CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilianza kutumia helkopta katika mikutano yake ya
kampeni za ubunge katika Jimbo la Igunga na kusababisha baadhi ya mikutano ya vyama vingine vinavyoshiriki kampeni hizo kuvunjika.
Helkopta hiyo inayoendeshwa na Kapteni Paul Denge iliwasili saa 6:00 mchana katika kiwanja cha Shule ya Msingi Choma cha Nkola na kusababisha walimu na wanafunzi kuvunja vipindi vya masomo kushuhudia chopa, pia wananchi waliikimbilia kwa baiskeli na pikipiki, kitendo kilicholazimisha walinzi wa Chadema kufanya kazi ya ziada kuzuia wananchi walionekana kutaka kuishika na kupiga picha.
Wakati Chadema kikianza kutumia helkopita hiyo na kupata wananchi wengi kwenye mikutano yao, Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana kilikuwa kimesimamisha kampeni kusubiri helkopita zake mbili ambazo zilitarajiwa kuwasili muda wowote, zikitokea Dar es Salaam.
Nacho Chama cha Wananchi (CUF), kilikutana na waandishi wa habari na kuwaeleza nia ya kuleta chopa kama hiyo, ili kuwafikia wananchi katika maeneo ya jimbo hilo ambalo kijiografia limekuwa na miundombinu isiyopitika kirahisi.
Mara baada ya helkopita hiyo kuwasili, iliwachukua viongozi wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti, Bw. Freeman Mbowe, mgombea ubunge Bw. Joseph Kashindye na mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro, Bi. Susan Kiwanga pamoja na waandishi wa habari na kuelekea katika kijiji cha Chabiso.
Katika Kijiji cha Chabiso, CUF walikuwa wafanye mkutano eneo hilo lakini baada ya kukimbiwa na wananchi wote waliamua kuvunja mkutano na kuondoka.
Akizungumza katika mkutano kijijini hapo, Bw. Mbowe alisema CCM imekabwa kila kona na safari hii haitatoka, kisha akawataka wananchi kufumbua macho kwa kuwa saa ya ukombozi imefika kwani wameteseka ndani ya miaka 50 bila mafanikio.
“Nawaambia ndugu zangu Chadema imeikamata CCM kweli kweli hadi kufikia hatua ya kutuogopa, safari hii tutabanana na ninawahakikishia hawatoki, tumejipanga kupambana nao. CCM inaogopa sana Chadema ndiyo maana mnasikia kila siku kwamba wanasema chama chetu ni cha fujo, siyo kweli wameona tunakubarika kwa Watanzania roho imeanza kuwadunda,” alisema.
Aliwataka wananchi hao kuwa wanakabiliwa na mtihani mkubwa ambao hivi sasa Watanzania wote wameelekeza macho na masikio yao kwao, kusikia wataamua nini juu ya hatma ya kupata kiongozi atakayewasaidia matatizo yanayowakabili.
“Nimepata taarifa kwamba kuna matatatizo makubwa yakiwemo maji, zahanati na barabara, lazima mfanye maamuzi mazuri, CCM hii ni ya matajiri ambao wanawakumbuka kila uchaguzi unapofika lazima muonyesha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania wameshindwa kumaliza kero zenu.
…Lakini pia nimesikia hapa kuna chakula cha msaada kinagawiwa, hizi ni fedha zenu si za CCM, kama wanavyopita humo wanawadanganya…kama kuna mwanachama wetu yeyote atakayenyimwa atoe taarifa kwa viongozi wetu haraka, kwa sababu ni haki yenu kupata chakula,” alisema.
Endelea kusoma habari hii.................
Wednesday, September 28, 2011
Monday, September 26, 2011
Prof Wangari Maathai afariki dunia
Mtunukiwa wa tuzo ya Amani ya Nobel Prof Wangari Maathai ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 71.
Mwanaharakati huyo mashuhuri wa mazingira na haki za binadamu wa Kenya Profesa Wangari Maathai amefariki dunia mjini Nairobi usiku wa kuamkia , Jumatatu kutokana na maradhi ya saratani.
Prof Karanja Njoroge ambaye ni mkurugenzi wa Green Belt Movement, shirika ambalo Prof Maathai alilianzisha amethibitisha kifo hicho.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Prof Njoroge amesema wakati wa kifo chake Wangari alikuwa na wanafamilia na marafiki.
Marehemu ameacha watoto watatu, wawili wakiume na mmoja wa kike.
Profesa Wangari Maathai alipata tuzo la amani ya Nobel mwaka 2004, kufuatia juhudi za kupigania uhifadhi wa mazingira nchini Kenya.
Mbali ya kuwa Mwanaharakati wa Maswala ya Mazingira na haki za binadamu , Wangari Maathai pia alikuwa mwanasiasa shupavu.
Amewahi kuhudumu kama Mbunge na Naibu waziri wa Mazingira nchini Kenya.
Prof Maathai pia katika uhai wake alipata tuzo mbalimbali za kimataifa kwa kutambua mchango wake.
Prof. Wangari Muta Maathai alianzisha vuguvugu la Green Belt mnamo mwaka 1977, ambapo alifanya kazi na wanawake kote nchini kuboresha maslahi yao na kuhifadhi mazingira.
Alikuwa mtetezi mashuhuri wa matumizi bora ya mali asili .Shughuli zake zilitambuliwa mara kwa mara kote duniani.
Chanzo: BBC

Saturday, September 24, 2011
Liyumba atoka jela
Hatimaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Amatus Liyumba (63), jana aliachiwa huru na Jeshi la Magereza, baada ya kumaliza kifungo chake cha miaka miwili kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi.
Liyumba aliachiwa jana asubuhi baada ya kutumikia kifungo cha miaka miwili alichohukumiwa na jopo la mahakimu wawili kati ya watatu waliosikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na NIPASHE jana majira ya saa 4:42 asubuhi, kwa njia ya simu, msemaji wa jeshi hilo, Kamishna Mwandamizi, Omary Mtiga, alisema kuwa Liyumba aliachiwa baada ya kumaliza kifungo chake mapema saa 3:00 asubuhi na kuongeza kuwa alikuwa huru rasmi nje ya gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.
“Ndiyo Liyumba ameachiwa leo (jana) asubuhi kwa sababu ameshamaliza kutumikia adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili katika gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam,” alisema Kamishna Mtiga.
Mei 24, mwaka jana, mahakimu wawili, Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa kati ya watatu walitoa hukumu iliyomtia hatiani bosi huyo wa zamani wa BoT, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.
Liyumba alituhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 221 kupitia kwenye mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo.
Hukumu ya Hakimu Edson Mkasimongwa ilimuona Liyumba ana hatia katika kosa hilo.
Mbali na kuachiwa huru, Liyumba yuko nje kwa dhamana kwa shtaka la kukutwa na simu gerezani kinyume na kifungu namba 86 kidogo cha kwanza na cha pili cha Sheria ya Jeshi la Magereza.
Ilidaiwa kuwa Julai 27, mwaka huu kinyume cha sheria hiyo ya magereza, Mkurugenzi huyo wa zamani, alikutwa na simu ya mkononi aina ya Nokia 1280 ya rangi nyeusi iliyokuwa inatumia laini namba 0653-004662 pamoja na namba ya utambulisho ya simu (IMEI) 356273/04/276170/3.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alikutwa na simu hiyo katika chumba chake cha magereza bila kuwa na kibali cha kufanya hivyo huku akijua ni kosa.
Mshtakiwa alikana shtaka hilo na mahakama ilimtaka kujidhamini kwa hati ya dhamana ya Sh. 50,000 na mdhamini mmoja ambaye ni mtumishi wa serikali au kutoka kwenye taasisi inayotambulika.
Mshtakiwa alitimiza masharti hayo na mahakama ilimuachia kwa dhamana hadi Septemba 29, mwaka huu.
Friday, September 23, 2011
Waziri amuumbua daktari
NAIBU Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya, ameelezea udhaifu wa utoaji huduma za afya kwa baadhi ya hospitali nchini, baada ya kwenda katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru na kuandikiwa dawa bila kujieleza kwa daktari.
Dk. Nkya alisema hayo wakati akizungumza na menejimenti, wafanyakazi na wanafunzi wa uuguzi na udaktari katika Hospitali Teule ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai, baada ya kupata hati rasmi ya kutambua kupanda hadhi kwa hospitali hiyo.
Huku akiitaja hospitali hiyo, Naibu Waziri alisema alifika hapo bila kujitambulisha huku amejifunika nguo hadi usoni akaingia kwa daktari ambaye hakumtaja jina, lakini daktari huyo alimwandikia dawa bila kumwuliza tatizo lake.
“Niliingia kwa daktari na kabla sijakaa, akaanza kuniandikia vipimo huku akinihoji kama nina homa na shinikizo la damu (BP), nilimjibu nitajuaje wewe ndiye mtaalamu, akanieleza tena natakiwa kupigwa picha za mionzi (X-ray), nilishangaa sana,” alisema.
Alisema kutokana na hali ile, alimweleza daktari husika kwamba anatakiwa amsikilize kabla ya vipimo, lakini katika hali ya kushangaza, alisisitiza kuwa anatakiwa kwenda kupigwa picha za X-ray.
“Niligundua kuwa daktari yule alikuwa amedhamiria na analosema nilijitambulisha kwamba mimi ni Dk. Lucy Nkya, Naibu Waziri … alipatwa mshtuko, nikamhoji kama ndivyo anavyotoa huduma kwa wananchi wa kawaida, nilimwonya nikaondoka,” alisema.
Alisema aliondoka na kuahidi kurejea wakati mwingine bila kutambulika, ili kuangalia mwenendo wa mtumishi huyo kama anatekeleza wajibu wake kulingana na sheria, kanuni na taratibu za utoaji tiba.
Akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo teule, alisema imekuwa miongoni mwa hospitali teule 34 nchini na kuwataka watumishi wake kuzingatia kanuni na taratibu za afya kwa kutoa huduma kulingana na viapo vya taaluma yao.
“Ninyi leo mmepata hati rasmi ya utambuzi kuwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Hai, hakikisheni mnatimiza wajibu wenu … hii sasa ni hospitali ambayo inatoa huduma kwa vigezo vya Serikali, nisingependa kusikia malalamiko dhidi yenu,” alionya.
Aliitaka Halmashauri ya Hai kutohamisha watumishi wa hospitali hiyo kwa namna yoyote na badala yake wajitahidi kukabili changamoto zilizopo ili iweze kutekeleza wajibu wake.
“Sasa Serikali itakuwa ikilipa mishahara na marupurupu kwa watumishi wa hospitali hii, tukisikia halmashauri mnahamisha watumishi au kutumia fedha zinazotumwa ili kufanyia vikao, safari za namna yoyote … tutawachukulia hatua kisheria,” alisema.
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk . Saitore Laizer, aliiomba Serikali ianze kutoa ruzuku ya mishahara, dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa hospitali hiyo, ili wananchi wapate huduma kwa gharama nafuu kama ilivyo kwa hospitali zingine za umma.
Alisema changamoto nyingine ni uhaba wa watumishi unaosababishwa na kuhama kwa watumishi kutoka mashirika ya dini na ya binafsi kwenda serikalini, jambo ambalo limeiathiri hospitali hiyo hususani idara za meno na macho.
Chanzo ; HabariLeo

Thursday, September 22, 2011
Michael Sata ashinda uchaguzi Zambia
![]() |
| Mshindi wa uchaguzi wa Zambia Michael Sata |
Kiongozi wa chama cha Patriotic Front, Micheal Sata ametangazwa kwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Zambia
Tangazo hilo lilitolewa na Jaji Mkuu wa Zambia Ernest Sakala.
Awali watu wawili waliuawa kufuatia ghasia katika maeneo ambayo ni ngome ya upinzani.
Mkuu wa Polisi wa jimbo hilo maafuru kwa uzalishaji Shaba ameliambia shirika la habari la Reuters watu wamejitokeza katika barabara za mji wa Kitwe na Ndola wakivurumisha mawe.
Mwandishi wa BBC anasema ghadhabu hizi zimechochewa na agizo la serikali kupiga marufuku vyombo vya habari kutangaza matokeo bila ya idhini ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC Mutuna Chanda akiwa Lusaka kilomita 300 kusini mwa Kitwe, anasema huko Kitwe, waandamanaji waliteketeza soko moja usiku na Polisi wameweka vizuwizi katika mji wa Wusaikile.
Rais Banda alimshinda Bw Sata kwa kura 35,000 katika uchaguzi wa mwaka 2008, matokeo yaliozusha ghasia kutoka upande wa upinzani katika ngome zao za mijini.
Tangu uchaguzi wa mwaka 2008, watu wengine milioni moja wamejiandikisha kuwa wapiga kura,wengi wao vijana wasio na ajira.
Chanzo: BBC
Upinzani waelekea kushinda Zambia
![]() |
| Bwana Michael Sata |
Hata hivyo, ghasia kubwa ziliripotiwa kuibuka katika Jimbo la Kaskazini mwa Zambia la Ukanda wa Shaba, kwenye ngome kuu ya Sata, kufuatia kusitishwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi, yaliyokuwa yakionyesha kwamba kiongozi huyo anaongoza dhidi ya Rais anayemaliza muda wake, Rupiah Banda.
Matokeo ya awali ya uchaguzi huo uliofanyika Jumanne wiki hii, yalitangazwa jana jioni na Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo, yakionyesha kuwa Sata alikuwa akiongoza kwa kura 639,787 dhidi ya 542,362 za Banda, ambaye ni kiongozi wa Chama cha The Movement for Multi-party Democracy (MMD) kilichotawala taifa hilo tangu 1991.
Matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia, Irene Mambilima yalikuwa ni yale yaliyokusanywa katika majimbo 85 kati ya 150.
Hatua ya kusitishwa kwa matokeo yaliyokuwa yakimpa matumaini Sata (74) maarufu kwa jina la "King Cobra" kutokana na kauli zake kali, kumezusha ghasia kubwa kutokana na kuwapo kwa hisia za wizi wa kura.
Wakati matokeo ya uchaguzi huo yakisubiriwa kwa hamu, Mahakama Kuu ya nchi hiyo imevizuia vyombo vya habari kutangaza matokeo kabla ya kutolewa na Tume ya Uchaguzi.
Amri ya Mahakama Kuu ilitolewa kufuatia ombi lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zambia. Jaji wa Mahakama Kuu, Jane Kabuka, alisema wanavizuia vyombo vya habari kutangaza au kuchapisha matokeo yasiyo rasmi hadi yapate idhini ya Tume ya Uchaguzi.
Katika toleo lake la juzi, gazeti binafsi la The Post lilikuwa na kichwa cha habari kuwa Satta ameshinda uchaguzi huo. Na hata baada ya pingamizi hilo la Mahakama Kuu, jana tena gazeti hilo liliandika kuwa kiongozi huyo wa upinzani anaongoza kwa 59%.
Hatua hiyo ya Mahakama Kuu imekuja huku Tume ya Uchaguzi ikisema kuwa wezi wa mitandao wameingilia mtandao wao na kuweka matokeo ya uongo yanayoonyesha kuwa kiongozi wa chama cha upinzani cha Patriotic Front, Satta, anaongoza.
Msemaji wa Tume hiyo, Cris Akufuna, alisema kutokana na hitilafu hiyo maofisa wake wanafanya kazi kuhakiki zaidi ya mara mbili matokeo kutoka maeneo mbalimbali.Alisema mchakato huo umesababisha kuchelewa kutolewa kwa matokeo, hali ambayo imeanza kuzua hofu ya kwamba matokeo ya uchaguzi huo yamefanyiwa hila.
Katika maeneo kadhaa tayari washabiki wa kiongozi huyo wa upinzani wameanza kusherehekea wakiamiani kuwa kiongozi wao ameshinda.Rais Banda anatarajiwa kupata kura nyingi katika maeneo ya mikoani, ambako kuna uwezekano wa matokeo kutolewa taratibu, kuliko maeneo ambayo ni ngome ya upinzani, ambayo ni mji mkuu Lusaka na maeneo ya Ukanda wa Shaba, ambako ndiko kitovu cha uchumi wa Zambia.
Hata hivyo, kwa mujibu wa duru za habari ni mapema mno kusema iwapo Satta, yuko katika nafasi nzuri ya kushinda na kukiondoa madaraka chama tawala kwa mara ya kwanza tokea kumalizika kwa mfumo wa chama kimoja mwaka 1991.Akufuna alisema bado wanaendelea kupokea matokeo kutoka maeneo mbalimbali na kwamba mpaka itakapofika leo jioni watatangaza matokeo rasmi.
Vurugu mpaka Mbeya
Mpaka wa Zambia na Tanzania katika eneo la Tunduma mkoani Mbeya umefungwa upande wa Zambia kutokana na vurugu zinazoendelea maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Maeneo hayo ni pamoja na mji wa Nakonde katika mpaka huo upande wa Zambia, ambako magari yanadaiwa kupigwa mawe.
Habari kutoka ndani ya vyombo vya usalama Mkoa wa Mbeya zinadai kuwa katika mji huo unaopakana na Tunduma, kumezuka vurugu ambapo wananchi wa Nakonde wamekuwa wakifanya vurugu kwa kupiga mawe magari, huku polisi nao wakituliza vurugu hizo kwa kurusha mabomu ya machozi.
"Vurugu hizi zipo mpakani upande wa Zambia kwani hata wenzetu Zambia wameamua kufunga mpaka, lakini siyo kiofisi ni kienyeji kwa ajili ya kuzuia vurugu zisiweze kuvuka upande wetu wa Tanzania na kuepusha mali, yakiwamo magari kuharibiwa na vurugu hizo,"inadai taarifa hiyo.
Taarifa hizo zilisema kuwa, magari yaliyopigwa mawe ni pamoja na basi aina ya Taqwa linalofanya safari zake kutoka Tanzania kwenda Zambia na lori la mkoani Iringa la kampuni ya Asasi ambapo yalipigwa mawe yakiwa mpakani upande wa Zambia.
Aidha, kwa upande wa Tanzania katika mji wa Tunduma hakuna kinachoendelea, kwani malori yote yaliyopo Tunduma yamezuiwa kuvuka mpaka hadi hapo vurugu hizo zitakapotulia.
Chanzo: Mwananchi
Wednesday, September 21, 2011
Msuya aonya Serikali isicheze na mgawo umeme
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya ameitahadharisha Serikali kuwa makini
na suala la mgawo wa umeme ambao amesema unaongeza ugumu wa maisha kwa
wananchi, kwani unaweza kusababisha matatizo makubwa kiasi cha nchi
kushindwa kutawalika.“Hali ikiendelea hivi tusishangae kutokea kwa mambo
kama yaliyotokea kwa nchi za Kiarabu ambazo wananchi wake wameshindwa
kuvumilia ugumu wa maisha na kuamua kuandamana.” Msuya alitoa tahadhari
hiyo, Dar es Salaam jana wakati wa mjadala wa kitaifa kuhusu
miundombinu, nishati na madini kwenye Wiki ya Maonyesho ya Miaka 50 ya
Uhuru yaliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Angalizo la Msuya inakuja kipindi ambacho nchi ipo katika mgawo wa umeme kutokana na uhaba mkubwa wa nishati hiyo hali ambayo inaathiri sekta mbalimbali za uzalishaji na watumiaji wa kawaida.
Msuya alikuwa Waziri Mkuu kati ya Novemba 7, 1980 hadi Februari 24, 1983 na kushika tena wadhifa huo Desemba, 1994. Pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha, Viwanda katika vipindi tofauti.
Ili kukabiliana na tatizo hilo, Serikali kupitia kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ilitangaza mpango wa dharura wa Sh1.2 trilioni kukabiliana na mgawo, lakini hadi sasa hakuna mabadiliko yoyote yanayoonekana tangu ulipoasisiwa Agosti, mwaka huu.
Kauli ya Msuya
Msuya alisema Tanzania inahitaji uchumi unaokua na kwamba Serikali isipoangalia, tatizo la kushindwa kukua kwa uchumi, maendeleo ya nchi hayatafanikiwa. “Kabla ya uhuru idadi ya watu ilikuwa milioni nane na sasa tuko zaidi ya watu 53 milioni, kuna haja ya kuwa na uchumi unaokua badala ya kuzalisha bila mafanikio, Serikali iwe makini katika kuimarisha mambo muhimu kama nishati,” alisema na kuongeza:
“Serikali inatakiwa kufikiri juu ya kuimarisha masuala ya umeme nchini wakati wawekezaji wanapoingia ili kusaidia uchumi kukua haraka na kuepusha kutokea kwa mambo yaliyozikumba nchi za Kiarabu.” Ingawa hakuzitaja nchi hizo, lakini Misri, Tunisia, na Yemen ndizo zilikumbwa na maandamano kupinga hali ngumu ya kiuchumi na kusababisha viongozi wa Misri na Tunisia na kung’olewa madarakani.
Msuya alisema Serikali ina jukumu la kuimarisha mazingira yatakayoendeleza uchumi na kwamba ipo changamoto kubwa ya kuziunganisha sekta binafsi ili kuinua uchumi. “Tatizo ni namna Serikali itakavyokubaliana na sekta binafsi katika kuimarisha uchumi wake na kuwainua wananchi kibiashara kwa sababu miundombinu ya uzalishaji hasa umeme bado haijasambaa katika mikoa yote,” alisema.
Alisema Serikali itakapoiunganisha mikoa 26 katika kuzalisha biashara na kuipatia nguvu ya umeme, itakuwa njia mojawapo ya kuimarisha mafanikio ya kila mwananchi na kuondokana na umaskini. “Sasa hivi tunaambiwa kuwa kuna fungu la fedha la kutekeleza kilimo, lakini bado kuna maswali mengi ya kujiuliza juu ya uwezeshwaji wa kilimo, kwa sababu maeneo ya vijijini ambayo ndiyo yanayojishughulisha na kilimo hayana umeme, Kilimo Kwanza kitatekelezwaje?,” alihoji Msuya. Msuya alisema, ipo haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya kiutendaji ya halmashauri mikoani ili kila mkoa uunganishiwe umeme kirahisi.
Kauli ya Ngeleja
Ngeleja akizungumza kwenye hafla hiyo alisema, Serikali imetoa fursa kwa sekta binafsi kuwekeza hasa katika masuala ya nishati ili kuzalisha, kusambaza na kusafirisha.Alisema sekta binafsi imepewa jukumu hilo ili kuzalisha zaidi na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kiwango kinachotakiwa na kuboresha miundombinu yake.
“Tangu Serikali ilipofanya mageuzi ya kisera katika uendeshaji uchumi wa nchi, sekta binafsi imekuwa ikiongezewa nguvu ya biashara hivyo ni vyema sekta hiyo ikatumia fursa ya kuwekeza zaidi katika sekta muhimu na kuzingatia sera ya nishati ya mwaka 2008,” alisema.
Alisema matatizo ya umeme yaliyopo yanatokana na mfumo wa kuunganisha umeme na kiwango kikubwa kinachopotea kutokana na usambazaji kuanzia katika chanzo cha umeme.
“Uwekezaji mdogo katika umeme unaochukua muda mrefu pia ni chanzo kikubwa katika kuchangia umeme, tozo zinazotozwa hazikidhi mahitaji yaliyopo na gharama kubwa za mafuta katika soko la dunia zinaongeza gharama za uzalishaji,” alisema. Akizungumzia tatizo la mgawo wa umeme, Ngeleja alisema uchumi wa nchi umeporomoka kwa asilimia 6.9 na kuwa megawati 236 za mgawo huo kwa siku moja zinagharimu Dola za Marekani 400 milioni (takriban Sh500 bilioni).
Mgawo wa umeme umekuwa ukiitikisa nchi zaidi tangu mwaka 2006 na hadi sasa Serikali imekuwa na mipango mingi ukiwamo ule uliopitishwa na Bunge hivi karibuni, kuonekana kukosa tija. Katika mpango huo wa dharura, Serikali ilitangaza kuwa itatumia kiasi hicho cha Sh1.2 trilioni kwa ajili ya mpango huo wa ili kunusuru uchumi wa nchi kuanzia Agosti hadi Desemba mwaka huu na Januari hadi Desemba mwakani.
Wiki moja iliyopita, Waziri Ngeleja alitoa ahadi ya kupungua makali ya mgawo huo lakini hadi sasa, hakuna nafuu iliyojitokeza.

Wednesday, September 14, 2011
Rais Kikwete ateua wakuu wapya wa mikoa 15
RAIS Jakaya Kikwete amewateua wakuu wa mikoa wapya 15, kuwabadilisha
vituo vya kazi wakuu wa mikoa watano huku wengine saba wakielezwa kwamba
wamestaafu kwa mujibu wa taratibu. Katika uteuzi huo, wa wakuu wa mikoa
21, kati yao 11 walikuwa wakuu wa wilaya na ni Perseko Ole Kone pekee
aliyebaki katika kituo chake cha kazi cha Mkoa wa Singida.
Mbali ya idadi kubwa ya wakuu wa wilaya waliopandishwa vyeo, katika uteuzi huo, Rais Kikwete pia amewateua waliokuwa Manaibu Waziri watatu, Mwantumu Mahiza, Ludovick Mwananzila na Joel Bendera, kuwa wakuu wapya wa mikoa.
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotolewa Dar es Salaam jana iliwataja wakuu hao wa wilaya waliopandishwa vyeo na mikoa yao katika mabano kuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, John Tupa (Mara), DC wa Morogoro, Saidi Mwambungu (Ruvuma), Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Gallawa (Tanga), DC wa Ilala, Leonidas Gama (Kilimanjaro), DC wa Newala, Dk Rehema Nchimbi (Dodoma), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Elaston Mbwillo (Manyara).
Wengine ni DC wa Karagwe, Kanali Fabian Massawe (Kagera), DC wa Mvomero, Fatma Mwassa (Tabora), DC wa Manyoni, Ali Rufunga (Lindi), DC wa Kilombero, Mhandisi Ernest Ndikillo (Mwanza), DC wa Bagamoyo, Magesa Mulongo (Arusha). Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Stella Manyanya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Katika uteuzi huo, Mahiza anakwenda Mkoa wa Pwani, Bendera ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mwananzila Shinyanga. Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Mahiza alikuwa ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Mwananzila huku Bendera akiwa ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.
Waliobadilishwa vituo vya kazi ni Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza, Said Mecky Sadiki anayehamia Dar es Salaam akitokea Lindi, Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma, Luteni Kanali Issa Machibya kutoka Morogoro kwenda Kigoma na Kanali Joseph Simbakalia anakwenda Mtwara akitokea Kigoma.
Wakuu wa mikoa waliostaafu ni Mohammed Babu aliyekuwa Kagera; Isidore Shirima (Arusha), Kanali Anatory Tarimo (Mtwara), John Mwakipesile (Mbeya), Kanali Enos Mfuru (Mara), Brigedia Jenerali Dk Johanes Balele (Shinyanga) na Meja Jenerali Said Kalembo (Tanga).
Wakuu wa wanne wa mikoa waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni Amina Mrisho aliyekuwa Pwani, Dk James Msekela aliyekuwa Dodoma, Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Daniel Ole Njoolay wa Rukwa.
Taarifa hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu imesema: “Wakuu wa mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika watatangazwa baadaye.”
Taarifa hiyo iliongeza: "Wakuu wote wa mikoa waliopo sasa wameagizwa kuandaa hati za makabidhiano katika muda wa siku 14 kuanzia siku ya kuapishwa kwa wakuu wapya wa mikoa. Aidha, wakuu wa wilaya ambao wamepandishwa vyeo kuwa wakuu wa mikoa nao wanapaswa kufanya hivyohivyo kwa ajili ya wakuu wa wilaya watakaopangiwa vituo vitakavyokuwa vimeachwa wazi kutokana na uteuzi wao.”
"Makabidhiano hayo lazima yahusishe pia kutembelea kwa pamoja baadhi ya maeneo na miradi ambayo ni muhimu kama sehemu ya makabidhiano yao," ilisisitiza taarifa hiyo na kuongeza:
"Wakuu wote wa mikoa walioteuliwa na wakuu wa mikoa minne mipya watakaoteuliwa pamoja na wakuu wote wa wilaya watakaoteuliwa baada ya zoezi kukamilika watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya wiki tatu kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kiuongozi na kiutendaji.”
Wakuu hao wapya wa mikoa wataapishwa na Rais Kikwete kesho saa 4.00 asubuhi kwenye Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Monday, September 12, 2011
Miss Universe 2011 ni Leila Lopes Kutoka Angola
![]() |
| Miss Universe 2011 Leila Lopes |
Lopez, alikuwa katika la watu watano walioweza kufika katika fainali za mashindano hayo. Wengine walikuwa ni kutoka China, Brazil, Philippines, Ukraine na Panama.
Nchi zilizoingia katika kumi bora ni Australia, Costa Rica, France, Ukraine, Portugal, Panama, Philippines, Angola, China na Brazil.
Lopez ameweza kuwashinda washiriki wengine 88 kutoka nchi mbambali duniani zilizoshiriki mashindano hayo ikiwamo Tanzania.
Mashindano hayo yalikuwa ni ya 60 kufanyika tangu yaanzishwe 1952.
Boma la mafuta lalipuka Kenya na kuua zaidi ya 100
![]() |
| Waokozi wakisaidia watu baada ya Bomba kulipuka mjini Nairobi |
Zaidi ya watu mia moja wamekufa baada ya bomba la
mafuta kupasuka na kulipuka katika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi,
polisi wamesema.
Bomba hilo la mafuta limepita katika makazi ya watu wengi kwenye mitaa ya mabanda katikati ya mji wa Nairobi na Uwanja wa ndege.
Zaidi ya majeruhi 100 wamepelekwa hospitali, maafisa wanasema.
Msemaji wa magari ya huduma za dharura alisema waathirika wengi waliungua kiasi cha kutokufatambulika.
Taarifa zinasema mlipuko huo huenda umesababishwa na kishungi cha sigara kilichotupwa katika mtaro wa maji ambao ulikuwa ukielea mafuta.
Mafuta hayo yalivuja kutoka kwenye tangi moja katika ghala linalomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Kenya, msemaji wa polisi Charles Owino ameliambia shirika la habari la Reuters.
‘Miili yaelea
Polisi na jeshi wameweka vizuizi katika eneo hilo, ambapo wakazi walisema kuvuja kwa mafuta kwenye bomba hilo na kusababisha watu wengi kukimbilia kuchota mafuta yaliyovuja.
"Kulikuwa na sauti kubwa ya mlipuko, mlipuko mkubwa, na moshi na moto ukiwaka juu angani," mkazi mmoja Joseph Mwego aliliambia shirika la habari la AFP.Sehemu ya miili ilionekana ikiungua kiasi cha mita 300 (futi 1,000) karibu na eneo la tukio, wenyeji walisema.
Miili mingine likuwa inaelea katika mto karibu na eneo hilo ambapo watu walioungua iliripotiwa waliruka baada ya kushika moto.
Vibanda vilivyoezekwa kwa mabati vimejengwa karibu kabisa na bomba hilo, wakazi walisema.
Kumekuwa na vifo vingine ambavyo vimetokana na watu kuchota mafuta yanayovuja: Zaidi ya watu mia moja walikufa eneo la Molo, magharibi mwa Kenya mwaka 2009 baada ya lori la mafuta kupinduka na moto kulipuka.
Chanzo: BBC
Saturday, September 10, 2011
Ajali ya meli Zanzibar: Mamia wafariki
Watu wasiopungua 187 wamekufa baada ya meli iliyokuwa
imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na
watu takriban 800.
Inadhaniwa kuwa meli hiyo ilizama baada ya injini yake kukosa nguvu.
Shughuli za uokoaji zilikwazwa kwa kuwa meli hiyo ilizama usiku.
Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo, lakini watu 325 walionusurika wameokolewa, kwa mujibu wa waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar.
Meli hiyo, MV Spice Islander ilikuwa ikisafiri kati ya Kisiwa kikuu cha Unguja kuelekea Pemba.
Meli hiyo ilikuwa ikirejesha watu baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.
Msaada
Mamlaka za huko zimezidiwa na tukio hilo na zimeomba msaada kutoka nje.
Serikali ya Zanzibar imeunda kituo cha uokoaji na kutoa wito kwa taasisi zote kusaidia katika shughuli za uokozi. Serikali hiyo pia imeomba msaada kutoka nchi nyingine za nje, kama vile Kenya na Afrika Kusini.
Walionusurika walichukuliwa na boti za kibinafsi na kupelekwa katika bandari ya Zanzibar, amekaririwa kamishna wa polisi wa Zanzibar Mussa Hamis.
Miili ya watu imekuwa ikisukumwa katika pwani ya Zanzibar na mawimbi. Mpaka sasa miili ya watu 100 wamepatikana, amesema mwandishi wa BBC Ali Saleh akiwa Zanzibar.
Maelfu ya ndugu na jamaa wanasubiri kusikia taarifa za ndugu zao ambao walikuwa ndani ya meli hiyo, anasema mwandishi wetu.
Mohhamed Aboud, waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar anasema watu 259 walionusurika wameokolewa lakini 40 kati yao wamejeruhiwa sana.
Catherine Purvis, mtalii kutoka Uingereza aliyepo Zanzibar, akisubiri boti ya kwenda Dar es Salaam amesema ameshuhudia miili ya watu wengi ikitolewa ndani ya maji.
"Nimesimama katika bandari ya Zanzibar nikiwa na watalii wengine kama 10 wa Marekani na Uingereza.
"Boti yetu imechelewa kwa sababu wanatumia vyombo vyote vya baharini kuokoa watu".
Rubani mmoja wa helikopta Kapteni Neels van Eijk alipita juu ya eneo la tukio.
"Tuliona walionusurika wakiwa wameshikilia magodoro na majokofu au chochote kile kinachoweza kuelea. Ni vigumu kusema idadi kamili, lakini naweza kusema walikuwepo zaidi ya watu 200 walionusurika ndani ya maji na miili ya watu pia," ameiambia BBC.
"Wakati huo, kulikuwa na boti chache zilizofika katika eneo hilo. Walikuwa wakitafuta walionusurika, ingawa bahari haikuwa imechafuka sana, mawimbi walikuwa makubwa, kwa hiyo ilikuwa vugumu kuona walionusurika.
"Tulirusha ndege yetu na kuziongoza boti hadi kwa watu walionusurika ili waweze kuwachukua. Kulikuwa na miili kadhaa ndaniya maji."
Meli hiyo iliondoka Unguja takriban saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki na inadhaniwa kuwa ilizama majira ya saa saba usiku.
Ilikuwa imebeba abiria wengi kiasi kwamba baadhi ya abiria waligoma kupanda, amekaririwa abiria mmoja aliyenusurika Abdullah daid, akizungumza na shirika la habari la AP.
Chanzo: BBC
Friday, September 9, 2011
Hatimaye BAE yakubali kuilipa Tanzania fedha za Rada
Kampuni ya kutengeneza silaha za kijeshi ya Uingereza
BAE Systems, hatimaye imekubali kuilipa moja kwa moja serikali ya
Tanzania dola milioni 47.
Uamuzi huo unahitimisha mvutano wa muda mrefu kuhusu ununuzi wa rada hiyo ambao ulifanyika katika mazingira ya rushwa na kusababisha mahakama nchini Uingereza kuamuru fedha hizo zirejeshwe Tanzania
Kampuni ya BAE Systems ilishutumiwa na wabunge wa Uingereza kwa kujivuta kutekeleza amri ya mahakama iliyotolewa zaidi ya mwaka mmoja uliopita .
Serikali ya Uingereza ilisema imeiambia BAE kuwa hawana budi kulipa malipo hayo na kutarajia kuwa suala hilo lingefikiwa muafaka kwa faida ya watanzania.
Awali katika taarifa yake rasmi BAE ilisema inafanya kazi na serikali ya Uingereza kupitia wizara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) kutoa malipo hayo kulingana na utaratibu wao.
BAE haikuwa tayari kuilipa serikali ya Tanzania fedha hizo na ilitaka ilipe kupitia misaada yake kwa mashirika ya hisani ya Uingereza yanayofanya kazi nchini Tanzania.
Akizungumza na BBC Idhaa ya Kiswahili kutoka Kongwa Dodoma, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai alisema ‘huku Tanzania tumeupokea uamuzi huo kwa furaha kubwa sana sana sana, kwa sababu ni jambo ambalo kwa upande wetu tukuwa tunaona kuwa si haki na kwa kuwa sasa fedha hizo zinarudi Tanzania,
‘Ni matumaini yetu kuwa fedha hizi zitatumika vizuri, kupitia serikali yetu kwa manufaa ya watanzania wote kama ilivyokusudiwa.’ Aliongeza Bw Ndugai.
Naibu Spika Job Ndugai miezi michache iliyopita aliongoza ujumbe wa wabunge wa Tanzania mjini London kufuatilia malipo hayo, baada ya kutokea mvutano wa muda mrefu kati ya serikali Tanzania na kampuni hiyo ya BAE.
Chanzo: BBC
Thursday, September 8, 2011
Chadema yazindua kampeni, Mkapa atua Igunga
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezindua kampeni zake za kuwania Jimbo la Igunga huku Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, akiwataka wananchi kumchagua mgombea wa chama hicho, Joseph Kashindye ili alinde rasilimali za wana Igunga.
Wakati Chadema wakizindua kampeni hizo kwa mtindo wa kumwaga tuhuma na kashfa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais wa Awamu ya Tatu, alitua Igunga tayari kwa uzinduzi wa kampeni za chama hicho na kuelezea furaha aliyonayo ya kusafiri kwa lami kutoka Dar es Salaam hadi Igunga.
Katika uzinduzi wa Chadema, Dk. Slaa aliwataka wananchi waliokuwa wamefurika katika Uwanja wa Sokoine mjini hapa, kumchagua Kashindye ili alinde rasilimali hizo na kupunguza aliowaita panya wanaozitafuna.
Alidai kuwa mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, hawezi kuleta mabadiliko yoyote Igunga na kwa Taifa kutokana na alichoita kuwepo kwa mfumo mbovu wa CCM katika kusimamia maslahi ya wananchi.
Dk. Slaa alisema kuwa nchi inahitaji kutetewa na makamanda, ili ifanikiwe kwa kuwa CCM imeshindwa kazi ya kuwasaidia wananchi.
Aliwaambia polisi aliowaita wanaoagizwa kuwapiga mabomu wananchi, wasifanye hivyo kwa kuwa kazi ya Chadema, ni kuwatetea polisi wa vyeo vya chini ambao alidai wanapewa posho ndogo isiyokidhi mahitaji yao.
Naye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kazi hivyo haifai kuwa madarakani wala kuongezewa wabunge kwa kuwa itazidi kuwadidimiza wananchi.
Kwa upande wake Kashindye alijinadi mbele ya wananchi hao kuwa wakiona mwalimu anaachia chaki na kwenda kwenye siasa, basi wajue hali ni mbaya kwa kuwa Taifa linahitaji ukombozi.
“Hata Mwalimu Nyerere (Baba wa Taifa Mwalimu Julius), aliachia chaki alipoona hali ni mbaya na akaamua kuingia kwenye siasa na kuikomboa Tanzania tunayoishi leo,” alisema.
Alidai kuwa CCM wanadhani kuwa watumishi wa Serikali ni mali yao kitu ambacho si kweli na ameamua kuingia Chadema ili awatetee wananchi wa Igunga na Taifa kwa ujumla.
“CCM ni chama kinachokufa nisingeweza kuondoka na kuingia CCM kuwa mbunge wa kusinzia kwa kuwa hawana hoja,” alidai.
Alidai kuwa fedha nyingi za kujenga barabara zimeliwa kitu ambacho kimesababisha wananchi kuteseka kutokana na mfumo mbovu wa CCM.
“Nawaombeni mnitume niende huko bungeni niende nikawe Spika ya Igunga; nikaseme yote na tupate mafanikio wote,” alisema.
Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Susan Kiwanga alisema ni lazima Igunga wahakikishe chama hicho kinashinda kwa kumchagua Kashindye ili awatetee bungeni.
Alisema, ataweka kambi Igunga na kuhakikisha chama hicho kinashinda kwa kuwa Chadema ni chama cha kutetea wanyonge ambao wamekuwa wakinyonywa na CCM kwa miaka nenda rudi.
Mkapa atua Igunga Lakini Mkapa baada ya kutua Igunga, aliweka bayana kuwa amefika kupambana na kumnadi mgombea wa CCM kwa kuwa anajisikia faraja na matunda ya CCM yakiwemo kutembelea barabara ya lami kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza.
Akiwahutubia wananchi katika Kitongoji cha Makomero alisema kuwa ni muhimu kwa wana Igunga kupuuza vyama vingine kwa kuwa CCM ikitoa ahadi, inatimiza na viongozi wake ni makini.
“Kazi yetu ni moja tu, kila mtu ahakikishe Dk. Kafumu anashinda na kila mtu ambaye amejiandikisha aende kupiga kura ili mambo yawe poa,” alisema Mkapa.
Chanzo: HabariLeo

Mbuzi mwenye miguu nane azaliwa Bunda
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mbuzi mmoja katika Kijiji cha Nafuba kilichoko Kata ya Nansimo wilayani hapa, amezaa mapacha huku mmojawao akiwa na miguu minane, mikia miwili na kichwa kimoja.
Habari zilizopatikana kutoka kijijini hapo na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kilomo, kulikotokea tukio hilo, Fabian Kamanyi zinasema tukio hilo la kustaajabisha lilitokea jana mnamo saa 1:45 asubuhi wakati mbuzi huyo aliyekuwa ametimiza miezi tisa ya ujauzito wake kuzaa mapacha hao kikiwamo kiumbe hicho ambacho hata hivyo kilikufa saa mbili baadaye.
Fabian alisema kabla ya kuzaa mbuzi huyo ambaye hiyo ni mara yake ya tatu kuzaa usiku, alikuwa akilia kama ishara ya kutaka kuzaa hali iliyomfanya mmiliki wake Silvanus Bernado, asubuhi yake kumtenganisha na wenzake kwa kumfunga jirani na nyumbani ili ampatie uangalizi wa pekee.
Alisema hatimaye ulipotimia muda wake wa kuzaa (usiku), mbuzi huyo alizaa mapacha hao akiwamo huyo mmoja wa ajabu ambaye alikuwa wa kwanza kuzaliwa akiwa haonyeshi jinsi ya aina yoyote tofauti na mwenzake ambaye alikuwa ana jinsi ya kiume.
Ingawa mwenye mbuzi huyo (Bernado), alilielezea tukio hilo kama kitu cha kawaida, lakini baadhi ya wakazi wa kijiji hicho ambacho ni moja ya Visiwa ndani ya Ziwa Victoria eneo la Wilaya ya Bunda wanaliona kama moja ya matendo ya ushirikina hali iliyosababisha wazee wa kisiwa hicho kulikemea kwa kumtaka aliyefanya hivyo aache mara moja.
Kwa upande wake daktari wa mifugo wa wilaya hiyo, Dk Ndyanabo Tibaijuka alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo licha ya kusema hakuwa hajapata taarifa rasmi, lakini alisema kama limetokea ni jambo la kawaida katika maisha ya viumbe linalojitokeza wakati wa hatua za awali za uchanga wa mimba pindi viungo mbalimbali vya mwili vinapogawanyika ili kujiumba katika umbo linalotakiwa.
“Sijapata taarifa rasmi za tukio hilo; lakini kama limetokea hilo ni jambo la kawaida linalotokea katika hatua za awali za uchanga wa mimba viungo vinapojigawanyisha,”alisema Dk Ndyanabo.

Wednesday, September 7, 2011
Wakutwa na heroine za bilioni 4/-
JESHI la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, limewakamata watu watano akiwemo raia wa Iran, Ali Mirzael Pirbaksh, kwa tuhuma za kukutwa na kilo 97 za dawa hizo aina ya heroine zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 4.4.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo hicho Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Godfrey Nzowa, alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na taarifa walizopewa na raia wema.
Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Said Mrisho (31) wa Tandale, Aziz Kizingiti (32) wa Magomeni Mapipa, Abdul Lukongo (36) wa Kariakoo na Hamidu Karimu (43), wa Tandale.
Nzowa alisema watuhumiwa hao waliokuwa wamepakia dawa hizo ndani ya magari mawili, Toyota Carina namba T 954 BGT na Caldina namba T 107 BAS, walikamatwa jana saa 9.30 alifajiri eneo la Afrikana Mbuyuni, Kinondoni.
“Baada ya mimi kupewa taarifa za watu hao, nilichukua vijana wangu na kuwafuatilia taratibu katika maeneo waliyokuwa wakienda na hatimaye kuwakamata eneo hilo,” alisema Nzowa.
Alisema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao, isipokuwa raia huyo wa Iran, ambaye ndiye anadaiwa kuingiza dawa hizo nchini, walidai kuwa zilikuwa mali ya Pirbaksh, ambaye hata hivyo hakuhojiwa baada ya kukosekana mkalimani.
Nzowa alisema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi wa tukio hilo utakapokamilika, huku akiwataka wananchi wanaojihusisha au kutumiwa kufanya biashara hiyo kuacha, ili kuepuka mkono wa sheria.
Aidha, aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wanaolipa Jeshi hilo katika kupambana na biashara hiyo haramu, huku akiwataka kuendelea kudumisha uhusiano huo hadi mapambano hayo yatakapofanikiwa.

Monday, August 29, 2011
Familia ya Gaddafi yatorokea Algeria
![]() |
| Mke wa Kanali Gaddafi wanawe wa kiume na binti yake |
Mke na watoto watatu wa kiongozi wa Libya aliye mafichoni Muammar Gaddafi wako nchini Algeria, maafisa wa Algerian wamesema.
Balozi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa amesema walipokelewa kwa misingi ya kibinadamu.
Waasi wa Libya wamesema kuwapa hifadhi familia ya Gaddafi ni kitendo cha uchokozi, na wametaka warejeshwe nchini Libya.
Haijulikani mahali alipo Kanali Gaddafi.
Wakati huo huo waasi wamesema mtoto mwingine wa kiume wa Kanali Gaddafi, Khamis, huenda aliuawa katika mapigano karibu na Bani Walid.
Taarifa hizo zimetolewa wakati waasi wa Libya wakijaribu kumaliza upinzani uliopo katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo yanayomtii Gaddafi, na kujiandaa kuendelea kwenda katika mji aliozaliwa kanali Gaddafi wa Sirte ili kumalizia upinzani unaonekana kuwa ngome yake ya mwisho.
Kuwasili kwa mke wa kanali Gaddafi na watoto watatu nchini Algeria kuliripotiwa Umoja wa Mataifa na kwa viongozi wa waasi wa Libya, wizara ya mambo ya nje ya algeria imesema katika taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la Algeria, APS.
Taarifa hiyo imesema familia ya Gaddafi walivuka mpaka kati ya Libya na Algeria Jumatatu, saa Mbili na dakika arobaini na tano za huko.
Algeria ni mahali dhahiri pa kukimbilia familia ya Gaddafi kutokana na nchi mbili hizo kuwa na mpaka mrefu na serikali ya Algeria bado halijalitambua Baraza la Mpito la Taifa la Libya.
Source: BBC
Sunday, August 28, 2011
Wananchi wamepoteza imani na CCM-Msekwa
Via Majira
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Pius Mseka, amekiri wananchi kupoteza imani na chama hicho, kutokana na
matukio mbalimbali yanayojitokeza, huku viongozi wa chama na serikali wakishindwa kuchukuliwa hatua.
Pia alisema kutokana na hali hiyo, ndio maana katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010, CCM ilipata ushindi wa asilimia 61 ikilinganishwa na asilimia 82 ambazo chama hicho kilipata mwaka 1995.
Bw. Msekwa, alitoa kauli hiyo jana wakati akuhojiwa na kituo cha televisheni cha Star Tv katika kipindi cha Medani za Siasa na Uchumi.
Alisema chama tawala kinapaswa kutambua kuwa kina wajibu wa kutimiza majikumu yake sasa, kwani inapofika mahala chama kikasahau wajibu wake wananchi wana haki ya kutokukichagua.
"Ili chama kichaguliwe ni lazima kioneshe kwa vitendo nia na malengo ya kutimiza wajibu kwa wananchi, ili waweze kukiamni," alisema.
Bw. Msekwa alisema kiongozi yoyote anayeficha ukweli kwamba wananchi wamepoteza imani na CCM, mtu huyo hayuko makini na hatakiwi kuendelea kuwa mwanachama.
Alisema kuwa kutokana na mambo yanavyoendelea na viongozi wa serikali kushindwa kuchukua hatua ni chanzo cha wananchi kupoteza imani na chama.
Aliongeza kwa kutambua hilo, ndio maana chama kimekuja na dhana ya kujifua gamba kwa kuwataka wanaotuhumiwa kukipotezea mwelekeo chama hicho, wajiondoe wenyewe.
Hata hivyo alijigamba kwamba vyama vya upinzani kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kilipata wabunge wengi bungeni kutokana na wanachama wa CCM waliokuwa wanagombea ubunge kuachwa katika kura za maoni na kukimbili upinzani.
"Ni kweli kabisa kuna baadhi ya makosa tulifanya kwa kuwapitisha wagombea wasiokubalika kwa wananchi na wale waliokubalika tuliwaacha na wao kuhamia CHADEMA na ndio hao wameshinda," alisema Bw.Pius.
Alisema vya upinzani havikuwa na uwezo wa kuwashawaishi wananchi ili wavichague, bali ilitokana na nguvu ya CCM kwa kuwa wananchi walikuwa na imani na CCM na ndio maana walichaguliwa kupitia mgongo wa CCM.
Aliongeza kuwa CCM iliwaacha watu hao waliokimbilia vyama vya upinzani kwa kuwa CCM ilikwishawabaini kwamba si watu wema ndani ya chama.
Bw. Msekwa alisema si jambo jema kwa wananchi kuelekeza matatizo yote yanayotokea hivi sasa kwa chama cha mapinduzi japo kinashika dola.
Alisema kiwango cha uadilifu kwa watendaji kwa sasa kimepungua tofauti na zamani, kwa kuwa zamani kulikuwa na chama kimoja na watendaji pia walikuwa waaminifu sana tofauti na sasa.
"Zamani uadilifu ulikuwa mkubwa kwa watendaji kwa kuwa kulikuwa na mfumo wa chama kimoja na wanachama wote macho yao yalikuwa yakilinda uadilifu tofauti na sasa", alisema.
Alisema watu wanaotakiwa kujivua gamba wapo kwenye ngazi zote.
Akizungumzia suala la makundi ndani ya chama, alisema hali hiyo inatokea wakati wa kura za maoni, ambapo majungu yanaanzia hapo na siri nyingi kuvuja na hatimaye wale walioachwa kuanzisha makundi na kuwashawishi wanachama kutowapigia kura waliopitishwa.
Alisema wanapaswa kukaa chini na kutafuta njia za kuondoa makundi ndani ya chama. "Changamoto si kuyafumbia macho kwa kuwa yasipofanyiwa kazi yatapeleka chama pabaya," alisema.
Endelea kusoma habari hii...................

Friday, August 26, 2011
Maiti zagundulika hospitalini Libya
Zaidi ya miili ya watu 200 imepatikana katika hospitali iliyotelekezwa katika mji mkuu wa Libya Tripoli .
wanawake na watoto kwenye vitanda na veranda na pia damu nyingi iliyotapakaa kwenye sakafu.
Madaktari na wauguzi walikuwa wameitoroka hospitali hiyo kufuatia mapigano.
Walionusurika wanasema wengi waliokuwa na majeraha waliachwa bila matibabu hadi kufa, huku wengine ikioza kando yao.
Katika mji mkuu wa Tripoli kuna taarifa kuhusu kupatikana kwa mamia ya miili ya watu waliouawa baadhi yao wakiwa wamekatwa mikono.
Pande mbili zinazohusika na mzozo nchini Libya zimekuwa zikilaumiwa kwa mauji hayo.
Chanzo: BBC
Thursday, August 25, 2011
Rais Kikwete amsimamisha Jairo
RAIS Jakaya Kikwete amemsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, ili Tume atakayoiunda Spika wa Bunge, Anne Makinda imchunguze.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameliarifu Bunge kuwa, Rais ameamuru Jairo aende likizo, na kwamba, Serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kwa tume itakayoundwa.
Pinda ametoa taarifa hiyo kwa wabunge mjini Dodoma wakati anajibu maswali ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Mbowe alihoji kwa nini Jairo aendelee na kazi wakati Bunge limeamua kuunda tume kuchunguza kwa nini limedhalilishwa na pia kuchunguza mchakato wa kukusanya fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka huu wa fedha.
Mbunge huyo alimuuliza Waziri Mkuu, uhalali wa kauli ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kwamba, suala la idara kuchangia fedha za kupitisha bajeti za Wizara ni la kawaida.
Kwa mujibu wa Mbowe, bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ilijadiliwa kwa siku tano, zilitumika shilingi milioni 174/- kwa ajili hiyo, lakini bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini imegharimu shilingi milioni 578/-.
Mbunge huyo wa Hai (Chadema) alimuuliza Pinda, waliohusika katika ubadhirifu wa fedha Wizara ya Nishati na Madini wamechukuliwa hatua gani za kinidhamu, na je kweli ni sera ya Serikali kuchangisha fedha kwa ajili ya bajeti za Wizara kama alivyosema Luhanjo?
Luhanjo juzi alimuamuru Jairo arudi kazini jana kwa kuwa uchunguzi uliofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) haukumtia hatiani. Bunge jana lilisema, uamuzi alioutangaza Luhanjo umelidhalilisha na amemfedhehesha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Jairo jana alikwenda ofisini kwake wizarani jijini Dar es Salaam, wafanyakazi wakampokea kwa shangwe na vigelegele huku wakiimba kwamba wana imani naye.
Wabunge walisema jana bungeni kuwa, taarifa ya uchunguzi ya CAG kuhusu tuhuma kwamba, Jairo alichangisha Sh. Bilioni moja ili kuwezesha bajeti ipitishwe bungeni ilistahili kupelekwa bungeni waijadili kabla Serikali kutoa uamuzi.
Wabunge jana walijadili kauli ya Luhanjo kama jambo la dharura baada ya wabunge kukubali hoja ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto aliyoitoa jana asubuhi kabla ya kipindi maswali na majibu na kuifafanua baada ya Kamati ya Bunge ya Uongozi kukutana katika ukumbi wa Spika.
Zaidi ya robo tatu ya wabunge waliokuwa ukumbini wakiwemo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliunga mkono hoja ya Zitto. Ndugai, alisema , hoja ya Zitto ni ya msingi kwa kuwa Bunge limedharauliwa.
“Kwa sababu Bunge ni mhimili, hatuwezi kudharauliwa kirahisi”alisema Ndugai na kusisitiza kwamba,Wabunge hawawezi kukaa kimya wakati Waziri Mkuu anadhalilishwa.
“Kama dharau inaweza ikatokea basi huko huko lakini sio ndani ya Bunge hili” amesema Ndugai baada ya wabunge kuijadili hoja ya Zitto na kusisitiza kwamba, kwa kuwa suala hilo lilianzia bungeni, taarifa ya CAG ingepelekwa kwanza kwenye mamlaka hiyo kabla ya uamuzi wa Serikali.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Zainab Vullu, alisema, wabunge wamepewa jukumu la kuisimamia na kuishauri Serikali kwa niaba ya wananchi hivyo kauli ya Luhanjo imewadhalilisha, na limepokwa mamlaka yake.
Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, alisema, suala hilo lina maslahi kwa Taifa, taarifa ya CAG ingepelekwa kwanza bungeni itendewe haki. Sendeka alisema, Waziri Mkuu amefedheheshwa kwa kuwa kiongozi huyo wa Serikali Bungeni alisema, kama angekuwa yeye angemchukilia hatua Jairo, na pia Bunge limedhalilishwa.
Kwa mujibu wa Sendeka, kauli ya Luhanjo imelilidhalilisha Bunge na imekiuka Sheria ya Kinga na Madaraka ya Bunge na ibara ya 100 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Mbunge huyo alitumia Kanuni 117 ya Bunge kuomba iundwe kamati teule ya Bunge kuchunguza jambo hilo ukiwemo utaratibu wa Jairo kukusanya fedha za kupitishia bajeti hasa ikizingatiwa kuwa, kila Waziri huwa na fungu la kugharamia bajeti kila idara zikiwemo fedha za kununulia mafuta.
Sendeka aliomba wabunge waunge mkono hoja yake ili kulinda hadhi ya Bunge. Wabunge walikubali isipokuwa mawaziri na manaibu mawaziri.
Wakati anatoa hoja hiyo, Zitto alisema, kwa kuwa jambo hilo lilianzia bungeni wakati Mbunge wa Beatrice Shelukindo alipolieleza Bunge kuwa ana barua ya Jairo kuzitaka idara zichangie shilingi milioni 50 kila moja, wabunge walistahili kuijadili ripoti ya CAG kabla ya Serikali kufanya uamuzi.
Zitto alilieleza Bunge kuwa, kauli ya Luhanjo ni dharau kwa Waziri Mkuu, na imeingilia hadhi, kinga na madaraka ya Bunge kwa kuwa wabunge ndiyo wana mamlaka ya kuisimamia Serikali.
Zitto alipendekeza kwamba, shughuli na hoja zote za Serikali bungeni zisitishwe, kwanza wabunge waijadili taarifa za CAG kwa kuwa Bunge limepokwa nafasi yake.
Ndugai amewaeleza wabunge kuwa, Spika wa Bunge, Makinda, ataunda tume kuchunguza kudharauliwa kwa Bunge, na kukusanywa kwa fedha kwa ajili ya kupitishwa bajeti yaWizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Bunge tume hiyo itapaswa kufanya kazi haraka ili taarifa yake ijadiliwe katika mkutano ujao wa Bunge.

Jairo awasha moto bungeni
BUNGE jana lilisitisha kwa muda shughuli zake za kawaida kujadili hatua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo kabla ya Bunge kujadili Ripoti ya uchunguzi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Luhanjo kukutana na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi na kuutangazia umma kwamba kutokana na matokeo ya uchunguzi huo kutomtia hatiani anaamuru Jairo arejee ofisini mara moja.
“Kutokana na matokeo haya ya uchunguzi wa awali, mimi kama Mamlaka ya Nidhamu ya Katibu Mkuu Nishati na Madini, sitaweza kuendelea na hatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma. Ninaamuru David Jairo arejee kazini kuanzia siku ya Jumatano.”
Hata hivyo, uamuzi huo wa Luhanjo jana uliamsha hasira za wabunge bila kujali itikadi zao za kisiasa ambao ambao walitaka Bunge lisitishe kujadili shughuli zozote kutokana na hatua hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi wakisema ni kudharau Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.
Hoja ya Zitto
Hoja hiyo iliwasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) muda mfupi kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu. Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni alitoa hoja kutaka Bunge lisitishe kujadili hoja zote za Serikali hadi hapo ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali iliyomsafisha Jairo itakapofikishwa bungeni na kujadiliwa.
Zitto alianzisha moto huo mnamo saa 3:17 asubuhi ikiwa ni dakika moja tu baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kutangaza taratibu za safari ya wabunge kwenda Zanzibar kwa ajili ya mazishi ya Mbunge Mussa Khamis Silima aliyefariki juzi.
Alitumia kanuni ya 51 kulieleza Bunge kuwa kitendo kilichofanywa na Luhanjo kilikiuka haki, maadili na madaraka ya Bunge na hivyo akataka wabunge wenzake wamuunge mkono ili wagome kufanya shughuli zozote za Serikali hadi hapo ripoti ya CAG kuhusu tuhuma dhidi ya Jairo itakapowasilishwa rasmi bungeni.
“Mheshimiwa Naibu Spika, jana kupitia vyombo vya habari tulimsikia Katibu Mkuu Kiongozi kupitia vyombo vya habari akieleza kuwa tuhuma zilizokuwa zikimkabili Jairo si za kweli na kwamba anatakiwa kurudi kazini kuanzia leo (jana),’’ alisema Zitto na kuongeza:
“Mheshimiwa Naibu Spika unafahamu ya kwamba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizungumza ndani ya Bunge hili ya kwamba angekuwa ni yeye angeshamchukulia hatua Ndugu Jairo kuhusu vitendo alivyofanya, hivyo basi naomba nitoe hoja kwamba Bunge lisitishe hoja yoyote ya Serikali mpaka itakapoleta bungeni taarifa ya CAG kuhusiana na uchunguzi huo.”
Baada ya kutoa hoja hiyo, Zitto aliungwa mkono na wabunge zaidi ya nusu waliokuwamo ndani ya ukumbi, hali ambayo ilimlazimisha Naibu Spika wa Bunge, Ndugai, kuitisha Kamati ya Uongozi kwa dharura kujadili suala hilo.
Hoja ya Lukuvi
Baada ya hoja ya Zitto, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama kupinga hoja hiyo akisema Mbunge huyo hakufuata taratibu zilizotakiwa ambazo ni kuwasilisha kusudio kabla ya kutoa hoja rasmi.
“Mheshimiwa Naibu Spika, najua jambo hili lina public interest (masilahi ya umma), lakini kanuni zinasema kuwa mbunge anayetaka kuwasilisha jambo lolote linalohusiana na shughuli za Bunge atafanya hivyo wakati unaofaa na uliowekwa na kanuni na atakuwa amemwarifu Spika mapema kuhusu kusudio lake, hivyo ulitakiwa kuwasilishiwa mapema ili uweze kuamua,’’ alisema Lukuvi.
Akijibu hoja hiyo, Ndugai alisema: “Wakati nasoma matangazo mbalimbali kuhusiana na kifo cha Mbunge, nilipata taarifa kutoka kwa Zitto kuhusu kunitaarifu juu ya jambo hilo, hivyo basi, hoja iliyotolewa na Zitto imetolewa kwa wakati na ilifuata utaratibu unaotakiwa.’’

Sunday, August 21, 2011
Waasi wa Libya wathibiti mji wa Tripoli
Picha za televisheni zinaonyesha waasi katika uwanja wa Green Square katika mji mkuu, huku makundi ya watu wenye furaha wakisheherekea kuwasili kwa waasi hao katika uwanja huo.
Inaripotiwa waasi wamemkamata mwanawe Gaddafi Saif al-Islam, huku kiongozi mwenyewe akiahidi kuwa ataendelea kupigana.Mwendesha mashtaka wa mahakama ya uhalifu wa kivita, Luis Moreno Ocampo amethibitisha Saif al-Islam, mwanawe Gaddafi, na ambaye alitarajiwa kumridhi babake amekamatwa.
Mwanawe wa kifungua mimba Mohammed Al Gaddafi naye amejisalimisha kwa waasi na anazuiliwa ndani ya makaazi moja mjini Tripoli.
Serikali ya Libya imesema takriban wanajeshi elfu 65 watiifu kwa kanali Gaddafi wamebakia mjini Tripoli lakini ni wachache tu walioonekana wakati waasi walipokuwa wakielekea kuuteka mji huo.
Mapigano yameripotiwa katika maeneo mengine ya mji. Mwandishi wa BBC mjini Tripoli amesema waasi wanajaribu kushika udhibiti wa jengo ambalo waandishi wa habari wako.
Inaaminika kuwa bado Kanali Gaddafi ana maelfu ya wafuasi waliojihami, japo ripoti zinaashiria kuwa idadi kubwa wamejisalimisha kwa waasi.
Msemaji wa serikali ya Libya , Moussa Ibrahim, amesema takriban watu 1300 wameuwawa mjini humo.
Awali Kanali Gaddafi aliwataka raia kujitokeza na kuukomboa mji wa Tripoli. '' Jitokezeni, jitokezeni niko nanyi. Msirudi nyuma. Tutapigana hadi kuikomboa nchi yetu kuzuia uthibiti. Msiwakubalie wanyakuzi kuiteka nchi yetu, nitapigana pamoja nayi kama nilivyoahidi'', Alisema Muammar Gaddafi.
Source: BBC
Saturday, August 20, 2011
Wapiganaji wa Libya wanajizatiti Zawiya
Wapiganaji wa Libya wanaendelea kusonga mbele kuelekea mji mkuu, Tripoli.
Baada ya kuteka eneo la kati ya mji wa Zawiya, magharibi ya Tripoli, wapiganaji sasa wanasema wameiteka bandari muhimu ya Brega, mashariki mwa nchi, yenye kinu cha kusafisha mafuta.
Hakuna taarifa ya kuthibitisha hayo yanayotokea Brega.
Mwandishi wa BBC mjini Zawiya anasema kwenye medani wanayoiita medani ya mashujaa, katikati ya Zawiya, aliona majengo yaliyopigwa mabomu, yanayowaka moto, na kuta zenye matobo ya risasi.
Jana eneo hilo lilidhibitiwa kabisa na jeshi la Kanali Gaddafi.
Kulikuwa na mapigano makali jana jioni hadi usiku.
Lakini wapiganaji sasa wanaudhibiti mtaa, wamewatimua wanajeshi wa Gaddafi ambao wameelekea barabara ya kwenda Tripoli.
Kati ya medani alikuta maiti kama watatu.
Ameona maiti wanaoonesha kama Waafrika, na wapiganaji wanadai kuwa wanajeshi wengi wa Gaddafi ni askari mamluki kutoka kusini ya Sahara.
Ukweli hasa haujulikani, lakini maiti nyingi huko zinaonekana ni za Waafrika.
Sasa wapiganaji wanajitayarisha kusonga mashariki zaidi mwa mji, kuwatimua wanajeshi wa Gaddafi waliobaki Zawiya, ili kufungua njia ya kuelekea Tripoli.
Wapiganaji wa Libya wanadai kuwa waziri mkuu wa zamani, Abdessalem Jalloud, amekimbia Tripioli na amejificha katika maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji.
Source: BBC
Thursday, August 18, 2011
Simba, Simba utaipenda tu
![]() |
| Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu Mumba akishangilia bao. |
Simba waliofungwa kwenye Kombe la Kagame na Ngao ya Jamii mwaka jana vijana hao wa Mganda Moses Basena walizinduka na kupata mabao ya mapema kupitia kiungo Haruna Moshi 'Boban' dakika 15 na penalti ya Felix Sunzu dakika 38.
Simba iliyoanza kwa kasi mchezo huo ilifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa Moshi 'Boban' aliyemalizia vizuri krosi ya kutoka upande wa kushoto iliyopigwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Sunzu aliyekuwa na ushirikiano mkubwa na Emmanuel Okwi.
Mshambuliaji Sunzu alifungia Simba bao la pili kwa mkwaju wa penalti baada ya Nadir Haroub kumchezea vibaya Moshi 'Boban', kwenye eneo la hatari dakika 35. Sunzu alilazimika kuonyesha ueledi wake pale alipotakiwa kurudia penalti hiyo baada ya mwamuzi Israel Mjuni kusema Kado alitokea kabla ya kupigwa kwa penalti ya kwanza pamoja na kuwa alikuwa amefunga.
Kocha Moses Basena aliyeonekana kujifunza kwa makosa alitumia mfumo wa 4:2:3:1 na kutoa nafasi kubwa kwa Okwi, Haruna na Sunzu kutawala sehemu kubwa ya kiungo tofauti na ilivyokuwa kwenye fainali ya Kombe la Kagame.
Okwi alifanya atakalo mbele ya mabeki wa Yanga walionekana kuwa kama watu waliozidiwa na mazoezi na kukosa unyumbulifu mchezoni, huku safu ya ulinzi wa Simba chini ya mkongwe Victor Costa aliweza kuwapoteza mchezoni kabisa mshambuliaji Keneth Asamoah na Jerry Tegete.
Kiungo Haruna Niyonzima alijitahidi kuonyesha uwezo mkubwa wa kutawala mpira na kujaribu kutafuta goli kwenye mechi yake ya kwanza ya watani wa jadi, lakini alikosa msahada kutoka kwa wenzake.
Simba ilianza mashambulizi kwa kasi na dakika kwanza Okwi alikosa bao baada ya shuti lake kumgonga Haroub na kupaa juu ya goli.
Okwi alipoteza nafasi nyingine dakika 8 baada ya kuwalamba chenga mabeki wa Yanga, lakini aliugonga mpira mbele zaidi na kipa Shaaban Kado akauwahi.
Beki wa Yanga, Chacha Marwa, nahodha Shadrack Nsajigwa alipewa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Okwi. Naye Juma Nyoso wa Simba alipewa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Asamoah.
Haruna Niyonzima alipiga shuti la umbali wa mita 25 baada ya kumchungulia Juma Kaseja kwa bahati mpira huo ulipaa juu ya goli.
Kipindi cha pili Yanga iliamka baada ya kuingia Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo lakini walishindwa kuipenya ngome ya Simba.
Yanga waliendeleza sera yao ya kugomea jezi za wadhamini wa ligi Vodacom zenye nembo nyekundu kwa kuvaaa jezi za mdhamini wao TBL tofauti na Simba wenyewe walivaa zile walizopewa na Vodacom
Vikosi Yanga; Shaaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Chacha Marwa, Juma Seif, Godfey Taita, Haruna Niyonzima, Keneth Asamoah/ Gumbo, Jerry Tegete, Kigi Makasi/ Kiiza.
Simba: Juma Kaseja, Said Nasoro, Amir Maftah, Juma Nyoso, Victor Costa, Partick Mafisango, Salum Machaku/ Kiemba, Jerry Santo, Felix Sunzu, Haruna Moshi/ Gervais Kago, Emmanuel Okwi/ Kapombe.
Source: Mwananchi
Monday, August 15, 2011
‘ Kutumia gesi kwenye gari Sh1 milioni’
WIZARA ya Nishati na Madini imesema zaidi ya Sh1 milioni zinahitajika kwa ajili ya kubadilisha mfumo wa gari moja linalotumia mafuta ya petroli kutumia gesi asilia, Bunge lilielezwa jana.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima aliliambia Bunge hayo jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Muheza (CCM) Herbert Mtangi aliyetaka kujua Serikali inasema nini kuhusu utekelezaji wa mradi wa gesi kwa magari hapa nchini.
Waziri Malima alisema mpaka sasa mifumo ya magari 36 yamebadilishwa ili kuweza kutumia gesi asilia ambapo alisema kasi ya ubadilishwaji wa mifumo ya magari ni ndogo kutokana na gharama za ubadilishaji kuwa kubwa.
Aidha Malima alisema kasi ndogo ya za elimu juu ya suala hilo imesababisha ufahamu mdogo wa manufaa ya matumizi ya gesi kwenye magari ikilinganishwa na matumizi ya petroli.Alifafanua kuwa mkakati wa Serikali wa awali mwaka 2008, ulikuwa ni kuanzisha vituo vya mfano na masoko ambapo walianzisha kituo cha kujaza gesi kwenye magari ubungo.
Alisema kituo hicho kina uwezo wa kujaza magari 200 kwa siku.
Alisema Serikali kupitia TPDC kwa kushirikiana na Pan African Energy walianza mchakato wa mradi wa kutumia gesi asilia kwenye magari, viwandani pamoja na majumbani kwa lengo la kupanua manufaa ya kiuchumi na kijamii.

Saturday, August 13, 2011
Kikwete aongoza maziko ya Mayunga
RAIS Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya waombolezaji kumzika Luteni Jenerali (mst) Silas Mayunga kwenye makaburi ya Wasabato ya Unyanyembe mjini hapa.
Jenerali Mayunga, shujaa wa Operesheni Chakaza ya kumng’oa Iddi Amin baada ya kuwa ameivamia Tanzania mwaka 1978, alifariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi, India, ambako alikuwa anatibiwa.
Alikuwa na umri wa miaka 71.
Jenerali Mayunga alizikwa juzi kwa taratibu zote za Kanisa la Wasabato na za kijeshi ikiwa ni pamoja na kupigiwa mizinga 15 na gwaride la heshima la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Rais Kikwete aliungana na viongozi wa kitaifa katika maziko hayo ambao ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Edward Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani na Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi.
Wengine ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Amina Masenza, wenyeviti wa CCM wa mikoa ya Shinyanga na Mwanza, wabunge wa Mkoa Shinyanga akiwamo Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davies Mwamunyange na viongozi wengine waandamizi wa Jeshi na wapiganaji.
Rais Kikwete akifuatana na mkewe Mama Salma, aliwasili makaburini saa 9.56 alasiri akitokea Dar es Salaam ambapo pia alikuwa na ziara ya siku mbili Shinyanga ikiwa ni pamoja na kuhudhuria maziko hayo.
Mara baada ya Rais kuwasili makaburini, gwaride la Jeshi lililobeba mwili wa marehemu, liliingia eneo la makaburi saa 10.12 jioni na mwili wa marehemu kuteremshwa kaburini saa 10.30.
Mjane wa marehemu na watoto wake walikuwa wa kwanza kuweka udongo kaburini wakifuatiwa na Rais na Mama Salma, Lowassa, Mwinyi, Masenza, Jenerali Mwamunyange na Naibu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda, Luteni Jenerali Colleta Ivan, ambaye baadaye
aliwasomea waombolezaji salamu za rambirambi za Rais Yoweri Museveni.
Katika salamu zake, Rais Museveni alielezea mchango wa Jenerali Mayunga katika Operesheni Chakaza akisema alikuwa Jenerali ambaye alimpokea Museveni na wapiganaji wake 28 wa awali kwenye Shule ya Msingi ya Nyamiyanga mkoani Kagera Desemba 23, 1978.
Alisema: “Wakati Kampala inatekwa kutoka mikononi mwa majeshi ya Iddi Amin na kufikia hatua muhimu ya kuikomboa Uganda Aprili 11, 1979, askari wapiganaji katika kikosi hicho cha Waganda walikuwa 9,000 na yote hii ilikuwa kazi ya Jenerali Mayunga ambaye alitoa
mchango mkubwa sana kuongeza askari hao kwa kiwango hicho kikubwa. Tumepotelewa na mpiganaji na Kamanda hodari.”
Source: HabariLeo

Wednesday, August 10, 2011
Ripoti ya kunyanyaswa watoto Tanzania
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika linaloshughulikia maslahi ya watoto la UNICEF karibu theluthi moja ya watoto wa kike nchini Tanzania wanakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia na kuingiliwa bila hiari kabla hawajatimia umri wa miaka 18.
Kinachotumika sana katika unyanyasaji huu ni kuwatomasa watoto ambako baadae hufuatiwa na jaribio lakutaka kuwaingilia.
Afisa mmoja wa shirika hilo Andy Brooks amesema uchunguzi huu ndio uliokamilika zaidi na umeonesha kuwa serikali iko tayari kukabiliana na tatizo hili.
Uchunguzi huu pia uligundua kuwa wale ambao wamejihusisha na mapenzi kabla ya kutimia umri wa miaka 18, asili mia 29.1 ya watoto wa kike na asili mia 17.5 ya wale wa kiume wamesema kuwa mara ya kwanza wao kujihusisha na ngono haikuwa kwa hiari yao.
Unicef inasema hii ina maana walilazimishwa ama kushawishiwa kujihusisha na ngono.
Waziri wa Elimu wa Tanzania Shukuru Kawambwa amesema kuwa serikali imejitolea kukomesha unyanyasaji wa kijinsia na kuingiliwa watoto.
Bw Brooks amesema uchunguzi sawa na huo utafanywa nchini Kenya, Rwanda, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kusini.
Source: BBC
Sunday, August 7, 2011
Kondoo mwenye Korani azaliwa
Via HabariLeo
KIJIJI cha Uduru wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kimegeuka eneo la utalii baada ya waumini wa madhehebu ya Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo na maeneo jirani, kwenda kumshuhudia kondoo aliyezaliwa ameandikwa maneno mwilini kwa lugha ya Kiarabu.
Waumini hao walifurika kijijini hapo juzi baada ya sala ya Ijumaa kumshuhudia kondoo huyo aliyezaliwa wiki tatu zilizopita na kuacha watu midomo wazi kutokana na kuwa na maandishi yanayosomeka kiarabu ubavuni, yakitafsiriwa kwa Kiswahili kama Yasini.
Kondoo huyo aliyezaliwa katika familia moja ya waumini wa dini ya Kikristo, aliwavuta
waumini wengi kijijini hapo na kutoka nje ya wilaya na mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la ajabu na la kihistoria ambalo halijawahi kutokea.
Akizungumza na HABARILEO Jumapili kijijini hapo, mmiliki wa kondoo huyo, Grace
Massawe (55) alisema kondoo huyo alizaliwa takribani wiki tatu zilizopita na hakuwahi kutambua kwamba beberu huyo alikuwa na maandishi hayo, kutokana na kutotolewa nje na mama yake.
Grace alisema baada ya kondoo huyo kuzaliwa, mama yake alibadilisha tabia na kukaa ndani ambapo awali alikuwa akila chakula nje na wenzake, lakini aligundua maandishi hayo baada ya kumtoa nje mwenyewe.
Alisema awali aliona herufi ya W yenye rangi ya dhahabu, lakini siku zilivyozidi kwenda neno hilo lilizidi kukua na kubadilika rangi na kuwa jeupe zaidi, hali iliyompa wasiwasi na kutafuta msaada ili kutambua maana ya maandishi hayo kutoka kwa waumini wa Kiislamu.
“Baada ya waumini wa Kiislamu kufika hapa nyumbani walibaini maandishi hayo ubavuni mwa kondoo huyo kuwa ya Kiarabu yanayosomeka kuwa Yasini,” alisema Grace.
Alisema waumini hao walimweleza kuwa neno hilo ni muhimu sana katika Kitabu Kitakatifu cha Korani, ambalo ni kama kitovu cha kitabu hicho, pia ni moja ya sura muhimu ndani ya kitabu hicho.
Katika hatua nyingine, Grace alisema katika ufugaji wake wa kondoo hakujawahi kutokea tukio la ajabu kama hilo na kueleza kuwa kondoo aliyemzaa alikuwa ni uzao wake wa mara ya pili ambapo awali alizaa kondoo wa kawaida.
Alisema kutokana na kondoo huyo kuvuta hisia za watu wengi, pia viongozi wakubwa wa dini hiyo walifika kushuhudia maajabu hayo, akiwamo Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (Bakwata) wa Mkoa wa Kilimanjaro, Shehe Rashid Mallya, na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Hai, Juma Lyimo.
Baadhi ya waumini waliofika kumshuhudia kondoo huyo na kuzungumza na gazeti hili Aman Ramadhan na Yacoub Mushi wa Lyamungo, walisema tukio hilo ni muujiza wa Mungu uliojitokeza, hususan kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Juhudi za kumtafuta Shehe Mallya kuzungumzia tukio hilo, zilishindikana baada ya simu yake kuita bila kupokewa.

Saturday, August 6, 2011
Itibari ya Marekani inapungua
Vyombo vya habari vya Uchina vimeilaumu vikali Marekani, baada ya itibari ya Marekani kama mkopaji kushushwa kutoka kiwango cha juu kabisa cha A tatu na kampuni moja inayotoa vipimo hivyo ya Standard and Poor's.
Shirika la habari la taifa la Uchina, Xinhua, lilisema siku za Marekani kuweza kukopa tu ili kuziba upungufu wake, zimekwisha.
Na lilitaka Marekani kuhakikisha kuwa pesa ambazo Uchina imeikopesha Marekani ni salama.
Mchambuzi wa maswala ya uchumi mjini Hong Kong - Francis Lun, Meneja Mkurugenzi wa Lyncean Holdings - anasema hayo yaliyotokea Marekani ni hasara kubwa kwa Uchina na Japani.
"Kwa kupunguziwa hadhi ya uwezo wa Marekani kulipa madeni yake, ina maana kiwango cha riba lazima kipande, kwa sababu mikopo ya Marekani sasa ni A-mbili na ushee, siyo A-tatu.
Serikali ya Marekani itabidi kulipa riba zaidi juu ya mkopo wa taifa, na hivo inamaanisha kuwa kiwango cha riba kikipanda, sehemu ya mkopo wenyewe inapungua.
Uchina imeikopesha serikali ya Marekani dola trilioni moja pointi moja.
Japani imeikopesha dola trilioni moja, na ikiwa bei itapungua kwa asili mia moja tu, basi Uchina itapoteza dola bilioni 11; na Japani itapata hasara ya dola bilioni 10 mara moja."
Soource: BBC

Thursday, August 4, 2011
Kikombe cha Babu chashindwa kutibu ukimwi
- Waliokunywa wapimwa baada ya siku 90
- Matokeo yaonyesha bado wana virusi
- Wailaumu Serikali ‘kubariki’ kikombe cha Babu
Kaaya na wenzake walikuwa na imani kubwa kuwa huenda tiba hiyo ikawa ndiyo mwisho wa mateso na mahangaiko ya muda mrefu yanayotokana na kusumbuliwa na virusi vya ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa dunia haijapata tiba yake.
Watu hao walikuwa wamesafirishwa kwa msaada wa shirika la (EACNASO) ambalo pia ni muungano wa mtandao wa mashirika yanayojishughulisha na ugonjwa huo kwa nchi za Afrika ya Mashariki lenye makao yake mjini Arusha.
Imani ya waathirika hao ilijengwa juu ya msingi kuwa dawa ya kikombe cha Babu kwa wakati huo ilikuwa gumzo kubwa nchini na viongozi mbalimbali wa serikali kutoka kada mbalimbali, kama mawaziri wa serikali, majaji wa Mahakama Kuu, wenyeviti wa vyama vya siasa, wakuu wa mjeshi na wananchi, walipigana vikumbo katika kijiji hicho kupata uponyaji wa maradhi yanayowasumbua kupitia tiba hiyo.
Baada ya safari ngumu ya siku moja na nusu kutokana na ubovu wa barabara, Kaaya na wenzake walifika Samunge na kupata tiba ya kikombe cha Babu; huku wakipewa siku 90 kama muda ambao virusi vitakuwa vimetoweka katika miili yao.
Aidha, majibu ya vipimo vya watu hao pia vilikuwa vinasubiriwa kwa hamu na makundi mbalimbali katika jamii kutokana na watu hao kujitangaza kuishi na virusi hivyo na kuwa tayari kuweka hadharani majibu ya vipimo vya hali zao.
Lakini miezi minne sasa tangu muda uliotolewa “kisayansi” na Mchungaji Masapila kuwa virusi vitakuwa vimeisha miilini mwao, Kaaya na wenzake wote waliotumia tiba hiyo wamevunjika moyo baada ya kupimwa upya na kuonekana kuwa bado wana virusi vya ugonjwa huo hatari.
Endelea kusoma habari hii......................
Wednesday, August 3, 2011
Treni mpya ya kasi yaanza Afrika Kusini
![]() |
| Gautrain |
Treni hiyo ijulikanayo kwa Gautrain inachukua chini ya dakika thelathini kwa safari ya umbali huo wa kilometa 54.
Kwa gari mwendo wa safari hiyo huchukua hadi saa mbili wakati watu wengi wakiwa wanatumia usafiri kwenda ama kurejea kazini.
Safari ya treni hiyo ya Gautrain kwa njia ya kueleka uwanja wa ndege ilizinduliwa wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010, ambapo maelfu ya mashabiki wa soka waliitumia kusafiria.
Lakini kwa kufika Pretoria, inaonekana itatumia zaidi na wasafiri wa kawaida nchini Afrika Kusini ili kukabiliana na foleni katika barabara yenye magari mengi nchini humo.
Mamia ya watu walimiminika katika kituo cha treni cha Rosebank mjini Johannedburg tangu mapema saa kumi na moja na nusu alfajiri kuwahi treni ya kwanza iliyoelekea Pretoria.
Kulikuwa na matatizo kidogo yalijitokeza, ikiwemo matatizo ya kiufundi katika behewa moja, lakini wahandisi wamesharekebisha tatizo hilo, kwa mujibu wa maafisa wa Gautrain.
Serikali imesema lengo lake ni kuufanya usafiri wa treni ndio uti wa mgongo wa mfumo wa usafiri wa umma, kwa mujibu wa Waziri wa Usafiri, Sbu Ndebele.
Treni hiyo ya Gautrain imegharimu randi bilioni 24 sawa na dola bilioni 3 kuijenga.
Kasi ya treni hiyo ni kilometa 160 kwa saa.
Gautrain inatarajiwa kupunguza idadi ya magari katika barabara ya N1 Ben Schoeman inayounganisha Pretoria na mji wa kibiashara wa Afrika Kusini wa Johannesburg kwa asilimia 20.
Source: BBC
Monday, August 1, 2011
Muafaka kuhusu deni la marekani
![]() |
| Rais Barack Obama |
Bw Obama amesema chini ya makubaliano hayo nchi hiyo itapunguza matumizi yake kwa dollar trilioni moja katika kipindi cha miaka kumi ijayo.
Hata hivyo mpango huo utapigiwa kura kwenye baraza za senate hii leo.
Muafaka huo umefikiwa ikiwa imebakia siku moja tuu kabla ya makataa ya kuongeza kiwango cha kukopa fedha za kulipia madeni yake.
Kwa wiki kadhaa, viongozi wa vyama hivyo wamekuwa wakivutana kuhusu njia bora ya kufuata kukabili madeni ya marekani.
Hali ambayo ilitishia kukwamihsa shughuli za serikali.
Baraza la senate lina hadi kesho kupiga kura kuongeza kiwango hicho cha kukopa hadi dola trilioni 14 lau sivyo shughuli za serikali zitakwama.
Rais Obama amesema kuwa mpango ulioafikiwa sio ule aliotarajia lakini amelazimika kuukubali ilikuwezesha huduma za serikali kuendelea na madeni yake yalipwe.
Utawala wa Rais Obama ulikuwa unakabiliwa na shinikizo kali kutoka kwa wapinzani kutoka chama cha Republican ambao walikuwa wanapinga pendekezo lake la kuwepo na mpango ambao utasitiri hali hadi mwisho wa mwaka ujao.
Chama cha Republicans kilitaka mpango huo uwepo hadi katikati ya mwaka ujao. Lakini sasa vyama hivyo vimekubaliana kuunda kamati maalum itakayotoa mapendekezo mapya mwezi Novemba.
Saturday, July 30, 2011
Iringa inaongoza kwa VVU
![]() |
| Sehemu ya mji wa Iringa |
Kauli hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Masasi, Mariam Kasembe (CCM), aliyetaka kujua ni mashirika mangapi kutoka nje ambayo yanatoa misaada nchini kwa ajili ya kupambana na janga la ukimwi.
Aidha mbunge huyo alitaka kujua hali ya maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini ikoje kwa sasa na takwimu za mikoa ambayo inaongoza na ambayo ina hali nzuri.
Dk. Mponda alisema kuwa kwa sasa mashirika ya nje 16 ndiyo yanayotoa msaada dhiti ya vita ya ukimwi nchini na kwamba mashirika hayo hutoa misaada ya kifedha na kiufundi katika kutekeleza afua mbalimbali zinazolenga kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) na kutoa huduma kwa wale wanaoishi na VVU.
Alisema baadhi ya afua zinazotolewa ni pamoja na uzuiaji wa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT), huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa VVU, kuelimisha jamii katika masuala mbalimbali ya ukimwi.
Alizitaja huduma nyingine kuwa ni pamoja na huduma za kimaabara, matibabu ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono, kusambaza kondom na kutoa huduma ya tohara kwa wanaume.
Aidha alisema kuwa ripoti ya tafiti ya viashiria vya VVU na malaria ya mwaka 2008 inaonyesha hali ya maabukizi ya VVU kwa ujumla ni asilimia 5.7 hali ya maambukizi inatofautiana miongoni mwa watu na katika makundi tofauti.
Dk. Mponda alisema kuwa maambukizi yapo zaidi kwa wanawake ambayo ni asilimia 6.8 tofauti na wanaume ambao ni asilimia 4.7, wakati mjini maambukizi ni asilimia 8.7 na vijiji ni asilimia 4.7.
Alisema katika suala la kijiografia mkoa wa Iringa ndio wenye maambukizi ya juu ukiwa na asilimia 14.7 na mikoa yenye maambukizi ya chini ni Kigoma, Arusha, Kilimajaro na Manayara ikiwa na asilimia 2.
Source: Tanzania Daima
Mbunge aliyeghushi saini ya Pinda abainika
![]() |
| Jengo la Bunge, Dodoma |
Akizungumza na NIPASHE jana, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alisema mbunge huyo alipatikana juzi jioni na jina lake lilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu siku hiyo hiyo.
Alisema walilikabidhi jina hilo kwa Waziri Mkuu ili aamue kama atamchukulia hatua ama la na kwamba wamefanya hivyo kwa sababu hakuna mtu aliyelalamikia tukio hilo.
“Hakuna hatua tutakayomchukulia kwa sababu hakuna mtu aliyekuja kulalamikia kwetu na jina la mbunge aliyegushi tumekabidhi kwa Waziri Mkuu ataamua yeye mwenyewe hatua gani atamchukulia,” alisema Joel.
Hata hivyo, alikataa kutaja jina la mbunge huyo wala chama chake. “Siwezi kukuambia jina wala chama anachotoka," alisema Joel.
Hata hivyo, chanzo kimeidokeza NIPASHE kuwa mbunge huyo ni wa jimbo moja la Mkoa wa Rukwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa baadhi ya wabunge ambao mbunge huyo hukaa nao jirani ndani ya ukumbi wa Bunge, alishauriwa kutokufanya hivyo, lakini alibisha.
“Tulimuona wakati akiandika barua ile na kuweka sahihi na tukamshauri tukamwambia Waziri Mkuu ana mamlaka ya juu sana huwezi kumfanyia mchezo halafu Selasini (Joseph Mbunge wa Rombo Chadema) si mtani wake, lakini yeye aliendelea na msimamo wake ndiyo yakampata haya,” alisema mbunge huyo.
Jumatano iliyopita, muda mfupi kabla ya kuahirishwa kikao cha Bunge cha jioni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisimama na kuomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge kuhusu baadhi ya wabunge kuwaandikia wenzao barua wakitumia jina la WaziriMkuu Pinda.
”Mheshimiwa Mwenyekiti, umeibuka mtindo kwa baadhi ya waheshimiwa wabunge kuandika vimemo kwenda kwa wenzao wakiwahadaa kuwa wanaitwa na Waziri Mkuu kwa majadiliano muhimu. Vimemo hivyo hughushiwa jina na sahihi ya Waziri Mkuu. Hii si tabia nzuri hata kidogo.
Mfano wa sasa hivi Mheshimiwa Selesini aliandikiwa kimemo kama hicho na alipoinukana kumfuata Waziri Mkuu, alimkuta anafuatilia kwa makini hoja za Waziri wa Kilimo,” alisema Lukuvi na kuongeza:
“Ilibidi Mheshimiwa Selasini aendelee kusimama pale kwa adabu na kwa muda mrefu hadi Waziri Mkuu alipomwambia kuwa memo hiyo hakuandika yeye. Naomba mwongozo wako Mheshimiwa Mwenyekiti kwa suala hili.”
Subscribe to:
Posts (Atom)