Muuwaji aliingia
katika ukumbi wa sinema (Movie Theater) na kuanza kupiga watu risasi wakati sinema
ya Batman inayoitwa “The Dark Knight Rises" ikionyeshwa.
Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanzo walifikili
wanachoona na kusikia ni sinema, lakini ukweli ni kwamba haikuwa hivyo, muuwaji
aliingia kwenye ukumbi huo akitumia mlango wa tahadhali (Emergency exit door)
dakika 30 baada ya sinema hiyo kuaanza.
Muuwaji ametambuliwa kwa jina la James Holmes,
ana miaka 24, mkazi wa Aurora. Mama yake anaishi San Diego katika jimbo la
California. Alikamatwa kwenye eneo la
kupaki magari la ukumbi huo wa sinema.
Rais Barack Obama na mkewe Michele wameelezea masikitiko yao
kufuatia mauawaji hayo. Obama alisema kuwa serikali itafanya kila juhudi kuwasaidia watu wa eneo la
tukio, la Aurora wakati huu mgumu.
No comments:
Post a Comment