Serikali ya mpito nchini Libya imekabidhi madaraka ya kulitawala
taifa hilo kwa baraza la Congress lililobuniwa baada ya uchaguzi mkuu wa
mwezi uliopita , ikiwa ni hatua muhimu katika kipindi cha mpito katika
siasa za taifa hilo.
Mziki
wa wa bendi ya jeshi ulichezwa kuwakaribisha wanasiasa na maafisa wa
ngazi ya juu katika jeshi waliokuwa wakiwasili tayari kwa sherehe hizo.
Kisha serikali ya mpito nchini Libya ikakabidhi
madaraka kwa baraza la Congress ambalo lilibuniwa baada ya uchaguzi wa
hivi maajuzi.
Hafla yenyewe ikajawa na taswira ya mwamko mpya katika mji mkuu wa Tripoli.
Hafla hii inaashiria hatua za mpito katika siasa
za Libya kutoka utawala wa ki-imla hadi utawala wa kidemokrasia wenye
viongozi waliochaguliwa.
Hii haingetokea kama Kanali Muamar Gaddafi angekuwa bado madarakani, wengi wanaamini.
Serikali ya mpito inayovunjwa iliwajumuisha
wanamgambo wa upinzani waliomng'oa madarakani na kisha kumuua kanali
muamar Gadaffi mwaka mmoja uliopita.
Mustafa Abdel Jalil mwenye kiti wa baraza la
kitaifa lililoendesha serikali hiyo ya mpito akihutubu wakati wa sherehe
hizo za kukabidhi madaraka, amesema baraza la Congress ndilo pekee
lenye haki ya kikatiba kuwaakilisha raia wa Libya.
Waandishi wanasema ingawa kuna utulivu katika mji mkuu, Tripoli, mapigano yanaendelea katika maeneo mengi ya Libya.
Baadhi ya makundi ya wanamgambo yangali yanashikilia madaraka makubwa.
Chanzo: BBC
Wednesday, August 8, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment