PESA OBILALE WA TOGO

Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Togo Kodjovi Obilale atapatiwa dola100,000 kutoka Shirikisho la Soka Duniani- Fifa baada ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi kabla ya kuanza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola mwezi wa Januari.

Rais wa Fifa Sepp Blatter, alimwambia Obilale mwezi wa Septemba kwamba malipo ya dola 25,000 zitatolewa kutoka mfuko wa Fifa wa misaada ya kibinadamu.

Hata hivyo Shirikisho hilo la soka Duniani kwa sasa limeamua kuongeza kiwango hicho cha pesa.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25 alifanyiwa upasuaji kutokana na majeraha ya risasi alizopigwa mgongoni na tumboni kufuatia shambulio hilo.

Shambulio hilo lililotokea katika jimbo la Cabinda nchini Angola, lilisababisha watu wawili waliokuwemo katika kikosi cha Togo kupoteza maisha pamoja na dereva wa basi lililokuwa limewachukua.
Obilale bado hawezi kutembea ikiwa ni miezi minane tangu lilipotokea shambulio la risasi lililofanywa na waasi wanaotaka kujitenga kwa jimbo la Cabinda na bado anaendelea kutibiwa nchini Ufaransa.

Togo ilijitoa katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola baada ya shambulio hilo na ilifungiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) kwa miaka minne kushiriki mashindano hayo.

Hata hivyo Fifa ilitengua adhabu hiyo.
Endelea kusoma habari hii...............
Best Blogger Tips
Mbio za Uspika: Kamati Kuu Yamuengua Sita


kamati kuu leo imepitisha majina matatu ya wana ccm watakaogombea nafasi ya uspika
kati ya wagombea 13 wa chama hicho waliojitokeza.

Nao ni Mh. Anna Abdallah,  Mh. Kate Kamba na Mh. Anna Makinda.

majina ya wanaowania unaibu spika yanatakiwa yafike ofisi za bunge keshokutwa novemba 15, 2010.

katibu mkuu wa ccm amesema sasa hivi kwamba kamati kuu ya ccm imeamua kwa makusudi kumpa nafasi mwanamke kuongoza moja wa mihimili mitatu ya nchi kwa mara
ya kwanza katika historia ya jamhuri ya muungano.

Tuesday, November 9, 2010

Best Blogger Tips
Wabunge Viti Maalumu

. CCM 65, CHADEMA 23 na CUF 8

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imekamilisha kazi ya kuwateua wabunge wa awali wa Viti Maalumu na kuwasilisha orodha ya wateule hao katika vyama husika vya siasa.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata kutoka ndani ya NEC na miongoni mwa viongozi wa juu wa vyama vitatu vya siasa vyenye wabunge wa Viti Maalumu wamethibitisha kupokea majina ya wabunge hao.

Kwa mujibu wa habari hizo, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata wabunge 65 wa Viti Maalumu, kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilichopata viti 23 na Chama cha Wananchi (CUF) kikapata viti vinane.

Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa, idadi hiyo ya viti maalum ambavyo jumla yake ni 96 itaongezeka kwa kila chama baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ulioahirishwa wa wabunge katika majimbo saba.
Chama cha NCCR Mageuzi kilichopata viti vinne vya wabunge, TLP na UDP kimoja, havikupata kiti hata kimoja cha wabunge wa viti maalumu kutokana na kukosa sifa ya kufikisha asilimia tano ya kura za wabunge wote kwa mujibu wa sheria.

Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao majina yao yamepitishwa na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Lucy Owenya (Kilimanjaro), Esther Matiko (Mara) Mhonga Luhanywa (Kigoma), Anna Mallac (Katavi), Paulina Gekul (Manyara) na Conchesta Rwalumulaza (Kagera).

Wengine ni Suzan Kiwanga (Morogoro), Grace Kiwelu (Kilimanjaro), Suzan Lyimo (Kilimanjaro), Regia Mtema (Morogoro), Christowaja Mtinda (Singida), Anna Komu (Dar es Salaam), Mwanamrisho Abama (Zanzibar), Joyce Mukya (Arusha), Leticia Mageni Nyerere (Mwanza) na Naomi Kaihula (Dar es Salaam).
Majina mengine ya wateule hao ni Chiku Abwao (Iringa), Rose Kamili (Manyara), Christina Lissu (Singida), Raya Ibrahim Khamis (Zanzibar), Philipa Mturano (Dar es Salaam), Mariam Msabaha (Zanzibar) na Rachel Mashishanga (Dar es Salaam).

Wabunge hao ambao wanatarajia kusafiri kwenda mjini Dodoma kuungana na wenzao, wanafanya idadi ya wabunge wote wa CHADEMA hadi sasa kufikia 45.

Kwa mujibu wa habari hizo idadi hiyo inakifanya chama hicho kiwe na sifa ya kuunda kambi ya upinzani bila kutegemea wabunge wa kutoka vyama vingine vya upinzani.

Kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho hata hivyo majina ya washindi hayakuweza kupatikana, kimepata idadi ndogo ya viti tofauti ilivyotarajiwa.
Endelea kusoma habari hii...............
Best Blogger Tips
Bush atetea mbinu za kuwatesa wafungwa

Aliyekuwa Rais wa Marekani, George W Bush, ametetea maamuzi yake yaliyosababisha utata mkubwa wakati wa mahojiano yake ya kwanza kwenye televisheni tangu aondoke madarakani.

Akizungumza kweye kituo cha televisheni cha Marekani cha NBC, Bw Bush alitetea mbinu ya kuwatesa wafungwa kwa kuwazamisha ndani ya maji wakati walipokuwa wakihojiwa, akisema ilisaidia kuokoa maisha na kuzuia mashambulio ya kigaidi.

Amesema uamuzi wake wa kuvamia Iraq haukuwa na kasoro na dunia kwa sasa ni salama zaidi bila Saddam Hussein.

Pia alitetea uamuzi wake wa kuyanusuru mabenki ya Marekani yaliyoporomoka kutokana na mdororo wa kiuchumi duniani.

Bwana Bush amesema anatarajia kuwa historia itatambua mafanikio yake ingawa atakuwa ameaga dunia kabla swala hilo kutokea.
Source: BBC

Monday, November 8, 2010

Best Blogger Tips
Michael Jackson's Children


Michael Jackson’s two oldest children say they’re adjusting well to private school, while their younger brother is still home-schooled.

Prince, Paris and Blanket have been living with grandparents Joe and Katherine Jackson since their pop singer father’s fatal anesthetic overdose in June 2009.

They appeared on Monday’s episode of “The Oprah Winfrey Show” and talked about their famous father.
In the pre-taped interview, 13-year-old Prince says he and his father often walked the beach early in the morning with Coca Cola and candy. Twelve-year-old Paris says her father took her to the art museum and was “the best cook ever.”

Prince says he wants to produce and direct movies someday. Paris says she wants to be an actress.
Source: Access Hollywood

Sunday, November 7, 2010

Best Blogger Tips
Mziray: Aliondoka Tanga na African Sports yetu......


Via Raia Mwema

NYINGI  ya tanzia nilizosoma kuhusu upande wa michezo wa maisha ya marehemu Syllersaid Mziray aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita zimejikita zaidi kwenye mafanikio yake katika kuzifundisha timu mbili kubwa za soka nchini za Yanga na Simba za Dar es Salaam kwa vipindi tofauti.

Yameorodheshwa pia mafanikio yake kwenye timu ya taifa ambapo yeye alikuwa miongoni mwa walimu watatu ambao mwaka 1994 waliiwezesha timu ya taifa ya soka, Taifa Stars kutwaa Kombe la Challenge mjini na Nairobi baada ya kuwa tumelikosa kwa miaka 20 kabla ya hapo. Walimu wengine walikuwa ni Sunday Kayuni na Charles Boniface Mkwasa.

Syllersaid Mziray alikuwa ni miongoni mwa walimu wa soka wachache sana nchini ambao waliweza kuzifundisha timu mbili kubwa nchini za Yanga na Simba kwa nyakati tofauti na akaweza kufanya kazi yake kwa mafanikio makubwa bila fitna za timu hizo kumuathiri kwenye utendaji wake wa kazi.

Kwa hakika, kocha Mziray alikuwa kama kocha kiraka kwa timu hizo kutokana na ukweli kwamba mara nyingi timu zilipokuwa na matatizo ya kocha zilimkimbilia Syllersaid Mziray aokoe jahazi ingawaje pia mara kadhaa ilitokea kuwa hawakuachana vizuri.

Hata hivyo, maelezo mengi yanayohusu mchango wa kocha Mziray kwenye michezo yamesahau kurodhesha mchango wake muhimu sana katika soka ambao kwangu mimi ndio uliotengeneza jina lake na kuwa miongoni mwa makocha bora kabisa wazalendo tuliopata kuwa nao.

Kumbukumbu zangu kuhusu Mziray zinanirudisha miaka 22 nyuma, mwaka 1988, wakati alipokuja mjini Tanga kufundisha timu ya African Sports ya Tanga ambayo mwaka huo ilikuwa imepanda daraja na kuingia iliyokuwa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Katika kupanda daraja huko African Sports ilikuwa imemfuata mpinzani wake wa jadi mkoani Tanga Coastal Union ambaye tayari ilikuwa ‘mzoefu’ wa kucheza Ligi ya Daraja la Kwanza iliyokuwa ya juu kabisa kwa wakati huo.

Kupanda daraja kwa African Sports na kuwapo uhakika wa kukutana na mpinzani wa jadi nchini, Coastal Union katika msimu wa ligi ya mwaka 1988 kulileta msisimko wa aina yake mjini Tanga kwani kabla ya hapo timu hizo zilikuwa hazijakutana kwenye michuano mikubwa ya soka nchini.

Chini ya Mziray, African Sports ilisuka kikosi mahiri cha wachezaji kama Francis Mandoza, Bakari Tutu, Hassan Banda, Hamza Maneno, Mhando Mdeve, Raphael John, Juma Burhani, Victor Mkanwa, na kuweka kambi kwenye mji wa Korogwe wakifadhiliwa na kampuni ya Sikh Garage.
Endelea kusoma habari hii.................
Best Blogger Tips
Mkakati waundwa kummaliza Sitta

Via Majira

KUNDI la watu wanaodaiwa kuwa ni mahasimu wa kisiasa linadaiwa kuanza mikakati mizito kuhakikisha linamwangusha Spika wa Bunge anayetea nafasi yake Bw. Samwel Sitta.

Vyanzo vyetu ndani ya CCM makao Makuu vilieleza Majira Jumapili kwamba kundi hilo tayari limeanza kutekeleza mkakati wake wa kwanza wa kutuma watu wake kuwania nafasi hiyo ili kupambana  na Bw. Sitta.

Mkakati wa pili wa kundi hilo wa kumwangusha Bw. Sitta ulitajwa kuwa ni kushawishi wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho (CC) itakayokutana kati ya Novemba 10 au 11 mjini Dodoma kukataa jina Mbunge huyo wa Urambo Mashariki.

"Tayari watu wao wawili wamechukua fomu kupambana na Mhe. Sitta, lengo ni kuhakikisha wanapata watu hata 10 kuchuana naye ili wakifika kwenye Kamati Kuu waseme kwamba hafai na ili wananchi wasipate nafasi ya kuhoji kama ameonewa wataachwa wengi.

"Wameanza kuwazungukia wajumbe wa Kamati Kuu na wapo wazee wachache wanawaunga mkono akiwemo kigogo mmoja wa chama,"kilisema chanzo chetu ndani ya CCM.

Hadi sasa waliokwishachukua famu ya kupambana na Bw. Sitta katika nafasi hiyo ni pamoja na aliyekuwa Naibu wake Bi. Anna Makinda, Bw. Andrew  Chenge, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Bw. Job Ndugai, Mbunge wa Afrika Mashariki Bi. Kate Kamba pamoja na Bi. Anna Abdallah. 
Endelea kusoma habari hii........................

Saturday, November 6, 2010

Best Blogger Tips
Hotuba ya Rais JK baada ya kuapishwa



Hotuba ya Lipumba ya kumpongeza Rais JK



Source: Habari ni habari ndugu yangu
Best Blogger Tips
JK aapishwa kuwa Rais wa Tanzania

Rais Jakaya Kiwete ameapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa asilimia 61 za  kura zote zilizopigwa.

Akitoa hotuba mara baada ya kuapishwa  alisema kuwa kipao mbele chake kwa hivi sasa ni kuhakikisha kuwa wanajenga umoja wa kitaifa na kurudisha amani iliyokuwepo awali kwani anaamini kuwa uchaguzi uliweza kuwagawa watanzania kwa namna moja ama nyingine.

Alisema mchakato wa jinsi serikali yake itakavyofanya kazi ataitoa hivi karibuni wakati akilihutubia Bunge jipya.

Alisema  kuwa katika mchakato wa kuwania uongozi nchini ni wazi kuwa yapo majeraha yaliyotokea hivyo muda huu ni mzuri kwa  baadhi ya taasisi kurejesha amani ya watanzania.

Amevipongeza vyama vya upinzani kwa  kukipa changamoto Chama Cha Mapinnduzi na kudai kuwa wamewaamsha katika usingizi kwani hivi sasa watakaa chini na kujiuliza kuwa ni wapi walipo na wafanyaje katika chaguzi zingine zijazo.

Wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi waliweza kuhudhuria katika hafla hiyo ya kuapishwa rasmi kwa rais kikwete akiwemo, Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Rais wa Zammbia Rupia banda, Rais wa Jam huri ya Demokrasia ya Kongo Joseph kabila, Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma, Rais wa Kenya mwai Kibaki, Rais wa Zanzibar Ally Mohamed Shein, maraisi wastaafu wa Tanzania Ally Hassan Mwinyi, Benjamini William Mkapa na Rais mstaafu wa Zanzibar Ally Karume.

Sherehe hizo zilipambwa na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo rais Kikwete alipigiwa mizinga 2I pamoja na ndege za kivita kufanya maonyesho na baadaye alikagua gwearide likiwa katika muonekano wa alfa.

Friday, November 5, 2010

Best Blogger Tips
JK Ateuliwa Kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kuapishwa kesho

 Akitangaza rasmi matokeo ya Urais sasa hivi katika viwanja vya Karimjee,jijini Dar Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Lewis Makame,ametangaza rasmi kuwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete kupitia chama cha CCM ameteuliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu nyingine tena ya pili.

Rais Kikwete ameibuka kwa ushindi wa kura Mil.5,276,827 ambayo ni asilimia 61% ya watu wote waliopiga kura,Huku mpinzani wake wa karibu kupitia chama cha CHADEMA,Dk.Willbroad Slaa (ambaye hakuwepo kwenye kushiriki hafla hiyo ya kutangazwa rasmi kwa kiti cha urais) ameibuka na idadi ya kura Mil.2,271,941 ambayo ni 20% ya wapiga kura.Mh Makame amesema kuwa idadi ya wapiga kura waliojiandikisha jumla yao ilikuwa ni Milioni 20,137,303,lakini waliopiga kura idadi yao ilikuwa ni Milioni 8,626,283 ambayo ni 42% ya waliopiga kura.

Thursday, November 4, 2010

Best Blogger Tips
Bungeni hapatoshi

BUNGE la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa linaweza kuwa na sura tofauti kiutendaji kwa kuzingatia matokeo ya kura za ubunge na urais zilivyo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ikionekana kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekwishamudu vigezo vya kuongoza Kambi ya Upinzani Bungeni, kama kilivyo Chama cha Mapinduzi (CCM), Raia Mwema limebaini.

Kwa kadiri ya mwenendo wa matokeo, chama chenye kupata wabunge wengi ndicho kitakachoweza kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kile kitakachofuata kwa idadi ya wabunge kitaongoza Kambi ya Upinzani Bungeni. Mchuano huo wa ama kuongoza kambi ya upinzani au kuunda serikali sasa ni dhahiri ni kati ya CCM na CHADEMA.

Kwa mujibu wa mwenendo ya matokeo ya kura za ubunge, CHADEMA inaelekea kupata wabunge wengi zaidi ya Chama cha Wananchi (CUF) ambacho awali ndicho kilichokuwa kikiongoza Kambi ya Upinzani Bungeni chini ya kiongozi wake, Hamad Rashid Mohammed.

Hata hivyo, katika Bunge la tisa lililovunjwa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, CUF ilikuwa na uwezo wa kuunda Kambi ya Upinzani bila kushirikisha chama kingine cha upinzani na ilifanya hivyo mwanzoni mwa Bunge lakini baadaye chama hicho kiliwashirikisha wabunge wa vyama vingine ambayo ni CHADEMA, UDP na TLP.

Katika mazungumzo yake na Raia Mwema kuhusu mazingira hayo, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohammed ameliambia Raia Mwema kwamba taratibu za sasa zinabainisha chama chochote cha siasa kinaweza kuunda kambi yake kama kitafikisha asilimia 12 ya wabunge wote wa Bunge.
Endelea kusoma habari hii................
Source: Raia Mwema

 

Best Blogger Tips
Mbio za uspika zapamba moto

* Chenge, Ndugai wajitosa
* Jenista kuwania unaibu

MCHAKATO wa wana-CCM kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Spika wa Bunge, umezidi kupamba moto, baada ya aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, kuchukua fomu. Mbali na Chenge, ambaye ameshinda ubunge jimbo la Bariadi Magharibi, wengine waliochukua fomu jana ni Job Ndugai, aliyeshinda ubunge Kongwa, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bunge lililopita.
  
Wengine ni Kate Kamba, ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Benedict Lukwembe. Wana-CCM hao walikabidhiwa fomu na Katibu Mkuu wa Chama, Yussuf Makamba. Aliyekuwa Spika wa Bunge lililopita, Samuel Sitta, amechukua fomu kutetea nafasi hiyo. Pia aliyekuwa Naibu wake, Anne Makinda, naye anawania kiti hicho na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tambaza, Salimu Kungulilo. Makamba akiwakabidhi fomu kwa nyakati tofauti katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, alisema kutokana na Chama kutaka wana-CCM wengi wagombee, wameamua kuogeza siku za uchukuaji fomu.

“Mwisho wa kuchukua fomu ni Novemba 8, mwaka huu. Wanachama wote watatakiwa wawe wamemaliza kuchukua na kurudisha fomu,’’ alisema. Makamba alisema lengo ni kutoa nafasi kwa majina kupelekwa ngazi husika kwa ajili ya mchakato wa uteuzi, ambapo baadae Kamati ya Wabunge wa CCM itateua jina moja, litakalopelekwa ofisi ya Bunge. Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Chenge alisema amejitokeza kuwania nafasi hiyo kutokana na kuwa na uzoefu wa shughuli za Bunge. “Nina mambo mengi nataka kulifanyia Bunge, kwa kuwa ni kiungo muhimu kati ya mwananchi na serikali, hivyo naweza kuwa Spika na kulisimamia hili vyema,’’ alisema Chenge.

Naye, Ndugai alisema uwepo wake bungeni kwa vipindi vitatu unampa uwezo mkubwa wa kuendesha shughuli za Bunge.
“Nina uzoefu mkubwa. Nimekuwa Mwenyekiti wa Bunge, Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Mazingira na Utalii na kamati nyingine za mabunge ya Jumuia ya Madola,’’ alisema Ndugai.

Wakati huo huo, Makamba alisema fomu za kuwania unaibu spika zimeanza kutolewa na Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama kwa gharama ya sh. 100,000. “Fomu za unaibu spika zimeshaanza kutolewa, lakini hizi ni kwa wabunge pekee, ambapo wabunge wanapaswa kuchukua fomu hizo,’’ alisema
Kwa upande wake, Jenista alisema fomu hizo zinapatikana Dodoma na Dar es Salaam, ambapo aliwataka wabunge wote wanaotaka kugombea waende kuchukua. Jenista aliyeshinda ubunge jimbo la Peramiho, alisema yeye atachukua fomu kuwania nafasi hiyo, kwa kuwa anataka kuendelea kulipa heshima Bunge la Tanzania kimataifa. Alikuwa Mwenyekiti wa Bunge lililopita.
Source: Uhuru

Wednesday, November 3, 2010

Best Blogger Tips

Republican yashika udhibiti wa bunge


 Imekuwa siku muhimu kwa chama cha Republican nchini Marekani baada ya matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula kuangazwa. Baadhi ya maeneo muhimu ambayo yalikuwa ngome ya chama cha Democratic sasa yako chini ya chama cha Republican.

Chama hicho kimetwaa viti sita vya bunge la Senate kutoka kwa chama cha Democratic na katika bunge la wawakilishi wamepitisha idadi ya wabunge 118 wanaohitajika ili kuwa na idadi kubwa.

Hii ina maana kwamba spika mpya atakuwa John Boehner kutoka jimbo la Ohio.

Amesema kwa kuwa sasa chama chake kina idadi kubwa ya wabunge watajiandaa kufanya mambo kwa njia tofauti. Ameongeza kuwa watazingatia kupunguza matumizi badala ya kuongeza.

Hamasa kubwa inayoonekana katika kampeni za chama cha Republican imetoka kwa vuguvugu la Tea party ambalo limeundwa na wanaharakati.

Chama cha Rais Barack Obama kimepata pigo kubwa kama ilivyotarajiwa lakini pia wamejipatia ushindi katika maeneo machache ikiwa ni pamoja na Nevada ambapo kiongozi wa Senate Harry Reid alimshinda mpinzani wa vuguvugu la Tea party.

Baada ya kutangazwa mshindi seneta Reid alikiri kuwa kilikuwa kibarua kigumu kuhimili upinzani huo.
Rais Obama sasa atakabiliwa na changamoto kubwa katika kutimiza ajenda yake.
Source: BBC

Tuesday, November 2, 2010

Best Blogger Tips
Sitta: Bunge lijalo linatisha

Asema limesheheni watu makini kutoka upinzani

SPIKA wa Bunge lililomaliza muda wake, Samuel Sitta, amesema Bunge lijalo litakuwa tishio na anatamani kuwa spika wake.

Sitta alitoa kauli hiyo jana muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge katika Jimbo la Urambo Mashariki (CCM).

Sitta ambaye amejiita kuwa ni ‘Chuma cha Pua’ kutokana na ushindi alioupata, alisema amekuwa akisoma majina ya wabunge wateule walioshinda na kubaini kuwa limesheheni vijana wengi machachari na watu wenye uwezo na uzoefu wa siasa kutoka vyama vya upinzani.

“Bunge lijalo ninavyoliona mimi, litakuwa Bunge la kutisha, maana lina vijana na watu machachari, ukisoma majina yao utaona kabisa kwamba ni watu makini na ni tishio, hivyo natamani kuwa spika wa Bunge hilo ili nikabiliane na changamoto zitakazojitokeza,” alisema Sitta.

Kwa mujibu wa Sitta, pamoja na bunge hilo kuwa na watu machachari, anaamini kwamba atalimudu vyema hivyo amekiomba chama chake kumpa ridhaa ya kushika wadhifa huo kwani ana uzoefu wa kutosha.
Alipoulizwa jambo gani analolikumbuka katika Bunge lililopita na lililotoa changamoto kubwa kwake, Sitta, hakusita kutaja sakata la Richomnd, lililosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa huo.

Sakata hilo lilisababisha pia aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha na wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kujiuzulu.
Endelea kusoma habari hii....................
Best Blogger Tips

CCM yapata pigo katika ubunge Tanzania

Via VOA News

Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Tanzania ulofanyika tarehe 31 Oktoba, yanaoynesha baadhi ya wakuu wa serikali katika nafasi za mawaziri na wakuu wa mikoa, wametupwa katika nafasi za ubunge zilizokuwa na upinzani mkali.

Miongoni mwa waliopteza nafasi katika serikali kuu, ni Dk. Batilda Buriani ambaye alikua akiwania ubunge kaika jimbo la Arusha mjini ameshindwa kwa kishindo na Godbless Lema wa CHADEMA.

Philip Marmo ambaye ni kiongozi wa siku nyingi katika serikali naye ameshindwa kuitetea nafasi yake ya Mbulu. Vongozi wengine ambao wanasadikiwa wamepoteza nafasi zao ni pamoja na aliyewahi kuwa waziri katika serikali Anthony Dialo, Waziri wa sasa wa mambo ya ndani Lawrence Masha aliyeshindwa na Ezekiah Wenje wa CHADEMA pia katika jimbo la Nyamagana.

Waziri wa viwanda na biashara Mary Nagu ambae alikua anatetea kiti chake cha huko Hanang ameondolewa sawa na Getrude Mongella wa CCM aliyekua spika wa Bunge la Afrika.

Viongozi wengine wa serikali za mikoa walioshindwa ni pamoja na Monica Mbega wa Ruvuma, na Mohamed Abdulaziz wa Lindi. Vincent Nyerere ambaye ni mtoto wa kakake rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere, ameshinda jimbo la Musoma mjini.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi jaji mstahafu Lewis Makame, alitangaza Jumatatu matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais ya majimbo 10 ya Tanzania bara na visiwani.


 

Monday, November 1, 2010

Best Blogger Tips

DK SHEIN ATANGAZWA RAIS ZANZIBAR!

Tume ya Uchaguzi ya Taifa imemtangaza sasa hivi Dk. Mohamed Shein wa CCM kuwa Rais wa Zanzibar baada ya kupata jumla ya kura 179,809 sawa na 50.1% dhidi ya maalim Seif wa Cuf. Maalim Seif ameyakubali matokeo na amempongezi kwa dhati kabisa Dk. shein kwa kupata ridhaa ya Wazanibari ya kuwaongoza kwa miaka 5. "Najua kabisa dk. Mohamed Shein ana uwezo na mahaba ya dhadi ya kuongoza na kuiunganisha nchi yetu", alisema Maalim Seif na kushangiliwa kwa makofi. Kwa maana hiyo Maalim Seif atakuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi kwa mujibu wa muafaka.

Sunday, October 31, 2010

Best Blogger Tips
Upigaji kura wamalizika Tanzania

Via BBC

Mamilioni ya Watanzania wamejitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, uchaguzi ambao kwa jumla umekwenda kwa hali ya utulivu licha ya matatizo na vurugu za hapa na pale.

 Wapiga kura kadha hawakuweza kupiga kura kutokana na majina yao kutokuwemo katika daftari la wapigaji kura, kwingineko karatasi za kupigia kura zilichelewa kufika au hazikufika kabisa.

Katika visiwa vya Zanzibar, karatasi za kupigia kura katika uchaguzi wa rais na wabunge wa muungano zilikosekana katika vituo mbalimbali.

Uchaguzi wa madiwani umelazimika kuahirishwa hadi siku zijazo kwa sababu hizo hizo.

Vituo vya uchaguzi vimefungwa rasmi saa kumi jioni, huku kazi ya kuhesabu kura ikianza katika vituo hivyo.

Wapiga kura milioni 19.6 walitarajiwa kushiriki katika upigaji wa kura.

Wakati huo huo Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania imetangaza imeahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata kutokana na upungufu uliojitokeza hususan katika karatasi za kura.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rajabu Kiravu, Kata na Majimbo ambayo uchaguzi wake umeahirishwa ni kama ifuatavyo:-

1. Uchaguzi wa Wabunge katika majimbo ya Nkenge, Mpanda Mjini na Mpanda vijijini. Kwa upande wa Zanzibar (Unguja) Majimbo ya Mwanakwerekwe, Mtoni na Magogoni, na Wete (Pemba)
2. Uchaguzi wa Madiwani katika kata zifuatazo:


HALMASHAURI KATA

1. Newala DC Mtonya

2. Mbulu DC Endegikot

3. Manyoni DC Kitaraka

4. Same DC Kisiwani

5. Kibaha DC Janga

6. Rufiji (a)Kibiti

(b) Chemchem

(c) Ngorongo

(d) Kipugira

(e) Mjawa

7. Uyui DC (a)KIgwa

(b)Ibelamilundi

8. Sikonge Kisanga

9. Njombe Mji Mwema

10. Ulanga DC Msogezi

11. Karagwe DC (a) Kimuli

(b) Kamuli

12. Kasulu Kitagata

13. Chato DC Buseresere

14. Mwanza (Jiji) (a) Mkuyuni

(b) Mirongo

Hata hivyo katika majimbo hayo matatu ambapo Uchaguzi wa Wabunge umeahirishwa, uchaguzi wa Rais na Madiwani umefanyika kama ilivyopangwa.

Vile vile, katika Kata ambazo Uchaguzi wa Madiwani umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Wabunge umefanyika kama ilivyopangwa.

Tume hiyo ya Taifa ya Uchaguzi imesema tarehe za kufanyika uchaguzi huo itatangazwa hapo baadaye.
Best Blogger Tips

Jina langu lilikatwa nisigombee ubunge - Dk. Mwakyembe

Via Ippmedia

  Mgombea Ubunge Jimbo la Kyela kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Harrison Mwakyembe, amevunja ukimya kwa kutoboa siri kwamba Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mbeya ilikata jina lake ili asiwe mgombea.

Lakini akasema pamoja na mbinu hiyo, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, ndiye aliyeokoa jahazi kwa kuamuru jina lake lirejeshwe ili kulinda heshima na maamuzi ya wananchi wa Kyela waliompa kura nyingi wakati wa mchakato wa kura za maoni.

Dk. Mwakyembe alitoa madai hayo mazito wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Mpunguti, kata ya Makwale, alipokuwa akieleza sababu zinazomfanya aendelee kumnadi mgombea urais kupitia CCM, Dk. Kikwete, licha ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk.Wilbroad Slaa, kumtaka asimnadi mgombea huyo ili chama chake kisiweke mgombea ubunge wa kupambana naye jimbo la Kyela.

“Nawajibika na nalazimika kumpigia debe Rais Kikwete kwa sababu bila ya JK nisingesimama kuongea nanyi hapa, Kamati ya Siasa Wilaya walinipa alama A kwa maana ya kwamba nafaa kugombea kwa tiketi ya CCM, lakini jina lilipopelekwa kwenye kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa ambayo miongoni mwa wajumbe wake ni Mkuu wa Mkoa walikata jina langu,” alisema.

Dk. Mwakyembe ambaye alipata kura 15,336 wakati wa mchakato wa kura za maoni, alidai kuwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mbeya walichukua uamuzi wa kukata jina lake na kumpa mgombea aliyeshika nafasi ya pili katika kura za maoni kwa madai kuwa “yeye ni mkorofi, amewaumiza wenzake hasa katika suala la mkataba tata wa kampuni ya Richmond”.

"Kamati ya siasa ya Mkoa imekata jina langu, wengine tunapenda kutoa hoja za msingi na siyo hadithi, walikata jina langu na leo nalazimika kusema hivyo, kisa eti mimi ni mkorofi nilishawaumiza wenzangu, mimi nashangaa watu wanaozungumzia mambo hayo, unajua tunaanza kuwa taifa linalokosa maadili, umeumiza nini, mwizi umwangalie umchekee chekee?" alihoji.

Hata hivyo, alisema baada ya matokeo ya maamuzi hayo kupelekwa Dodoma kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoketi chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, kiongozi huyo wa CCM aliamuru jina lake lirejeshwe haraka ili kuzingatia demokrasia ya wananchi wa wilaya ya Kyela ambao walimpa kura nyingi wakati wa mchakato wa kura za maoni.

Alisema kutokana na upendo alionao Rais Kikwete kwa wananchi wenzake, kuna kila sababu kwa wana- Kyela kuhakikisha leo wanamchagua mgombea huyo wa urais wa CCM ili aweze kuendeleza mipango ya maendeleo katika jimbo hilo.

Saturday, October 30, 2010

Best Blogger Tips
R.I.P Syllesaid Mziray


Kocha aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya soka nchini Tanzania, Syllesaid Mziray "Mwanangu", amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Agakhan, jijini Dar-es-salaam. 

Coach Mziray, aliyekuwa mwajiriwa wa Chuo kikuu huria kama Mhadhiri, atakumbukwa kwa umahiri katika ufundishaji soka katika vilabu mbalimbali hadi timu ya Taifa iliyoshinda ubingwa wa Nchi za Afrika Mashariki.

Alifundisha pia Pilsner, Simba, Yanga, Pan African na kabla mauti kumkuta alikuwa mwalimu wa viuongo na saikolojia wa klabu ya Simba.


Mwenye-ezi Mungu Umuweke Mahala Pema Peponi Super Coach Syllesaid Mziray.

Friday, October 29, 2010

Best Blogger Tips

Leo ni funga kazi ya kampeni 2010
 
HATIMAYE mbio za kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu zinahitimishwa leo kwa wagombea kufunga pazia kwenye maeneo mbalimbali kabla ya Watanzania kuamua mustakabali wa nchi yao kesho.
Kampeni hizo zilizinduliwa rasmi Agosti 20 na vyama kuanza kujinadi siku iliyofuata wakati CCM ilipofanya mkutano wake kwenye viwanja vya Jangwani na kufuatiwa na CUF iliyoendesha mkutano wake Agosti 27 kwenye Uwanja wa Kidongo Chekundu na baadaye Chadema ilizindua kampeni zake Agosti 28 kwenye viwanja vya Jangwani.

Vyama hivyo vitatu, ambavyo vinachuana vikali kwenye kinyang'anyiro cha urais, vilifungua pazia kwa vyama vingine kuzindua kampeni zake kwa staili tofauti na viwanja tofauti na leo vitakuwa vikitupa karata ya mwisho baada ya safari ndefu zaa kujaribu kuwafikia wananchi kwenye mikoa tofauti ya Bara na Visiwani.

Wakati vyama hivyo vilitegeana wakati wa uzinduzi, leo vyote vitakuwa majukwaani kuhitimisha kampeni hizo ili kuwaweka sawa wapigakura kabla ya kufanya maamuzi yao kwa siri kesho.
CCM, ambayo inawania kubakia madarakani ili kuendeleza ubabe wake wa takriban miaka 49, itahitimisha kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani ambako mgombea wake wa urais, Jakaya Kikwete atahutubia wafuasi na wanachama wa chama hicho kikongwe.

Chadema, ambayo bila ya kutarajiwa imeonekana kutoa upinzani mkali kwenye kinyang'anyiro cha urais ambacho katika chaguzi zilizopita kilikuwa kati ya CCM na CUF, itahitimisha kampeni zake mkoani Mbeya ambako mgombea wake wa urais, Dk Willibrod Slaa atahutubia.
CUF, ambayo mgombea wake wa urais, Prof Ibrahim Lipumba anawania kwa mara ya nne kuingia Ikulu, itahitimisha kampeni zake kwenye Uwanja wa Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam ambako watapokonyana mashabiki na CCM.

Monday, October 25, 2010

Best Blogger Tips
Mauaji Maswa: Shibuda aachiwa huru



 JESHI la Polisi limemwachia huru mgombea ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Shibuda, kwa madai hakuhusika na mauaji yaliyosababishwa na vurugu zilizotokea katika Kijiji cha Kizungu, wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Maswa jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba, alisema wameamua kumwachia huru mgombea huyo kutokana na upelelezi wa awali kuonyesha kuwa hakuhusika na tukio hilo.

Alisema upelelezi huo umeonyesha wazi kuwa hakuwepo katika eneo la tukio ambapo mauaji hayo yalipotokea baada ya wafuasi wa vyama vya CHADEMA na CCM waliposhambuliana na kusababisha kifo cha Stephen Kwilasa.

“Unajua linapotokea tukio kama hilo la mauaji ni lazima tufanye upelelezi kwa makini, ili kuweza kutenda haki kwa pande zote na sisi kama polisi tupo hapa kwa ajili ya kulinda usalama wa raia, hasa katika matukio haya ya kampeni za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu, ni lazima tufanye kazi kwa umakini mkubwa,” alisema.

Alisema bado wanaendelea na upelelezi na iwapo itabainika kwa namna moja au nyingine alihusika na tukio hilo, atafikishwa mahakamani na kuongeza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Aidha, alisema Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Kata ya Nyalikungu, Abel Jombo, amelalamika katika Kituo cha Polisi Maswa dhidi ya Shibuda akidai kuwa alimpiga mateke alipopelekwa katika eneo la mkutano, ambapo alikuwa akihutubia mgombea huyo na kusisitiza kuwa upelelezi wa tukio hilo haujakamilika.
Endelea kusoma habari hii..............
Best Blogger Tips
Gregory Isaac Dead - Reggae Star dies of cancer

Reggae legend Gregory Isaacs has died after a battle with cancer.
Isaacs, who was 59 years old, died on Monday morning at his home in London where he spent part of his time.

He leaves behind a wife and children.

Close friends told BBC Caribbean that he had originally been diagnosed with cancer of the liver which had then spread.

The Jamaican reggae singer, who was nicknamed the Cool Ruler, was best known for the song 'Night Nurse'.








 

Saturday, October 23, 2010

Best Blogger Tips
Mugabe hands Munya US$300,000



BIG Brother Africa star Munyaradzi Chidzonga has received US$300,000 from President Robert Mugabe following his disappointment of controversially missing out on winning the reality TV show last Sunday.

The money was raised overnight after businessmen Phillip Chiyangwa and David Chapfika set up a Chidzonga Trust Fund and opened a bank account on Tuesday to marshal donations.

Wednesday’s gift, received by Munya at State House, means he has now received MORE MONEY than the show’s winner Uti Nwanchukwu of Nigeria who took home US$200,000.

Munya received a hero’s welcome as he emerged from the arrivals terminal at the Harare International Airport, coming from South Africa where the show is filmed.
 
But fans were left high and dry after the Big Brother star was bundled into a maroon Chevrolet and driven to State House.
   
Best Blogger Tips
CCM, Chadema walumbana mauaji Maswa

Via Mwananchi

WAKATI Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akikitupia makombora Chadema kwamba kinahusika na mauaji yaliyotokea katika mkutano wa kampeni, Jimbo la Maswa Magharibi, Chadema kimesema chama hicho tawala ndicho kitabeba lawama kwa kuvamia mkutano wao.

Mgombea urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akiwa katika mkutano wa kampeni mkoani Tanga jana alisema maafa hayo yamesababishwa na CCM kwa kuwafundisha na kuhamasisha vijana wake kuvamia mikutano ya vyama vingine vya siasa.

Alisema muda sasa umefika kwa serikali kuonyesha kwa vitendo kwa kuwashughulikia wote wanaohusika kuvunja amani ya nchi bila kujali itikadi zao za kisiasa kwa kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria kwani kuvunja amani ni kosa la jinai.

Dk Slaa alitaja baadhi ya maeneo nchini ambako umwagaji damu umetokea mpaka sasa kutokana na sababu za kisiasa kuwa ni pamoja na Hai, Kagera, Tarime, Mwanza, Mpanda na Maswa na kuhoji sereikali inasubiri watu wangapi wajeruhiwe au kupoteza maisha ndipo ichukue hatua.

"Tangu nimeanza mikutano yangu inayokaribia zaidi ya mikutano 460 hadi sasa nimesisitiza amani na kueleza wazi kuwa siko tayari kwenda Ikulu kwa wananchi wangu kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa na wengine kupata ulemavu au kupoteza maisha. Nimekuwa nikimuomba Kikwete ajitokeze hadharani kukemea vitendo vya vijana wa CCM kuanzisha vurugu na avunje na kupiga marufuku makambi ya vijana hao lakini hata siku moja hajafanya hivyo ikiwa ni dalili ya kuunga mkono vitendo hivyo," alisema Dk Slaa.

Wakati Slaa akisema hayo, kwa upande wa CCM Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusufu Makamba amesema kuna ushahidi wa kimazingira unaoonyesha kuwa mgombea wa Chadema jimbo la Maswa Magharibi, John Shibuda amehusika katika mauaji yaliyotokea juzi wilayani humo na kusababisha kifo cha mtu mmoja

Makamba ambaye alikuwa wilayani Maswa jana ambapo mbali na kufanya shughuli za chama pia alikwenda kutoa salamu za rambirambi kwa ndugu wa merehemu Steven Kwilasa, ambaye alikuwa dereva wa mgombea ubunge wa jimbo la Maswa Magharibi kupitia CCM, Robert Kisena.
Endelea kusoma habari hii..............

Monday, October 18, 2010

Best Blogger Tips

Alicia Keys Calls Motherhood ‘Bliss’


Alicia Keys is “Fallin’” for motherhood!
The gorgeous Grammy-winner, who gave birth to her son, Egypt, on Thursday, took to her Twitter page to share her maternal joy.

“There is no word to properly describe LOVE, to describe BLISS, to express a FEELING like this!!!” Alicia Tweeted on Sunday.

“Thank U 4 your love, support & prayers! ;-),” she added.

As previously reported on AccessHollywood.com, a representative for Alicia said the star gave birth on Thursday night in New York. Alicia and her husband, rapper-producer Swizz Beatz, have named their son Egypt Dean.

Egypt is the first child for the 29-year-old superstar and the fourth child for Swizz, whose real name is Kaseem Dean. The couple married on July 31.

Swizz, 31, took time to Tweet about his son’s arrival on Friday, calling the arrival another blessing.

“I’m so thankful for everything I been blessed with in my life wowwwwww!” he wrote.
Source: Access Hollywod

Thursday, October 14, 2010

Best Blogger Tips
Gari la Chenge lagonga tena, laua


MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi mkoani Shinyanga (CCM), Andrew Chenge ameingia matatani tena baada ya gari lake kudaiwa kumgonga mwendesha pikipiki na kusababisha kifo wakati akitoka kwenye kampeni.

Tukio hilo limetokea wakati mwanasheria huyo wa zamani akiendelea na kesi ya mashtaka mawili ya kuendesha kizembe na kugonga pikipiki ya matairi matatu na kusababisha vifo vya watu wawili na jingine la kuendesha gari ambalo bima yake ilishaisha.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa katika ajali ya jana waziri huyo wa zamani wa Miundombini hakuwa akiendesha gari hilo, bali alikuwa ndani.

Habari zilizopatikana jana kutoka wilayani Bariadi zimeeleza kuwa Chenge akiwa anatokea Kijiji cha Namisagusa na Kilalo alikokuwa na mkutano wa kampeni kuelekea mjini Bariadi, alipata ajali hiyo katika Kijiji cha Mbiti kilicho Kata ya Mhango, Tarafa ya Ntunzu.

“Hii ajali imetokea majira ya saa 1:00 usiku, Chenge baada ya kuona gari lake limegonga alishuka na kuhamia katika gari jingine na kuondoka eneo hilo. Wananchi walipofika hapo walilizuia gari hilo, lakini baadaye wakatimuliwa na polisi ambao waliliondoa gari hilo,” alieleza Patrick Liyuba mmoja wa wananchi wanaodai kushuhudia ajali hiyo.
Source: Mwananchi
Best Blogger Tips
'The View': Joy and Whoopi walk out on Bill O'Reilly


What you see here is the “Before” moment. Bill O’Reilly appeared on The View today to argue against Park51, the Muslim community center slated to be built two blocks from the World Trade Center.

 First he spoke to Joy Behar like a child: “Hold it, hold it. Listen to me because you’ll learn.” She responded in the only practical way: bunny ears. O’Reilly kept at it, insisting that 70 percent of Americans don’t want this mosque.

 “Where’s that poll?” Joy wondered. The eruption occurred after O’Reilly blamed Muslims for the WTC attacks: “Muslims didn’t kill us on 9/11? That’s what you’re saying?” O’Reilly wanted to make sure. And Whoopi and Joy stormed off the set! “I don’t want to sit here anymore,” Joy said, to clarify.

Barbara Walters took the reins.”You have just seen what should not happen. We should be able to have discussions without washing our hands and screaming and walking offstage. I love my colleagues, but that should not have happened.
Source: EW.com

Best Blogger Tips

Mgodi Chile: Miujiza yasherehekewa


Rais wa Chile amesema kamwe nchi yake haitarejea hali iliyokuwa nayo awali baada ya kukamilika kwa shughuli ya uokoaji wa wachimba migodi 33 waliokuwa wamenaswa chini ya ardhi kwa siku 69.

Sebastian Pinera amesema anahisi wananchi wa Chile sasa "wana umoja zaidi na imara kuliko wakati mwingine wowote" na wanaothaminika kote duniani.

Kulikuwa na kila hali ya ushangiliaji wakati Luis Urzua, mwenye umri wa miaka 54, mchimbaji wa mwisho alipotolewa nje ya mgodi huo.

Shughuli hiyo iliyofanyika kwa saa 22, ilitekelezwa kwa kila mmoja wao kutolewa kwa kutumia chombo maalum. Wote sasa wamepelekwa hospitalini.

Baadhi yao wamebainika kuwa na matatizo ya meno, na wengine wanasumbuliwa na macho kutokana na kuishi katika vumbi na giza mgodini humo. Mmoja wao amegundulika kuwa na kichomi, ingawa hali yake inaelezewa kuwa si mbaya sana.
Endelea kusoma habari hii...................
Best Blogger Tips

Inside Story: T.I. Knew in His Heart He Needed to Save Suicidal Atlanta Man


What started off as any other day for T.I. ended with an emotional rescue as the rapper helped coax a suicidal Atlanta man off a ledge Wednesday.

After hearing about the man, who was contemplating jumping off the V103 radio station building, the rapper decided he needed to stop listening and do something.

"People were trying to talk to him and tell him to get down," the rapper, 30, whose real name is Clifford Harris Jr., tells PEOPLE in a phone interview from the set of his new music video. "Something in my heart just said, 'You need to help.' At that point, I started calling people at the radio station."

But the radio station said the man was unresponsive to their pleas not to jump – so T.I. drove himself to the scene.

"I went down there and talked to a police officer and he sent me to the negotiator," the rapper says. "They told him I was there and he started responding a little bit."
Access the full story....................
Best Blogger Tips
Ndoto za Nyerere zimewekwa kando


WASOMI, wanasiasa na viongozi wa dini wamesema ndoto za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere zimemezwa na watu wachache wenye uchu wa madaraka na wasiojali wala kuitakia mema Tanzania.

Wakitoa maoni yao jana kwa nyakati kuhusiana na maadhimisho ya miaka 11 tangu Mwalimu Nyerere alipofariki dunia inayofanyika leo, wanazuoni na viongozi hao waliwataka Watanzania mwaka huu kumwenzi muasisi huyo taifa kwa kutowachagua watu wabaya na kuwahimiza wagombea wa nafasi mbalimbali kuheshimu matokeo ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Okotba 31.

Walisema maadili ya uongozi yaliyoachwa na Nyerere yamesahauliwa na viongozo hivyo kuna haja kwa taifa kurejesha maadili hayo ili kuinusuru nchi.
Mwalimu Nyerere alifariki dunia kwa ugonjwa wa saratani ya damu Oktoba 14, 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza alikoenda kutibiwa.

''Moja ya mambo ya msingi ambayo tunapaswa kumuenzi Mwalimu Nyerere, ni kuheshimu maamuzi ya wananchi katika kuchagua mgombea wa urais, ubunge na udiwani. Kuchakachua matokeo, itakuwa ni jambo la hatari,'' alisema aliyewahi kuwa Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Arcado Ntagazwa.

Ntagazwa alisema kuheshimu maamuzi ya wananchi ni sehemu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu.
Endelea kusoma habari hii..............

Wednesday, October 6, 2010

Best Blogger Tips

Sunday, October 3, 2010

Best Blogger Tips
Helkopta ya Dr Slaa ikitua Iringa

Helkopta ya Dr Slaa ikitua katika moja ya mikutano yake ya kampeni Mkoani Iringa. Picha kwa hisani ya francisgodwin.blogspot.com
Best Blogger Tips

 

Best Blogger Tips

Nigeria: Mshukiwa wa bomu akamatwa SA


Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi nchini Nigeria ametiwa nguvuni kuhusiana na mashambulio ya bomu nchini Nigeria ya Ijumaa iliyopita.

Henry Okah alikamatwa na maafisa wa polisi wa Afrika Kuisni katika nyumba yake mjini Johannesburg. Okah aliwahi kuwa kiongozi wa kundi la MEND kundi la waasi lililofanya mashambulio mengi dhidi ya maeneo ya mafuta.

Kundi hilo limedaiwa kuhusika katika mashambulio hayo japo lilikuwa linastahili kutekeleza usitishwaji wa vita chini ya makubaliano kati yake na serikali.
Source: BBC

Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits