Ndugu Wananchi,
Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa
Rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza nusu ya kwanza ya
mwaka 2012 salama. Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza nanyi kila
mwisho wa mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili. Jambo la kwanza
ni suala la usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili ni la
mgomo wa madaktari.
Usafirishaji Haramu wa Binadamu Nchini
Ndugu Wananchi;
Bila ya shaka mtakuwa mmezisikia taarifa za tukio la kushtusha na kuhuzunisha la kukutwa maiti 43
za watu wasiojulikana, zilizotupwa katika kichaka kilichopo kijiji cha
Chitego, Wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma tarehe 26 Juni, 2012. Pamoja
na maiti hao, walipatikana watu 84 wakiwa hai lakini wote wakiwa
wamedhoofu na baadhi yao wakiwa mahututi.
Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao hadi Dodoma ambapo wale waliokuwa mahututi walifikishwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na wengine walihifadhiwa katika Kituo cha Kati cha Polisi, Dodoma. Maiti 22 zilipelekwa Dodoma na 21 zilipelekwa Morogoro kuhifadhiwa.
Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao hadi Dodoma ambapo wale waliokuwa mahututi walifikishwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na wengine walihifadhiwa katika Kituo cha Kati cha Polisi, Dodoma. Maiti 22 zilipelekwa Dodoma na 21 zilipelekwa Morogoro kuhifadhiwa.
Taarifa
zilizopatikana kutoka kwa wale walionusurika zimebainisha kuwa watu hao
ni raia wa Ethiopia ambao walikuwa safarini kwenda Malawi na baadaye
Afrika ya Kusini ambako wangetengenezewa utaratibu wa kwenda kuishi
Marekani na Ulaya.
Kwa mujibu wa maelezo yao, safari yao ilianza miezi
mitano iliyopita. Mwezi mmoja waliutumia Ethiopia na miezi minne
waliitumia Kenya kabla ya kuletwa Arusha ambako walipakiwa kwenye lori
na kuanza safari ya kuelekea Malawi lakini ikaishia Chitego. Lori
walilopanda lilikuwa limezibwa kabisa na hivyo kusababisha vifo kwa
kukosa hewa.
No comments:
Post a Comment