Utafiti umebaini kwamba dawa iliyokuwa
ikitolewa na mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila maarufu kama babu wa
Loliondo ni feki na kwamba haina uwezo wa kutibu Ukimwi wala kisukari.
Hayo yalielezwa bungeni jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.
Hussein Mwinyi, alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na
matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2012/13.
Alisema utafiti wa kulinganisha wagonjwa wa ukimwi na kisukari
waliokunywa dawa hiyo na wale ambao hawakunywa umebaini kwamba hakuna
utofauti wa afya ya mgonjwa.
Alisema utafiti huo unafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa
ya Binadamu (NIMRI), ulianza Machi mwaka huu na kwamba unahusisha
wagonjwa 200 wanaofuatiliwa kwa kupimwa damu, kinga ya mwili (CD4) na
uzito wa mgonjwa, ambao ulifanyika tangu mgonjwa alipokunywa kikombe cha
babu.
“Matokeo ya awali ya utafiti yameonyesha kuwa hakuna utofauti katika
vipimo vya kimaabara pamoja na damu, CD4, uzito na ubora wa afya ya
wagonjwa kati ya waliokunywa na wale ambao hawakunywa dawa ya
mchungaji,” alisema Dk. Mwinyi.
Alisema lengo la utafiti huo ni kubaini uwezo wa dawa hiyo katika kutibu
magonjwa aliyosema dawa yake inayatibu ili kuona kama kuna utofauti
wowote baada ya mgonjwa kutumia dawa.
Chanzo: Ippmedia
Tuesday, July 31, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment