Tuesday, July 31, 2012

Harusi Ya Dirk Nowitzki

Best Blogger Tips

Mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Dallas Mavericks, DirkNowitzki, ambaye ni raia wa Ujerumani, amefunga ndoa na nchumba wake wa muda mrefu anayeitwa Jessica Olsson.

Jessica, ambaye Mama yake ni mzaliwa wa Kenya, na Baba yake ni mzaliwa wa sweden, anafanya kazi na kuishi Dallas, Texas.
  




‘Dawa ya Babu wa Loliondo ni feki’

Best Blogger Tips
 Utafiti umebaini kwamba dawa iliyokuwa ikitolewa na mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila maarufu kama babu wa Loliondo ni feki na kwamba haina uwezo wa kutibu Ukimwi wala kisukari.

Hayo yalielezwa bungeni jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2012/13.

Alisema utafiti wa kulinganisha wagonjwa wa ukimwi na kisukari waliokunywa dawa hiyo na wale ambao hawakunywa umebaini kwamba hakuna utofauti wa afya ya mgonjwa.

Alisema utafiti huo unafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), ulianza Machi mwaka huu na kwamba unahusisha wagonjwa 200 wanaofuatiliwa kwa kupimwa damu, kinga ya mwili (CD4) na uzito wa mgonjwa, ambao ulifanyika tangu mgonjwa alipokunywa kikombe cha babu.

“Matokeo ya awali ya utafiti yameonyesha kuwa hakuna utofauti katika vipimo vya kimaabara pamoja na damu, CD4, uzito na ubora wa afya ya wagonjwa kati ya waliokunywa na wale ambao hawakunywa dawa ya mchungaji,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema lengo la utafiti huo ni kubaini uwezo wa dawa hiyo katika kutibu magonjwa aliyosema dawa yake inayatibu ili kuona kama kuna utofauti wowote baada ya mgonjwa kutumia dawa.

Chanzo: Ippmedia

Mtikisiko

Best Blogger Tips
 NCHI imetikiswa. Mgomo wa walimu ulioanza jana katika sehemu mbalimbali nchini, umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu huku kukiwa na taarifa za matukio yasiyokuwa ya kawaida yaliyoambatana na mgomo huo usio na ukomo.

Katika sehemu mbalimbali nchini, walimu waliripotiwa kugoma kwa kutoingia madarasani na wengine walifika kazini na kusaini vitabu vya mahudhurio kisha kuondoka hali iliyosababisha wanafunzi kurandaranda ovyo katika sehemu za miji iliyo karibu na shule hizo.

Mjini Dodoma ,wabunge jana walimbana Naibu Spika, Job Ndugai wakitaka shughuli za Bunge zisitishwe ili kujadili mgomo wa walimu ambao umeanza rasmi jana nchi nzima, na kuziacha shule nyingi zikiwa na walimu wakuu na wakuu wa shule pekee.

Hata hivyo, Ndugai alisema Bunge lisingeweza kujadili suala hilo kwani tayari Serikali ilikuwa imelifikisha mahakamani baada ya kushindwa kuafikiana na walimu katika ngazi ya usuluhishi.Wakati hayo yakiendelea, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema Serikali itafuta mishahara kwa walimu walioitikia mwito Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa kushiriki mgomo ambao alisema siyo halali.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Kawambwa pia aliwaonya walimu ambao alisema wamekuwa wakiwabughudhi wenzao ambao waliamua kwenda kazini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akiwa Mjini Morogoro aliwaagiza wakuu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo kuandaa orodha ya majina ya walimu wasiofika kazini Julai 30 na waifikishe kwa maofisa elimu wa wilaya kabla ya saa 2:00 asubuhi ya Julai 31.

Waandishi wetu katika sehemu mbalimbali nchini pia waliripoti kwamba katika baadhi ya shule, wanafunzi waliruhusiwa kurejea nyumbani mapema kwa maelezo kwamba hakukuwa na masomo.Hali hiyo ilizua kizaazaa kwani katika baadhi ya mikoa wanafunzi walicharuka na kuitisha maandamano hadi katika ofisi za maofisa elimu wa wilaya, wakitaka Serikali iingilie kati mgomo huo ili waendelee kusoma.

Kadhalika, baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali walinukuliwa wakitoa matamko ya kuwasihi au kuwaamuru walimu warejee madarasani, kauli ambazo hata hivyo, hazikubadili uamuzi wa walimu hao.

Wanafunzi waandamana
Maandamano ya wanafunzi yaliripotiwa katika Mji wa Tunduma, Mbeya ambako polisi walitumia mabomu ya machozi kuwadhibiti wanafunzi.

Wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi katika Wilaya ya Mbozi mkoani humo waliandamana wakidai haki ya kufundishwa. Hata hivyo, maandamano hayo yaliingiliwa na vibaka ambao baadaye walivunja ofisi za Halmashauri ya Mji wa Tunduma na kuiba mali kadhaa kisha kuchoma nyaraka zilizokuwemo.
Tukio hilo lilitokea asubuhi wakati wanafunzi wa shule 14 za msingi zilizopo katika halmashauri ya Tunduma walipojikusanya na kufanya maandamano hadi nyumbani kwa diwani na baada ya kumkosa walielekea kituo cha polisi na baadaye ofisi katika hizo.

Katika manispaa ya Temeke, Dar es Salaam zaidi ya wanafunzi 400 wa shule nne za msingi wameandamana hadi katika Ofisi ya Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo kupinga mgomo huo.
Wanafunzi wao ambao waliandamana walitoka  katika Shule za Msingi Bwawani, Mbagala Kuu, Mtoni Kijichi na Maendeleo.

Wilayani Tarime, Mara wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi jana waliandamana hadi Ofisi ya Ofisa Elimu wa Wilaya hiyo na zile za CWT, wakidai haki yao za kupata elimu baada ya walimu kugoma kuingia madarasani na kisha kuwataka wanafunzi kurejea nyumbani.

Wanafunzi hao walisikika wakiimba na baadaye kuzungumza mbele ya Ofisa elimu wa Wilaya, Emmanuel Johnson kwamba kitendo cha walimu kugoma kufundisha kinawaathiri wao, hivyo waliitaka Serikali kuwalipa walimu madai yao ili waendelee na kuwafundisha.

“Watoto tunataka haki zetu, Watoto tunataka  kupata elimu,  watoto tunataka kusoma tunaomba walimu walipwe madai yao tuingie madarasani, watoto tusinyimwe haki yetu ya kupata elimu walimu wanapogoma waathirika ni sisi wanafunzi Serikali tatueni mgomo wa walimu,” walisema wanafunzi hao.
Johnson aliwatuliza wanafunzi hao na kuwaahidi kwamba atatatua tatizo hilo, hivyo kuwataka kurejea shuleni leo kuendelea na masomo.

Mkoani Pwani mgomo wa walimu ulisababisha maandamano yaliyowahusisha wanafunzi wa shule za msingi kadhaa katika Wilaya za Kisarawe, Mkuranga, Bagamoyo na Kibaha waliokuwa wakiishinikiza Serikali kusikiliza madai ya walimu ili wao waweze kupata haki yao ya kufundishwa.

CWT wanena
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel Olouch alisema mgomo wa walimu umefanikiwa kwa asilimia 90 nchi nzima na kwamba walimu katika mikoa mbalimbali hawakwenda kazini ikiwa ni hatua ya kushinikiza kupewa haki yao.

“Tunawashukuru walimu kwa kuunga mkono azimio lao ambalo walilipigia kura la kufanyika kwa mgomo na kubaki nyumbani bila ya kwenda kazi hadi pale Serikali itakaposikiliza matatizo yao” alisema Oluoch na kuongeza:

“Mgomo huu ambao umeanza leo (jana) hautahusiana na Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika usiku wa kuamkia Agosti 26, mwaka huu.”
Oluoch alisema kikomo cha mgomo huo ni pale itakapotolewa taarifa na Rais wa CWT, Gratian Mukoba na si mtu mwingine yeyote wala Serikali.

“Walimu wanatakiwa kutambua kuwa mgomo huu utaendelea hadi pale Rais Mukoba atakapowatangazia kinachoendelea hivyo kwa hivi sasa waendelee na mgomo huu,” alisema Oluoch.

Serikali yang’aka
Akizungumzia mgomo huo Dk Kawambwa alisema: “Tutatumia sheria kwa kushikilia malipo ya mishahara kwa walimu wanaogoma na tutatumia pia sheria kuwaadhibu walimu wanaowabughudhi wenzao kwa kuwalazimisha wagome.”

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Kazi ya mwaka 2004 ambayo vyama vya wafanyakazi vinaitumia kufanikisha migomo, Kifungu cha 83(4) kinaeleza kwamba mfanyakazi hatapaswa kulipwa mshahara katika kipindi chote ambacho itatokea amegomea utoaji huduma kwa umma.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Dk Kawambwa alisema Kuwa Serikali itahakikisha kwamba inawalinda walimu wote ambao hawaungi mkono mgomo huo aliodai ni haramu kwa kuwa suala hilo kwa sasa linashughulikiwa mahakamani.

Katika hatua nyingine, Dk Kawambwa aliwaonya wazazi kuhakikisha kwamba watoto wao hawatumiwi na wagomaji kwa kuhimizwa kufanya maandamano  na vurugu.
Chanzo: Mwananchi

Sunday, July 29, 2012

Rushwa bungeni moto

Best Blogger Tips
 SAKATA la wabunge kuhongwa kwa nia ya kuyatetea makampuni ya mafuta na menejimenti ya Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) linazidi kuchukua sura mpya kadiri siku zinavyosonga mbele.

Siku moja baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kuvurumisha makombora dhidi ya wabunge hao pasipo kuwataja kwa majina, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, ameibuka na jipya kuhusu sekeseke hilo.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi amesema wakati wowote kuanzia sasa atawataja kwa majina wabunge wote waliopokea rushwa kwa lengo la kuwalinda viongozi wakuu wa TANESCO wanaokabiliwa na tuhuma za kulihujumu shirika hilo.

Mbali ya hilo, Mbatia amemshutumu Spika wa Bunge, Anne Makinda, kwa kuwalinda wabunge hao aliodai wamehongwa na mafisadi hao wa TANESCO.

Kauli hiyo aliitoa jana mkoani hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Spika Makinda kuridhia kuivunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na kuiagiza Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwachunguza watuhumiwa.

Mbatia alisema Spika anao ushahidi wa kutosha wa majina ya wabunge waliohongwa kwani Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliliambia Bunge kuwa wana ushahidi wote.

Alibainisha kuwa ushahidi huo ndiyo uliomfanya Spika Makinda akaridhia kuivunja kamati husika na kuipa kazi Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwachunguza watuhumiwa.

Kiongozi huyo pia alisema hawana imani na kamati iliyopewa jukumu la kuwachunguza wabunge watuhumiwa wa rushwa kwa sababu inaundwa na baadhi ya watuhumiwa.

“Tunamtaka Spika ajitakase kwanza kwa kuwaengua wajumbe ambao ni watuhumiwa, kinyume na hapo hatuna imani na kamati hiyo,” alisema.

Alisema Bunge ni chombo kitukufu na ili utukufu huo uonekane ni lazima maamuzi yanayofanywa huko yaheshimiwe, hivyo akapendekeza kuwa mbali na Bunge kutumia kanuni zake kuwahukumu wabunge watuhumiwa au linaweza kuiga maamuzi ya baadhi ya mabunge ya Jumuiya ya Madola.

Alitolea mfano mabunge ya Uingereza na India, ambapo Bunge la Uingereza limewahi kuwatimua na kuwavua ubunge wabunge 57 na India imefanya hivyo kwa wabunge 11 kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

“Hivyo basi tunatoa wito kuwa mbunge yeyote wa chama chochote anayeamini kwa dhamira yake kwamba ni mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini na anafanya biashara na TANESCO kwa njia ya maslahi binafsi halafu anatumia rushwa kuwashawishi wabunge wengine au amepokea rushwa kutetea uovu ni bora akajiondoa mwenyewe kwenye ubunge kabla ya kuabishwa na Bunge,” alisema.

Mbatia aliongeza kuwa wanamtaka Spika awe amewataja kwa majina wabunge waliopokea rushwa si zaidi ya wiki moja ili Bunge liwachukulie hatua, huku akiwaomba wabunge wenzake bila kujali itikadi za vyama vyao wafanye azimio la Bunge ili wahusika mbali na kuvuliwa ubunge wafungwe jela miaka mitano.

“Kwa mujibu wa sheria namba 3 kifungu cha 32 ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ya mwaka 1988, mbunge anakatazwa kuzungumza, kuhoji, kupiga kura au kutetea jambo lolote bungeni ambalo litakuwa na ushawishi wa maslahi yake binafsi kutoka nje na kwamba adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka mitano jela,” alisema Mbatia.

Mwenyekiti huyo ambaye alifuatana na mbunge mwingine wa chama hicho wa Kasulu Mjini, Moses Machali, alimtaka Spika kuzitaja kamati nyingine ambazo wajumbe wake wanatuhumiwa kwa rushwa.

Mbali na Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, kamati nyingine zinazodaiwa baadhi ya wabunge wake kujihusisha na vitendo vya rushwa ni ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) chini ya Zitto Kabwe na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Augustine Mrema.

Nyingine ni ya Miundombinu chini ya Peter Serukamba, Viwanda na Biashara ya Mahmoud Mgimwa na Ardhi, Maliasili na Mazingira chini ya James Lembeli.

“Tatizo la nchi yetu ni kuchelewa kufanya maamuzi wakati muafaka. Tukilitakasa Bunge kwa kuwashughulikia wabunge waliokula rushwa ni wazi hata serikali itaanza kuwachukulia hatua wale ambao tumekuwa tukiwalalamikia kujihusisha na rushwa.”

Mbatia aliwatahadharisha wabunge wa chama chake kuwa kama kuna yeyote aliyechukua rushwa katika sakata hilo, ajiengue mapema.

Mbatia pia alitumia mwanya huo kuwatia matumaini wabunge waadilifu wenye misimamo mikali ya kuikosoa serikali kuwa wasiogopeshwe na sakata hilo ambalo alidai serikali italitumia kuwanyamazisha wabunge kwa vile walikuwa wakiikosoa.

Ingawa Mbatia hakuwataja kwa majina wabunge hao, habari ambazo Tanzania Daima inazo zinaeleza kuwa wabunge zaidi ya sita wanatajwa kuwa katika kundi la wale wanaotuhumiwa kuwatetea mafisadi wa TANESCO.

Inadaiwa wabunge hao walipewa fedha na kampuni za mafuta ili washinikize kung’olewa kwa Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliakim Maswi wanaodaiwa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kwa TANESCO kampuni ya Puma Energy.

Habari zinaeleza kuwa, wabunge hao wako katika Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Kamati ya Miundombinu, Kamati ya Viwanda na Biashara na Ardhi, Maliasili na Mazingira.

Gazeti hili limedokezwa kwamba wabunge takriban wote isipokuwa mmoja tu, walioko katika orodha hiyo wanatokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Chanzo: Tanzania Daima

Friday, July 27, 2012

Balozi auwawa Nairobi

Best Blogger Tips
 Kaimu balozi wa Venezuela nchini Kenya Olga Fonseca ameuawa na watu wasiojulikana.

 Kitengo cha polisi wanaoshughulikia usalama wa maafisa wa kibalozi nchini Kenya kimeupata mwili wa balozi huyo mwenye umri wa miaka 57 nyumbani kwake katika mtaa wa Runda.

 Balozi huyo amewasili nchini Julai 15 kuchukuwa mahala pa mtangulizi wake Gerardo Carrillo ambaye aliondoka Kenya baada ya wafanyakazi wa kike kwenye ubalozi wa Venezuela kumtuhumu kwa dhuluma za kimapenzi.

 Afisa mkuu wa polisi Nairobi Area Antony Kibuchi amesema kuwa ishara zote zinaonyesha kuwa balozi huyo alinyongwa nyumbani kwake alfajiri.

 Amesema kwamba polisi wanachunguza masuala mbali mbali kuhusiana na kifo hicho ikiwemo habari kuwa huenda wafanyakazi aliowafuta kazi wamekuwa na kisasi naye.

 Balozi huyo aliwafuta kazi baadhi ya wafanyakazi waliodai mtangulizi wake alikuwa akiwadhulumu kimapenzi. Tayari wafanyakazi wawili wa ubalozi huo wametiwa nguvuni.
Chanzo: Radio Maisha

Bunge lanuka rushwa

Best Blogger Tips
 BUNGE jana liliwaka moto baada ya baadhi ya wabunge kuwanyooshea vidole wenzao kwa madai kupokea rushwa kwa lengo la kuwapigia debe mafisadi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wanaowafilisi Watanzania.

Wabunge hao wanadaiwa kuwaunga mkono mafisadi ili Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, na Katibu Mkuu wake, Eliakimu Maswi, waonekane hawafai.

Akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti kwa wizara hiyo jana, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (CHADEMA), alisema kwa wiki nzima waziri na watendaji wake walikuwa wakidhalilishwa na baadhi ya watu kwa kupitia wabunge wakitaka Rais Jakaya Kikwete awaondoe kwa madai kuwa walikiuka sheria ya manunuzi ya umma na kuipa zabuni kampuni ya PUMA Energy.

“Mheshimiwa mwenyekiti baadhi ya makampuni ya mafuta yalikuwa hapa Dodoma na kutoa chochote kwa wabunge na hili si kwa upande wa serikali ya CCM bali wabunge wa pande zote tukiwemo wapinzani. Msione watu wanazungumza kwa nguvu hapa kutetea, hawa wamepewa chochote,” alisema.

Huku akishangiliwa na karibu wabunge wote, Selasiani alisema wanaohoji kuwepo ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya umma anawashangaa kwani katika jambo la msingi lazima uamuzi uwe mgumu huku akitolea mfano wa Yesu Kristo alivyoivunja Sabato aliyoiweka mwenyewe.

“Mheshimiwa mwenyekiti Maswi ametishwa tunajua hilo, ametumiwa meseji za vitisho, ameombwa rushwa na baadhi ya wabunge wenzetu hapa. Tunawajua wako wabunge wanafanya biashara na TANESCO, lakini humu waongea kwa nguvu na jazba wakijifanya watetezi wa wananchi kumbe ni nguvu ya rushwa,” alisema.

Selasini alimtadharisha Waziri Muhongo kuwa yeye ni msomi asiyetokana na siasa hivyo hawajui wanasiasa lakini ni vema afanye kazi kwa nguvu bila kutetereka na atawazoea.

Mbunge huyo pia alipendekeza sheria ya wahujumu uchumi irejeshwe ili wahusika wakiwemo wabunge waliohusika katika sakata hilo wahukumiwe kama wahaini.

“Wako wenzetu humu wamekuwa wakijifanya wapambanaji wanaongea kwa nguvu kuhusu ufisadi lakini leo wamekuwa madalali wa mafisadi na hawa wako kote CCM na huku kwetu wapinzani,” alisema.

Selasini alizungumza baada ya kutanguliwa na wabunge wenzake, Anne Killango Malecela wa Same Mashariki na Christopher Ole Sendeka wa Simanjiro (CCM), ambao walionekana kupishana katika kuwaunga mkono waziri na watendaji wake.

Licha ya kuwapongeza waziri na watendaji wake, Ole Sendeka alisema anapaswa kuwaeleza wananchi hali iliyopo ili mambo yakiharibika wasimshangae.

Alisema mitambo inayotumika kuzalisha umeme sasa ni ya kampuni binafsi inayoiuzia TANESCO uniti moja kwa dola senti 23 halafu shirika hilo linauza kwa dola senti 12 ambayo ni hasara ya dola senti 11.

“Hii ni mikakati ya kifisadi kwenye sekta ya gesi kwani kampuni za Songas zinauziwa gesi kwa bei ya kutupwa ndiyo maana wanaweza kuuza umeme wao kwa bei nafuu.

Sendeka alitaka kamati itakayoundwa kumchunguza Mkurugenzi wa TANESCO, William Mhando, iwachunguze pia na watendaji waliotoa zabuni za mafuta kinyume na sheria ya manunuzi kwa kisingizio cha bei nafuu ili wachukuliwe hatua.

Naye Kilango pamoja na kutumia muda mwingi kumsifu Maswi, lakini alipingana na Sendeka akisema kuwa hakuna sheria ya manunuzi iliyokiukwa na vile vile akatumia muda huo kumpongeza msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani kwa wizara hiyo, John Mnyika kwa hotuba yake.

Kilango aliyeonekana kuzunguka ukumbini na kuteta na Waziri Muhongo wakati wa asubuhi akiwa na kitabu cha hotuba ya upinzani, alisema kuwa amempongeza msemaji wa upinzani kwa vile masuala mengi ya ufisadi wa TANESCO aliyoyasema ni ya CCM waliyoyasema juzi kwenye kamati yao ya chama.

“ Tarehe 25 usiku kuanzia saa 3 mpaka 6 wabunge wa CCM tukutana na tukawa na mazungumzo marefu hivyo napongeza msemaji wa upinzani kwa vile yale aliyosema ukurasa wa 10 mpaka 16 ndiyo yale tuliyojadili kwa kirefu naona waliyapatapata,” alisema Kilango.

Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora alikuwa kivutio pale alipoomba aruhusiwe kwenda mbele ya wabunge kuwaonyesha jinsi Bunge lilivyoweza kusigina mirija yote ya mafisadi ndani ya TANESCO na hivyo kuwafanya wabunge kuangua kicheko na vigelegele.

Alihoji walikuwa wapi wale wanaosema kanuni za manunuzi ya umma zimekiukwa, kwamba mbona hawakujitokeza wakati nchi ikiwa gizani. Alishangaa watu kumsakama Maswi na wenzake wakati aliokoa fedha ambayo itasaidia kununulia dawa hospitalini, madawati, vitabu na huduma nyingine.

Lugora ambaye alikuwa akishangiliwa kwa nguvu, alifafanua kuwa kwa mujibu wa mkataba ni kwamba mwenye mamlaka ya kuwanunulia mafuta IPTL ni Wizara ya Nishati na Madini wala si TANESCO.

Alisema kuwa Bunge hilo halitaki na wala halitakubali kutumika kama kichochoro cha mafisadi, hivyo waazimie kwa kauli moja kwamba waziri awaeleze kuwa hakutakuwa na mgawo wa umeme tena. Hivyo kauli za kwamba nchi haitawaliki ni za kifisadi zinazoratibiwa na wale wanaozima mitambo ili kutengeneza mgawo.

Lugora alitaka Mhando achukuliwe hatua kuanzia leo kwa kutumia madaraka vibaya kwa kumpatia mkopo mkewe Eva wakati taratibu nyingine za kuchunguzwa kwa tuhuma nyingine pamoja na wenzake zikiendelea.

Naye mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, aliibua tafrani wakati akichangia pale aliposema kuwa nchi imebakwa kutokana na serikali kufa ganzi, kauli iliyopingwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), William Lukuvi, ambaye aliomba mwongozo wa kiti akidai mbunge huyo ametukana.

Hata hivyo iliwachukuwa muda kufikia muafaka baada ya Kafulila kugoma kufuta kauli hiyo alipotakiwa kufanya hivyo na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, akidai kuwa kwao Kigoma kubaka si matusi kwani wanabaka hata panzi.

Zungu alitumia burasa sana kumsihi Kafulila afute kauli hiyo lakini mwishowe alisimama na kusema kuwa analazimika kufanya hivyo kwa matakwa ya mwenyekiti na ndipo akaruhusiwa kuchangia.

Katika mchango wake alisema kuwa hakuna namna yoyote nchi inaweza kufikia mapinduzi ya viwanda bila kuwa na nishati ya umeme wa uhakika huku akitolea mfano nchi ya Malysia iliyokuwa na tatizo la nishati hiyo mwaka 1994 kama Tanzania.

“Wenzetu baada ya hapo walitafuta ufumbuzi wa kudumu na hivyo kuzalisha umeme wa megawati 10,000 wakati sisi tulikimbilia kwenye umeme wa dharura kwa kampuni binafsi ya APTL na leo tunazalisha megawati 1,000.
Chanzo: Tanzania Daima

Dar katika orodha ya majiji 12 machafu duniani

Best Blogger Tips
 INAKADIRIWA kuwa  Jiji  la Dar es Salaam, linazalisha tani 4,252 za taka kwa siku na kwamba ni kati ya asilimia 26 na 37 tu, zinazozolewa na kutupwa dampo.Hayo yalisemwajana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, katika hotuba yake katika warsha kuhusu kubuni mikakati ya kusimamia usafi wa mazingira ya jiji.

Warsha hiyo inawashirikisha wadau mbalimbali wa mazingira.Meya huyo alisema majiji mengi katika nchi zinazoendelea, yana mazingira machafu ikilinganishwa nay ale ya nchi zilizoendelea na kwamba hali hiyo inatokana na  changamoto  nyingi ukiwemo ukomo wa bajeti.

Hali  kadhalika wingi wa watu wanaohamia  mjini na mipangilio mibovu ya miji.Dk Masaburi alisema kwa assa Jiji la Dar es Salaam, linakadiriwa kuwa na wakazi milioni nne na nusu  huku ongezeko la wahamiaji likiwa limefikia asilimia 4.3.

Alisema ongezeko hilo la watu, limesababisha  Jiji hilo kukua kwa kasi kubwa.

“Asilimia 70 ya watu hao wanaishi katika maeneo yasiyopimwa na mimi ni miongoni mwao,” alisema Dk Masaburi.

Alisema ongezeko hilo la watu,  limesababisha mamlaka za halmashauri,  kushindwa kumudu kutoa kwa ufanisi,  huduma za miundombinu ya barabara, afya, majisafi, maji taka na mipango miji .

Alibainisha kuwa Jiji la Dar es Salaam, linakadiriwa kuzalisha wastani wa tani 4,252 za taka kwa siku.
Alisema kwa kuzingatia changamoto hizo, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na wadau wengine, imeanzisha sehemu ya kutengeneza mbolea ya mboji kwa kutumia takarejea, zinazotokana na mabaki ya vyakula mbalimbali.

Kwa mujibub wa meya, mbolea hiyo ya mboji inahitajika kwa kiwango kikubwa na wakulima wadogo wadogo na itasaidia kuwa sehemu ya vyanzo kwa vikundi vya kijamii vinavyojishulisha na udhibiti wa taka jijini. “Lakini pia itasaidia  kupunguza hewa ya Carbon inayotokana na taka zenye kemikali zinazosababisha madhara kwa binadamu ukiwemo ugonjwa wa kansa,” alisema.

Kaimu  Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Taka katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Membe Protus,  alisema Jiji hilo  ni la tatu barani Afrika linalokua kwa haraka.

Alisema pia ni moja ya  majiji 12 machafu duniani.Alisema halmashauri zinafanya kazi ya kukusanya uchafu  kwa shida kutokana na upungufu wa vifaa, ikiwemo vya  kuteketeza taka hatarishi husasani zile  za hospitali na zenye kemikali.
Chanzo: Mwananchi

Thursday, July 26, 2012

Kaburu anahatia kupanga kumuua Mandela

Best Blogger Tips
 Mtu aliyepanga njama za kutaka kumuuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amepatikana na hatia.

Mahakama ya Pretoria ilimpata kiongozi wa kundi la -Boeremag linaloamini kuwa mtu mweupe ni bora alipatikana na hatia ya kupanga kummua Mandela mwaka 2002.

Bwana Mike du Toit ndiye aliyepanga milipuko tisa katika eneo la Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.

Kiongozi huyo wa kundi la ki-baguzi ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia tangu utawala wa wengi uanze mwaka 1994 Afrika kusini.

Wachanganuzi wanasema kuwa bado kuna hali ya kutopendana katiki ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini.

Hata hivyo kundi kama la Boeremag,inayomaanisha Nguvu za Makaburu miongoni mwa Makaburu ,halina ufuasi mkubwa.

Mahakama hiyo ya Pretoria imempata Du Toit, ambaye alikuwa msomi baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa miaka tisa.
Chanzo: BBC

5 Secrets to a Happy Marriage: Revealed by Divorce

Best Blogger Tips
 In 25 years of studying marriage, Dr. Terri Orbuch, research professor at the University of Michigan and author of the new book "Finding Love Again: 6 Simple Steps to a New and Happy Relationship," has found that some of the best relationship advice comes from people who are actually divorced.

 In 1986, Orbuch embarked on a long-term study, supported by the National Institutes of Health (NIH), which followed the relationships of 373 newlyweds. By 2012, 46% had divorced, about the same as the national average. In interviews with Orbuch, people who had divorced or ended a serious relationship over and over again brought up the same five issues that they would improve if they had the chance to do it all again. 

1. Money. Over the course of her research, one the biggest surprises for Orbuch was the role money played in marital strife. “Many divorced singles say that money was the number one source of conflict in the early years of marriage,” she tells Yahoo! Shine. She also found that, “6 out of 10 said they would not share living expenses in their next relationship.” She recommends that each partner evaluate their own approach to spending and saving money and discuss with their spouse early on. She says there is no one-size-fits-all-financial plan, but couples need to determine their own rules and adhere to them. 

2. Affection. Another surprise was that men crave affection—but not necessarily sex—more than women. “It’s counterintuitive,” says Orbuch, “but men crave feeling special and being noticed by their wives.” She adds that men who report not getting enough nonsexual affection were twice as likely to ask for a divorce, but the reverse was not true for women. “Women are fortunate. We get this kind of affirmation from more people in our lives, our mothers, children, our best friends”—so women tend to need less from husbands.  She recommends carving out time for regular cuddling, kissing, hand holding, and saying “I love you.” 

3. Blame. “When divorced couples found fault with their relationship using ‘we’ statements, they were significantly more likely to find love than those who used ‘I’ or ‘you’ statements.” Those who found blame in factors such as being incompatible or too young experienced less anxiety, insomnia, and depression than those who blamed their former partner or themselves for a break-up. Examine what went wrong in the relationship instead of assigning individual blame, suggests Orbuch, and think about how you can resolve conflict better next time. 

4. Communication. Orbuch says a trap many couples fall into is “maintenance” rather than true communication. She suggests having a “10 minute rule” every day when you, “Talk to your partner about something other than work, the relationship, the house, or the children.” The key is revealing something about yourself and learning something about your spouse. “Forty-one percent of divorced people say they would change their communication style,” says Orbuch,“and, 91% of happily married couples say they know their partner intimately.” 

5. Move on. Letting go of the past is a key to being in a happy relationship. This is true for people who are currently married as well as those seeking love. If you are irked by thoughts of your partner’s old boyfriend or girlfriend or of a fight that happened weeks ago, you might not be interacting in a healthy, positive way. “That animosity prevents you from being fully present,” says Orbuch. She also points out that people who felt neutral toward their ex were significantly more likely to find love after a divorce. If you can’t let go of your anger, her book outlines a number of exercises including writing a detailed letter to the person you are angry at—and burning it. 

For more information on Dr. Orbuch or to ask her a question check out her website, The Love Doctor.

Wednesday, July 25, 2012

Vigogo wagawiwa viwanja Dar

Best Blogger Tips
MANISPAA ya Temeke imetoa orodha ya majina ya wananchi waliopewa viwanja katika manispaa hiyo, ambayo inaonyesha kuwamo kwa vigogo wanaojumuisha mawaziri, wabunge, watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya watoto wa vigogo hao.Katika orodha hiyo, jumla ya watu 1,800 walipatiwa viwanja hivyo, huku majina hayo ya vigogo yakiwa ni zaidi ya 50, ambao baadhi wamejiandikisha wenyewe, wengine wake zao, ndugu na watoto wao.

Majina hayo ambayo gazeti hili iliyaona jana, yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo wa manispaa hiyo, ili wananchi walioomba viwanja hivyo waweze kuangalia kama  wamo katika orodha ya waliopatiwa viwanja hivyo.

Baadhi ya wananchi waliofika kusoma majina hayo walisikika wakilalamikia hali hiyo, huku wakisema kuwa kinachoonekana ni vigogo kupendelewa na kuwanyima wananchi wa kawaida.

Katika orodha hiyo, majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na  Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe;  Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan  Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.

Mkurugenzi apatwa kigugumizi

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Magreth Nyalile alipoulizwa kuhusu orodha hiyo alisema  kuwa, majina hayo hajayaona na kwamba waliobandika wamefanya uamuzi huo bila ya yeye kuupitia.

“Majina yenyewe sijayaona, hivyo basi siwezi kujua ni kina nani waliopewa viwanja hivyo, kwa sababu wako zaidi ya 1,000, jambo ambalo litakuwa vigumu kwangu kubaini tatizo hilo,” alisema Nyalile.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo hawezi kusema lolote kwa sababu yuko nje ya ofisi kwa ajili ya shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.

Hata hivyo, Nyalile alisema mchakato wa ugawaji wa viwanja hivyo ulifuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna mtu au kiongozi yeyote aliyependelewa, jambo ambalo linaweza kusababisha mgongano wa hapa na pale.

Nyalile alisema kuwa kama kuna viongozi walipewa kwa njia zisizo sahihi, au kwa rushwa wakati wa uwasilishaji wa majina hayo, walipaswa kutoa taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wananchi walalama

Baadhi ya wananchi walikuwa wakiangalia majina hayo katika ubao huo walidai kuwa, baadhi ya maofisa wa halmashauri hiyo wamedaiwa kupewa rushwa wakati wa ugawaji wa viwanja hivyo.

“Walitangaza kama kiini macho, lakini tayari walikuwa na majina yao ili waweze kuwapatia na jambo ambalo limejionyesha wazi kwenye majina ya watu waliopewa viwanja hivyo,” alisema mwananchi mmoja (jina tunalihifadhi) na kuongeza:

“Kutokana na hali hii, hatuna imani na viongozi wowote wa Serikali kwa sababu inaonyesha wazi kuwa, kila mmoja anaangalia masilahi yake na si wananchi wasio na kipato”.

Aliongeza kuwa, wananchi hawana imani na viongozi wao, hivyo Serikali inapaswa kuingilia kati kwa sababu hali hiyo inaweza kusababisha matatizo.

Mwananchi mwingine aliyekuwa akifuatilia jina lake alisema: “Wewe unachokiona ni nini hapo kama siyo yaleyale ya ubinafsi!  Wewe unaamini kabisa kwamba kweli hawa viongozi wetu hawana nyumba au hawana viwanja hapa Dar es Salaam.

Aliongeza: ”Kama manispaa walitangaza viwanja ili wajiuzie wangesema tu badala ya kuchukua fedha zetu Sh30,000 halafu viwanja wakajigawia wenyewe.”

Mgawo wa Viwanja

Mapema mwezi Juni mwaka huu, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitangaza kwamba imepima viwanja 1,800 katika eneo la Gezaulole ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Upimaji Viwanja.

Fomu za maombi ya kununua viwanja hivyo zilianza kutolewa Juni 11 na  kila mwombaji alipaswa kulipia ada ya maombi ya kiasi cha Sh30,000 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke iliyopo mkabala na Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.

“Fedha hizo hazitarejeshwa na mwombaji atajaza nakala mbili za fomu ya maombi na kuzirejesha zikiwa zimebandikwa picha 3 za ukubwa wa pasipoti. Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 18.06.2012 saa 8 mchana,” linasomeka tangazo rasmi la manispaa hiyo.

Wakazi wenye nyumba na mashamba ndani ya eneo la mradi ambao walikuwa wametambuliwa kabla ya zoezi la upimaji kuanza, pia walitakiwa kununua fomu za maombi kwa utaratibu uleule.
Chanzo: Mwananchi

Zitto ataja wizi kampuni za simu

Best Blogger Tips
 MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), amesema Kampuni ya mtandao ya Onmobile inashirikiana na makamupni ya simu za mikononi kuwanyonya wasanii kwa kuwalipa asilimia ndogo ya mapato yanayotokana na matumizi ya nyimbo zao.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia iliyosomwa bungeni mjini Dodoma jana, Zitto alisema kinachoshangaza kampuni hiyo iliyohodhi mambo yote ya kampuni za Vodacom na Airtel, inafanya kazi bila leseni.

“Ukimpigia simu Waziri Mkuu… utasikia simu yake ina wimbo wa Rose Mhando, Naibu Waziri Adam Malima yeye upo wimbo wa Dar mpaka Moro wa Wanaume Familly na ukinipigia mimi utasikia Kurani ama wimbo wa CHADEMA.

“Lakini kinachoshangaza wasanii hawa wananyonywa licha ya nyimbo zao kutumika, tunadhani wasanii wanapata… si kweli kwani hata vituo vya redio na televisheni vya serikali vinatumia nyimbo hizi bila kuwalipa chochote.

Makampuni makubwa ya Vodacom na Airtel wameingia mkataba na Onmobile na wanaingiza sh bilioni 43 kutokana na milio,” alisema mbunge huyo aliyeonyesha nia ya kuutaka urais mwaka 2015 kupitia chama chake.

Zitto alifafanua kuwa katika mapato hayo Onmobile anachukua mgawo wa asilimia 80, mawakala wa kati asilimia 13 na wasanii wanaambulia asilimia saba pekee, jambo alilodai kwamba halikubaliki.

Pia alisema kampuni hiyo inayofanya shughuli za mtandao wa kuingiza milio ya nyimbo kwenye simu haina wafanyakazi wa kueleweka wala ofisi maalumu.

Kwa mujibu wa Zitto, ofisi za kampuni hiyo zipo ndani ya Vodacom na Airtel na wanaofanya kazi ni watu wawili.

“Mheshimiwa Mwenyekiti ukiona vijana wetu wanavyohangaika kutayarisha miziki yao halafu bado hawalipwi mrabaha kwamba kampuni inayofanya kazi ya networking ndiyo inapata asilimia 80, si jambo la haki,” alisema.

Mbunge huyo alibainisha kwamba alipata kuzungumza na Naibu Waziri wa wizara hiyo January Makamba na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akiwaeleza ujanja huo wa makampuni ya simu kutoingia mikataba na wasanii badala yake yanawatumia mawakala.

“Mheshimiwa Makamba tulikaa nikakweleza na leo narudia ili tusaidie vijana wetu maana hata wewe ni kijana. Wabunge tukubaliane hapa kuwa katika hii mikataba wasanii wetu wapate asilimia 50,” alisema.

Mbunge huyo aliitahadharidha serikali kuwa isiogope kuichukulia hatua kampuni hiyo kwa kisingizio kuwa mikataba itawafunga, akifafanua kwamba iwapo Kampuni ya Onmobile iliweza kuja nchini kufanya kazi bila leseni ni wazi kuwa inapaswa kuchukuliwa hatu kwa kuikosesha serikali mapato.

Aliitaka serikali kulitumia Shirika la Posta kuuza kazi za wasanii kwa kuwa liko kila sehemu nchi nzima na linaaminika.

Baadhi ya wabunge waliochangia hotuba hiyo kutoka Viti Maalumu ni Leticia Nyerere (CHADEMA), Riziki Omary Juma na Raya Ibrahim Khamis (CUF), mwingine ni Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mnyaa (CUF) walioitaka serikali kutunga sheria ya kudhibiti mitandao ya internet na kijamii ili kuzuia matumizi mabaya yanayofanyika sasa.

Pia walitaka serikali kueleza kiasi kinachopatikana kutoka kwenye makampuni ya simu kwani hupata faida kubwa kuliko mapato wanayolipa serikalini.

Wabunge hao pia waliitaka TCRA kuyachukulia hatua makampuni ya simu yanayowasumbua wateja kwa kuwapigia simu za matangazo kila wakati na kuwatoza malipo kwa huduma wasizozihitaji.
Chanzo: Tanzania Daima

Wanasayansi: Ukimwi siyo tishio tena duniani

Best Blogger Tips
WANASAYANSI mbalimbali wanaoendesha tafiti mbalimbali za kutafuta tiba na chanjo ya Ukimwi, wameitangazia dunia kuwa hatua waliyofikia sasa wanauona ugonjwa huo ‘siyo hatari tena’ kwa sababu wanazo silaha zote za kuweza kukabiliana nao.

Ila wakasema, kinachowakwamisha ni ukosefu wa fedha ambazo zinahitajika katika kuendeleza tafiti na kuweka sera mpya za kukabili Virusi Vya Ukimwi (VVU) duniani.

Hayo yalibainika kwenye siku ya pili ya Mkutano wa 19 wa Kimataifa wa Ukimwi unaofanyika mjini Washington DC, Marekani na unahudhuriwa na watu zaidi 22,000 miongoni mwao wakiwamo wataalamu wa afya, watunga sera na wadau wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo toka karibu kila kona ya dunia.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kitengo cha Habari cha Mkutano huo na gazeti hili kufanikiwa kupata nakala yake, ilieleza kwamba jopo la wanasayansi nguli duniani walikiri kuwa wamefanyia VVU utafiti wa kutosha ndiyo maana wanatamba kuwa wamefanikiwa katika kuvidhibiti.

 “Kwa sasa tunazo silaha zote za kisayansi kumalizia mbali gonjwa hili la Ukimwi. Kilichobaki ni kutumia kikamilifu utaalamu huu katika fursa hii tuliyo nayo,” alisema Rais wa Taasisi ya Kijamii ya Kimataifa ya Mapambano dhidi ya VVU (IAS), Dk Elly Katabira.

Kiongozi huyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Mkutano huo akitokea nchini Uganda, aliongeza: “Kufanikisha hilo ni lazima tukubali kubadili mfumo kwa maana kwamba kuweka sera mpya zitakazowezesha kuokoa kundi linaloathirika zaidi na ugonjwa huu.”

Dk Katabira alifafanua: “Kinachohitajika ni kuweka mfumo utakaowashirikisha wafadhili na watunga sera katika kuweka mpango mzuri wa pamoja tuweza kulimaliza tatizo kwa silaha hizi za kisayansi.”

Naye Mtaalamu wa Tiba katika Chuo Kikuu cha California, Profesa Diane Havlir alisema: “Ujumbe wangu kwenu, hasa kwa watunga sera ni kwamba: endeleeni kuwekeza katika mipango ya kisayansi.”

Kwenye mkutano huo walishiriki pia wanasayansi wenye dawa na ushahidi unaoonyesha kuwa katika miaka ya karibuni zimeonyesha dalili nzuri za kutibu Ukimwi na kifua kikuu (TB).

Wataalamu wengi wa afya waliunga mkono kauli hiyo wakisema kwa sasa kuna uelewa mkubwa wa kitaalamu juu ya muundo na tabia ya VVU hivyo ni rahisi kwao kutengeneza dawa kwa ajili ya kuzuia, kutibu na chanjo.

Tafiti za awali
Kauli ya wanasayansi hao imekuja baada ya miaka 30 ya kipindi kigumu cha kutafiti namna ya kupata chanjo au tiba ya ugonjwa huo ambao umeua mamilioni ya watu duniani, hususan wataalamu na nguvu kazi inayohitajika kuimarisha uchumi.

Waligundua VVU mwaka 1981 na ilikuwa vigumu kupata dawa ya kuviua kwa sababu ya tabia zao na uwezo wa kujigeuza kuwa sehemu ya mwili na kutumia selikinga kuzalisha virusi wengine.
 
Wanasayansi hao walitoa kauli hizo za matumaini kukabili VVU mbele ya viongozi mashuhuri wa kisiasa, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton na Rais wa Ufaransa, François Hollande.

Mtaalamu anayesimamia mipango ya afya Ikulu ya Marekani, Profesa Antony Fauci, ambaye piya ni Mkurugezi wa taasisi ya nchi hiyo ya Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (NIAID), alikuwa miongoni mwa waliohutubia na kusifu hatua iliyofikiwa na wanasayansi duniani.

Ofisa Mkuu na Rais wa Taasisi ya Mapambano ya Ukimwi nchini Marekani,  Phill Wilson aliweka bayana kuwa pamoja na ugonjwa huo kuonekana tishio hasa kwa nchi zinazoendelea, hakuna nchi, hata zile tajiri, ambazo zinaweza kutamba haziathiriki na tatizo hilo.

Kwa hivyo akasema mikakati na sera mpya za kisayansi zinahitajika dunia nzima, hivyo akawataka wanasayansi hao ‘kuanika hadharani silaha zao’ ili zianze kutumika ulimwenguni kote.

Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa Mapambano ya Ukimwi (UNAIDS), Sheila Tlou aliwataka wataalamu hao kuweka mkakati mzuri utakaowezesha silaha hizo za kisayansi kuelekezwa katika nchi maskini hasa barani Afrika.

Wanasayansi hao wamekuja na kauli hizo za matumaini wakati ambapo tayari wamefanya tafiti mbalimbali na kugundua tabia za VVU ikiwa ni pamoja na vitu ambavyo vinaviwezesha kushambulia seli nyeupe za damu, maarufu kwa jina la CD4, ambazo ni sehemu ya kinga ya mwili wa binadamu.

Licha ya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa kuna kila dalili ya kupatikana kwa chanjo, miaka michache iliyopita, waligundua moja ya dawa zinazotumika kupunguza makali ya VVU (ARV) ijulikanayo kama Truvada, yenye uwezo wa kumkinga mwathirika kumwambukiza mpenzi wanayeshiriki naye tendo la ndoa.

Wiki chache zilizopita, Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) iliidhinisha Truvada, ambayo ilianza kutumika sehemu mbalimbali duniani tangu mwaka 2004, kuwa ni tiba ya kuzuia kuenea kwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Kwa mujibu wa maelezo ya FDA, mwathirika anayetumia dawa hiyo anaweza kujamiiana na mwenza wake ambaye hana VVU bila kutumia kondomu na hatomwambukiza.

Matokeo ya utafiti huo wa ARV yaliwahi kuchapishwa kwenye gazeti hili toleo la Februari 12, mwaka huu. Kwa mujibu wa FDA, Truvada inatarajia kuanza kutumika na kusambazwa duniani katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Chanzo: Mwananchi

Monday, July 23, 2012

Ajali ya MV Skagit: Waziri Zanzibar ajiuzulu

Best Blogger Tips
 Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Hamad Masoud amejiuzulu kufuatia shinikizo za za watu na maandamano.

Kumekuwa na msukumo kutoka kwa makundi mbali mbali ya kutaka waziri huyo ang'atuke kufuatia kuongezeka kwa ajali za baharini kati Hatua hii imekuja kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa zikiongezeka mjini Zanzibar bila yeye kuchukua hatua yeyote.

Mbali na kujiuzulu kwa Hamad kama Waziri, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza kiiina cha Meli hiyo ya MV Skagit kuzama na kuuwa watu.

Mwenyekiti wa tume hiyo atakuwa Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wanachama watukiwa Meja Jenerali S.S. Omar, Komanda Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.

Kufuatia shinikizo hizo Siku ya Ijumaa ,tarehe 20 Julai ,Hamad Masoud alimuandikia barua rais wa Zanzibar kumuomba kujiuzu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chama tawala cha CCM, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.

Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais ,Dk Shein amemteua Mbunge wa Jimbo la Ziwani Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano.

Taarifa kutoka ikulu zinasemna kuwa uteuzi wa Bwana Rashid Seif Suleimna utaanza mara moja.
Chanzo: BBC

Saturday, July 21, 2012

Wabunge CHADEMA wafanyiwa ujasusi

Best Blogger Tips
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimedai kugundua mbinu zilizotumiwa na mtoto wa kigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) za kuingilia mawasiliano ya simu za wabunge wake kutuma ujumbe wa vitisho kwa mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA, Mabere Marando, alisema mtoto huyo wa kigogo ambaye hakumtaja jina, alinunua mitambo hiyo kutoka nchini Israel.

Alisema nchini Israeli kuna kampuni mbili alizozitaja kwa majina ya Nice System na Verinty System, ambazo zimefanikiwa kutengeneza mitambo yenye uwezo wa kuingilia mawasiliano ya mtu kwa umbali wa kilometa tano na kwamba moja ya mitambo hiyo ndiyo iliyotumiwa kusambaza ujumbe mfupi wa simu kwa Mwigulu, zikionyesha kuwa zimetoka kwa wabunge wa CHADEMA.

Aliongeza kuwa mfumo uliotumika kuingilia mawasiliano ya wabunge wa CHADEMA unaitwa sms proofing, na kwamba inaweza kutumiwa na idara za kiusalama kwa sababu maalum tu.

“Tuliwauliza wabunge wetu kama wamefanya suala hilo na wakatuhakikishia kuwa hawahusiki, tukashtuka na kama mshauri wa masuala ya kiusalama wa chama tukaamua kuingia kazini kufuatilia hili, tulichogundua ni kwamba mipango hii iko nyuma ya mtoto wa kigogo wa CCM ni mtaalamu wa mitandao na ana fedha nyingi za kufanyia kazi hii,” alisema Marando.

Alieleza kuwa jambo la kusikitisha ni taarifa walizozipata kuwa mwanasheria mkuu wa serikali Jaji George Werema kuwaagiza watumishi wa ofisi yake kuandaa mashtaka kwa ajili ya tukio hilo la kuwahusisha wabunge wa CHADEMA na meseji hizo badala ya kushughulika na watu walioingilia mawasiliano yao.

Alisema kwa nafasi yake, Werema kama msimamizi mkuu wa sheria nchini anajua wazi kuwa kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine ni kosa la jinai na mhusika anayefanya hivyo anapaswa kushtakiwa.

“Kitendo cha Jaji Werema kutoa maagizo ya kuandaa mashtaka kwa wabunge ni kuwasaidia wahalifu; tunachoweza kumuambia ni kwamba taarifa tunazo tutakutana mahakamani kuweka masuala haya wazi,” alisisitiza.

Alisema CHADEMA haitajishughulisha kulifikisha suala hilo mahakamani bali wanasubiri waitwe ili wakaudhihirishie umma namna viongozi wa CCM na watendaji wengine serikalini wanavyotumia vibaya nafasi zao kuwanyamazisha wapinzani wao kisiasa.

Alibainisha kuwa serikali ya CCM isidhani kuwafunga mdomo wakosoaji wake wa sasa ni suluhisho la ushindi kwao kwamba harakati za kudai uhuru wa kweli hazikuanza sasa na hazitaishia kwa kuwadhuru watu.

Wiki iliyopita mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu, alisimama bungeni na kuomba mwongozo wa Spika akidai kuwa amepokea ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA, akitishiwa kuuawa.
Chanzo: Tanzania Daima

Friday, July 20, 2012

Mauwaji Colorado

Best Blogger Tips
Mauwaji ya kutisha yametokea katika mji wa Aurora, ambao uko katika jiji la Denver kwenye jimbo la Colorado. Watu 12 wamefariki na wengine 50 wamejeruhiwa katika tukio hilo.

 Muuwaji aliingia katika ukumbi wa sinema (Movie Theater) na kuanza kupiga watu risasi wakati sinema ya Batman inayoitwa “The Dark Knight Rises" ikionyeshwa.

Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanzo walifikili wanachoona na kusikia ni sinema, lakini ukweli ni kwamba haikuwa hivyo, muuwaji aliingia kwenye ukumbi huo akitumia mlango wa tahadhali (Emergency exit door) dakika 30 baada ya sinema hiyo kuaanza.

Muuwaji ametambuliwa kwa jina la James Holmes, ana miaka 24, mkazi wa Aurora. Mama yake anaishi San Diego katika jimbo la California.  Alikamatwa kwenye eneo la kupaki magari la ukumbi huo wa sinema.

Rais Barack Obama na mkewe Michele wameelezea masikitiko yao kufuatia mauawaji hayo. Obama alisema kuwa serikali itafanya kila juhudi kuwasaidia watu wa eneo la tukio, la Aurora wakati huu mgumu.

Nakisi Ya Usaili, Mtaji Wa Ushirikina - Jenerali Ulimwengu

Best Blogger Tips
 NIMEKUWA nikisema kwamba tunahitaji kukua, na katika kukua tutende na tuenende kama watu wazima wasiohitaji ulezi wa karibu wa baba mkali wala uangalizi wa yaya.

Nimejaribu kuonyesha kwamba ingawaje mwanzoni mwa maisha yetu kama Taifa tulihitaji baba mkali wa kutuelekeza katika hatua zetu za mwanzo za kukua, hivi sasa hatumhitaji tena. Tunatakiwa tujitegemee, tujielekeze kama jamii iliyokomaa na ambayo hainyonyi dole-gumba tena.

Kwa bahati mbaya, bado tunazo dalili nyingi mno za jamii inayonyonya dole-gumba, jamii iliyoshindwa kukua na kukomaa, jamii changa ambayo uchanga wake ni wa tabia zisizofanana na wingi wa miaka ya umri wake. Katika mambo mengi ni jamii iliyovia.

Kinachotia hofu zaidi, kwa mtazamo wangu, ni kwamba hata katika yale mambo ambayo kwayo tulikwisha kuonyesha kwamba tunaanza kukomaa, tumefanikiwa kupata mbinu za kuturudisha uchangani.

Kwa mfano, miaka 50 ya Uhuru ni muda mrefu kwa jamii yo yote ile kuwa inatambua ni yapi matatizo yake yanayoisababishia unyonge, na ni nini inahitaji ili kujikomboa kutoka unyonge wa umasikini, ujinga na maradhi.

Utambuzi wa aina hii ni jambo la msingi mno, hata kama ufumbuzi utachukua muda mrefu ujao. Utambuzi huo unasaidia kuweka misingi ya kimkakati na hatua za kwanza za mbinu za  utekelezaji wa malengo hayo ya kimkakati.

Tunajua kwamba misingi hiyo ilikwisha kujengwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akisaidiwa na wazalendo wa kweli waliokabidhiwa majukumu wakati ule. Inawezekana kwamba wale vijana wasiopenda kuisoma nchi yao watakuwa hawajui hawa wazalendo ni akina nani waliomsaidia Nyerere kuweka misingi hiyo, lakini haiyumkiniki kwamba hata watu wa rika langu nao wanajifanya hawajui au hawakumbuki. Binafsi naamini kwamba hawataki, ama kwa sababu wanayo maslahi katika kutokumbuka au ni kutokana ule uvivu wa kufikiri tuliojijengea.

Tungekubali kuzisumbua kumbukumbu zetu kidogo tu tungeweza kuwatambua akina Amir Jamal, Amon Nsekela, Dickson Nkembo, Clement G Kahama, Derek Bryceson, Obeid Katikaza, Gabrieli Mawala, Cleopa Msuya… na wengine kama hao, pamoja na wale waliokuwa vijana, akina Bakari Mwapachu, Omari Abebe, Basil Mramba, Mbaruk Mwandoro na kadhalika.

Baadhi yao wamekwisha kututoka, na baadhi ya walio bado hai wanaweza kuonekana leo kama vile hawajawahi kuwa na thamani yo yote kwa sababu zama zao zimepita. Hata hivyo ni watu waliofanya kazi kubwa ya kuweka misingi fulani kama walivyoelekezwa na bosi wao, Nyerere.

Kazi waliyoifanya wakati ule ilitakiwa iendelezwe na kizazi cha vijana wa leo, iboreshwe na ipelekwe kwenye viwango vya juu zaidi,  lakini kwa sababu za upuuzi ambao nimekuwa nikiujadili, hilo halikufanyika, na wala sioni dalili kwamba watawala wetu wanalielewa hilo.

Hali hii ya kutokuthamini urithi wetu imetufanya sasa tutafute walezi wengine badala ya baba yetu, na walezi hawa ( ambao kwa hakika hawawezi kuwa na uchungu nasi) wanatuona kama “mazuzu” wa kutumiwa na watu wenye akili.

Wanatuona kama punguani kwa jinsi tunavyoweza kuendelea kuwa “omba-omba” miaka 50 baada ya Uhuru wakati tunazo rasilimali ambazo wao wanazimezea mate.

Nimewasikia, kwa mshangao mkubwa, watawala wetu wakitamka kwamba hawajui ni kwa nini nchi yetu ni masikini baada ya miaka yote hii na ikiwa na rasilimali zote hizi. Huko kutotambua ndiyo sababu mojawapo kubwa ya hali tuliyo nayo.

Haiyumkiniki kwamba mtu anaweza kugombea uongozi wa nchi au jamii, tena kwa juhudi kubwa na kwa kuahidi mambo lukuki, halafu baada ya kuwa ameingia madarakani akatangaza kwamba wakati wote huo alikuwa hajui matatizo ya jamii yake. Nini kilimsukuma kugombea?

Pasipo na shaka akilini mwangu, sababu moja kubwa iliyotufanya tukwame kiasi hiki imekuwa ni upuuzi wa uongozi na udhaifu wa watawala, vikiambatana na uwezo na utashi mdogo mno wa raia kuwasaili viongozi watawala wao na kusaili kila kilichowazunguka.

Tumefanikiwa kujenga jamii ya watu wasio na uwezo wa kusaili mambo ya msingi kabisa, na wasiotaka kuwasaili wale waliowakabidhi hatamu za uongozi, hata pale hao waliokabidhiwa hatamu hizo ni dhahiri kwamba wanazitumia vibaya; na matokeo yake ni kwamba wanawaumiza hao hao waliowaweka madarakani, na hao wanaoumizwa hawana la kufanya.

Kukosekana kwa utamaduni wa kusaili mambo yanayotuzunguka ndiko kunatufanya tuendelee kuamini kwamba binadamu anaweza kupaa kwa ungo; mwili wa albino una nguvu za miujiza; mtu anaweza kugeuka fisi na fisi akageuka mtu; kumbaka mtoto mchanga kunatibu Ukimwi…na ujinga mwingine wa aina hiyo.

Jamii isiyosaili mambo ni jamii ya wajinga, na wajinga wakisha kuwa wengi ndani ya jamii, hata weledi wachache ndani ya jamii hiyo hawafui dafu: watanyongwa.

Ndiyo maana tunapiga kelele siku zote kuhusu elimu bora, na elimu bora si ile ya kumeza “maarifa” bali ni ile inayomwezesha mtu kusaili mambo yanayomzunguka, kuuliza maswali ili apate majibu na kuuliza maswali kuhusu majibu anayopewa, na siku zote kuendelea kusaili hata yale mambo aliyodhani kwamba aliyaelewa awali. Ndivyo wenzetu walivyoendelea, na ndiyo sababu wako waliko nasi tunaendelea kurejea tulikotoka.

Bila shaka tunahitaji kuondokana na upuuzi na ujinga tulimozama iwapo tunataka kupiga hatua za kwenda mbele badala ya hizi za kurudi nyuma tunazozipiga kwa kasi leo hii (kwa sababu ni kweli tunarudi nyuma kwa kasi).

Mahali pa kuanzia ni mwanzo, na mwanzo daima  ni uongozi wa kisiasa. Siasa safi zitazaa mazingira safi ya watu kufanya kazi za kuleta maendeleo katika nyanja zote. Siasa hovyo zitajenga mazingira hovyo vivyo hivyo, ambayo yataendelea kutuzamisha katika upuuzi na ujuha.

Siasa zetu hazina budi kuwa na misingi ya usaili wa masuala yote yanayotuzunguka, na ziachane na unafiki wa wale wanaodhani kwamba kutosaili jambo au mtu ndio uaminifu na nidhamu.

Tukumbuke, wale wanaodhani viungo vya mwili wa albino vinaleta utajiri, au kwamba ungo ni helikopta, msingi wao mkuu ni kushindwa kusaili mambo na watu.

Katika siasa kushindwa kuwasaili wale waliokabidhiwa madaraka ya kuendesha jamii, au kushindwa kusaili miundo, mifumo na michakato inayoendesha jamii, ni ushirikina mwingine ambao matokeo yake ni kuidumaza jamii yetu. Htuna budi kupambana na dalili zo zote zinazotusukuma kutokomoea zaidi katika nakisi ya usaili.

Ndiyo maana napingana moja kwa moja na baadhi ya mambo yanayotamkwa na kufanywa na baadhi ya wakuu wa asasi za utawala nchini, ikiwa ni pamoja na wakuu wa shughuli za Bunge.

Ni kama vile wakuu hawa wa Bunge, pamoja na Spika na wasaidizi wake, wamo bungeni kuhakikisha watawala hawasailiwi, hawadadisiwi na hawakosolewi. Niliangalia kwa mshangao mkubwa ubishi kati ya Spika na mbunge aliyesema kwamba, pamoja na uzembe na upuuzi wa asasi nyingine, alibaini pia “udhaifu wa Rais,” na hili likawa ni tatizo kubwa lililositisha shughuli za Bunge kwa muda na likawa ni chanzo cha gumzo nchini.

Mimi najiuliza, iwapo mbunge wa upinzani atazuiwa kusema kwamba Rais, ambaye ni kiongozi wa chama tawala (ndiyo kusema chama anachokipinga mbunge huyo) ni dhaifu sasa aseme nini? Amsifu Rais kwa umahiri, ukakamavu na ushujaa? Apendekeze kwamba Rais abakie madarakani maisha, na chama chake kisipingwe? Kazi ya mbunge wa upinzani ni nini hasa?

Nadhani ni kutokana na ukali wa Spika kuhusu “udhaifu” wa Rais ndiyo ofisa mwandamizi serikalini akasimama bungeni kwa ukali kumshambulia mbunge aliyesema kwamba baadhi ya majaji hawafai na kwamba uteuzi wao ulikuwa wa kutiliwa shaka.

Ndipo nikatambua kwamba tunalo tatizo la msingi kuliko nilivyodhani mwanzo. Tatizo hilo ni la kifalsafa katika mfumo ambao msingi wake wa kidhana ni kwamba mkubwa hatiliwi shaka, na mambo yalivyo ndivyo yalivyo, na hakuna bora zaidi ya yalivyo.
Chanzo: Raia Mwema

Thursday, July 19, 2012

Uchina kutoa dola bilioni 20 kwa Afrika

Best Blogger Tips
Rais Hu Jintao
 Rais Hu Jintao, Uchina ameziahidi serikali za Afrika mkopo karibu dola za Marekani bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Amesema kuwa mkopo huo utasaidia katika ujenzi wa miundo mbinu, kilimo na maendeleo ya biashara.

Rais Jintao aliyasema hayo wakati wa mkutano wa ushirikiano baina ya Uchina na viongozi wa Afrika mjini Beijing.

Kuanzia barabara mpya za mjini Nairobi hadi wauza kuku katika soko la Zambia ni dhahiri kwamba Uchina imeweka nyayo zake katika kuinua uchumi wa Mataifa mengi barani Afrika.

Miundo mbinu ni mojawapo ya sehemu ambazo Uchina imewekeza vilivyo barani Afrika.

Biashara kati ya Bara Afrika na Uchina imeongezeka kutoka dola bilioni 10 miaka kumi iliyopita na kufikia takriban dola bilioni mia moja na sitini hii leo.

Nchi hiyo imetoa mikopo zaidi kuliko Benki ya Dunia.

Baadhi ya viongozi wa mataifa ya Afrika wamefurahia uhusiano huu wakisema kuwa utakomesha tabia na hali ya kukaliwa na Mataifa ya magharibi kiuchumi na kisiasa kwa masharti yanayoambatana na mikopo hiyo.

Kwa upande mwingine Uchina imeshutumiwa na nchi za magharibi kama yenye tamaa, hali inayoifanya kupuuza haki za utu na kupendelea maendeleo ya kiuchumi na mahitaji yake ya nishati.
Mataifa ya magharibi hayajasita kuinyooshea kidole Uchina kama Mkoloni mpya wa Afrika, kwa kutangaza rekodi yake ya ukiukaji wa haki za binadamu kwa kisingizio cha kuitojiingiza katika masuala ya ndani ya nchi wanakoendesha shughuli zao.

Mfano uliopo ni nchini Sudan ambako mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa uhusiano na Uchina, licha ya vitendo vya unyanyasaji vinavyoendelea huko Darfur.

Mashirika hayo yanaongezea kusema kuwa Uchina imesaidia katika kuchochea ghasia kupitia msaada wake wa fedha, silaha na sera.

Kwa upande wake Uchina imesisitiza kuwa itaendelea na sera yake ya kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine.

Mpango wa Uchina kwa Afrika ni bayana. Ina hamu ya maliasili kutoka Bara hilo pamoja na soko la bidhaa zinazotengenezwa Uchina. Vilevile, Uchina inataka kudhibiti ushawishi wake wa kibalozi ulimwenguni kwa msaada wa Afrika.

Hivyo ndivyo hali ilivyo kuhusu miradi ya Uchina kwa Afrika ambapo watu wengi hudhani kuwa Uchina ndiyo inayodhamini miradi yote.

Benki ya Maendeleo ya Afrika, ADB huenda ikahisi kuwa Wachina wameipokonya hadhi yake kutokana na kwamba watu wengi wanaonelea hata miradi ya Benki hiyo na kudhani imedhaminiwa na Wachina, ingawaje fedha zimetoka kwenye Benki hiyo lakini wahandisi na wajenzi ni Wachina.

Viongozi wa Kiafrika hukumbushwa kuhusu mshirika wao mpya wanapokwenda Addis Ababa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Jengo kabambe la kisasa lililojengwa kwa vioo na mawe kwa gharama ya dola milioni 200 lilidhaminiwa na Uchina, bila shaka.
Chanzo: BBC

Wednesday, July 18, 2012

Juhudi za uokozi zaanza Zanzibar

Best Blogger Tips
Meli iliyokuwa imewabeba takriban watu miambili imethibitiswha kuzama katika bahari ya hindi eneo la Chumbe kisiwani Zanzibar. Meli hiyo kwa jina Star Gate ilikuwa inatoka Dar Es Salam kuelekea Zanzibar.
Kulingana na taarifa za vikosi vya wanamaji , meli hilyo ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali.

Jeshi la polisi la wanamaji nchini Tanzania limeanza shughuli za kuwaokoa watu zaidi ya mbia mbili wanaohofiwa kuwa kwenye meli ya Skagit inayoripotiwa kuzama huko visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, ingawa hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo, lakini wamethibitisha kwamba meli hiyo imepigwa na dharuba ya upepo mkali katika eneo la Chumbe pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam kuelekea visiwani Zanzibar.

Itakumbukwa kwamba, ni takriban mwaka mmoja sasa tokea ajali ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.

Mwandishi wa BBC mjini Dar Es Salam, Aboubakar Famau anasema kuwa meli hiyo MV Skagit ilianza kuzama saa sita saa za afrika mashariki ikiwa inaelekea bara.

Safari kati ya bara na pwani huchukua saa mbili. Inaarifiwa huenda watoto thelathini na moja walikuwa kwenye meli hiyo.

Afisaa wa usalama katika bandari ya Zanzibar alifahamisha shirika la habari la Reuters kuwa meli hiyo sasa imebiruka.

"maiti kumi na wawili pamoja na manusura kumi tayari wameodolewa baharini kufikia sasa.

Shughuli za uokozi zinaendelea ingawa kuna changamoto ya hali mbaya ya hewa." hii ni kwa mujibu wa waziri katika ofisi ya rais Mwinyihaji Makame,

Kivukio kilichoko kati ya Dar es Salaam na Zanzibar huwa na shughuli nyingi sana na huvutiwa sana na watalii pamoja na wenyeji wa Tanzania.
Chanzo: BBC

Dunia yaadhimisha miaka 94 ya Mandela

Best Blogger Tips
 Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Nelson Mandela leo anatimiza miaka 94 tangu alipozaliwa.

Siku ya kuzaliwa kwake pia inaadhimishwa na Umoja wa Mataifa kutokana na mchango wake katika kuikomboa Afrika Kusini dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.

Na nchini Afrika Kusini kwenyewe Nelson Mandela, ataadhimisha siku hii na familia yake na Marafiki huku shughuli mbalimbali zikiandaliwa nchini humo kama katika kusherehekea siku hii.

Mwandishi wa BBC wa Afrika Kusini, Omar Murtasa, amesema kuwa Mzee Mandela anaheshimiwa na watu wengi nchini humo, wakitambua juhudi zake za kupigania Uhuru wa Taifa hilo lilolokuwa likiongozwa kirasmi na Ubaguzi wa rangi.

Ripoti zinasema raia wa nchi hiyo hii leo watajitolea kufanya kazi ya kuwasaidia wasiojiweza kwa muda wa dakika sitini na saba kama njia moja ya kuadhimisha siku hii.

Mandela aliachikiliwa huru kutoka gerezani akiwa na umri wa miaka 67.

Mandela alichaguliwa kuwa rais wa Afrika Kusini mwaka wa 1994.
Source: BBC

Monday, July 16, 2012

Wabunge wote vijana kupigishwa kwata JKT

Best Blogger Tips
 WABUNGE vijana walioko katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watapaswa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa Mujibu wa Sheria kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2012/13.
Waziri wa Ulinzi na JKT, Shamsi Vuai Nahodha alisema hayo alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya wizara yake bungeni jana. Alisema wabunge vijana watakuwa sehemu ya kundi la kwanza la vijana 5,000 katika mafunzo yatakayoanza Machi, mwakani.

Alisema wizara hiyo imelifanyia kazi ombi la kuandaa mafunzo ya JKT kwa wabunge vijana kama ilivyoombwa mwaka jana na kwamba wabunge hao wameandaliwa mafunzo hayo ya wiki tatu.
“Nafurahi kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba Wizara yangu imelifanyia kazi ombi hilo na kuandaa utaratibu wa mafunzo maalumu ya wiki tatu kwa waheshimiwa wabunge vijana,” alisema Nahodha na kuongeza:

“Kwa hiyo wabunge vijana wataungana na kundi la kwanza la vijana 5,000 niliowaeleza hapo juu… naomba waheshimiwa wabunge mjiorodheshe kwa maandalizi ya mafunzo haya.”
Waziri Nahodha alisema ni imani yake kuwa, pamoja na wabunge kunufaika na mafunzo hayo, watahamasisha urejeshwaji wa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria na kutoa taswira nzuri ya mafunzo hayo kwa jamii.

Alisema JKT tayari imefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kambi tano zenye uwezo wa kuchukua vijana 20,000 kwa wakati mmoja zimeshaandaliwa kwa ajili hiyo.
Alizitaja kambi hizo kuwa ni Bulombora na Kanembwa za mkoani Kigoma, Mlale ya Ruvuma, Msange mkoani Tabora na Oljoro hukoArusha.

Hata hivyo, alisema gharama ya kuendesha mafunzo hayo ni kubwa hivyo JKT haitaweza kuchukua vijana wote na ndiyo maana imeamua kuanza na hao 5,000.
“Vijana hao ni miongoni mwa vijana 41,348 ambao watahitimu mafunzo ya kidato cha sita katika mwaka 2013,” alisema Nahodha.

Kuhusu utaratibu wa kujiunga na kambi hizo, Nahodha alisema uandikishaji wa vijana shuleni utafanyika kati ya Desemba mwaka huu na Januari 2013 na kwamba kambi zitawapokea kati ya Machi 7 na 16, mwakani.Alisema mafunzo hayo ya miezi sita yataanza Machi 17 mwakani na kuendelea hadi Agosti 16.

Wanajeshi Syria

Katika hatua nyingine, Nahodha alisema wanajeshi wa Tanzania kati ya 100 na 200 wanatarajiwa kwenda Syria kuwa waangalizi wa amani ikiwa ni kuitikia ombi la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa Serikali.

Alisema ombi hilo linatokana na utendaji mzuri wa jeshi hilo na kwamba tayari Serikali imelikubali.
Nahodha alisema tayari Makao Makuu ya Jeshi yameanza maandalizi ya kuwapeleka waangalizi hao.
Alisema Tanzania ina wajibu wa kushirikiana na nchi nyingine kulinda amani duniani na imekuwa ikishiriki katika operesheni mbalimbali za kulinda amani.

Katika hatua nyingine; Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Christowaja Mtinda alilalamikia kitendo cha Wahindi kuuza bidhaa za maduka ya jeshi kwa gharama za juu, wakati bidhaa hizo hazilipiwi kodi.
Alisema ni lazima Serikali ieleze Wahindi hao wanauzaje bidhaa za kwenye maduka ya jeshi kwa gharama kubwa wakati maduka hayo yanatakiwa yauze bidhaa hizo kwa bei ya chini.

“Ukienda sasa hivi wanauza sukari Sh1,800 wakati nje ya maduka hayo sukari kilo ni Sh2,000, hili haliwezekani. Wanauza friji, tv kwa bei ya juu na TRA, maofisa wa jeshi wa ngazi za juu wote wanajua,” alisema.

Mtinda alitaka suala hilo litafutiwe ufumbuzi ili bidhaa ziuzwe kwa bei inayotakiwa. Pia alilalamikia nyumba za maofisa wa jeshi akisema haziridhishi na kwamba zinahitaji kukarabatiwa upya.

“Nyumba za maofisa wa jeshi zinatia aibu, hazijakarabatiwa kitu ambacho kinasababisha wafanye ukarabati kwa fedha zao wenyewe,” alisema.

Wapinzani wang’aka

Kwa upande wake, Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu wizara hiyo, Mchungaji Israel Natse aliitaka Serikali kutoa maelezo ya matumizi ya Sh4.048 bilioni ambazo zilitumika kuondoa matrekta bandarini.
“Hakika fedha hizi ni nyingi sana kwa kazi ya kuondoa tu matrekta bandarini, Kambi ya Upinzani inataka kupata majibu ni matrekta mangapi yaliondolewa na gharama ya kuondoa trekta moja ilikuwa kiasi gani?” alisema Natse alipokuwa akitoa maoni ya kambi hiyo.

Natse ambaye pia ni Mbunge wa Karatu (Chadema) alisema malipo hayo yanatia shaka na kwamba Serikali lazima ieleze fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya matumizi gani.
Kuhusu migogoro ya ardhi, mbunge huyo alisema kumekuwapo na migogoro kwa muda mrefu baina ya wanajeshi na wananchi kwenye maeneo mbalimbali ya nchini na kwamba ni kama hakuna dalili kwamba kuna nia ya dhati ya kumalizwa kwa matatizo hayo.

“Migogoro hii imesababisha kuwapo kwa mvutano baina ya wananchi na jeshi letu kwa upande mmoja na viongozi wa wananchi kwa upande wa pili,” alisema Natse.
Alitoa mfano wa maeneo hayo kuwa ni Ilemela, Tarime, Kunduchi na mengine mbalimbali ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wabunge kwa muda mrefu.

“Mara zote Serikali imekuwa ikitoa majibu kuwa itawalipa fidia wananchi ili waweze kuondoka na kuyapisha maeneo hayo kwa ajili ya jeshi, kwa mwaka huu wa fedha 2012/13 zimeombwa kiasi cha Sh1 bilioni kwa ajili ya kulipa fidia ya ardhi maeneo ya Mapinga, Shinyanga na Arusha.”
Alisema kutokana na fedha hizo ni dhahiri kwamba hakuna nia ya dhati ya kumaliza migogoro baina ya jeshi na wananchi kwani kiasi hicho kilichotengwa ni kidogo na ni kwa ajili ya kulipa fidia na sehemu chache tu.

“Tunaitaka Serikali iwe na nia ya dhati ya kuwalipa wananchi fidia ili kumaliza migogoro hii ambayo inawafanya wananchi walichukie jeshi lao,” alisema.
Chanzo: Mwananchi

Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits