NYOTA wa kimataifa wa mchezo wa kikapu, Hasheem Thabeet wa Tanzania,
ambaye ameshindwa kung'ara kwenye Ligi ya NBA tangu aliposhika nafasi ya
pili kwenye mashindano ya vyuo mwaka 2009, amesaini mkataba wa miaka
miwili kuichezea timu ya Oklahoma City Thunder, limeripoti gazeti la
Daily Oklahoman.
Thabeet alitasaini rasmi mkataba huo mpya Julai
11 mwaka huu.Makubaliano ya mkataba huo hayajawekwa wazi, lakini taarifa
zinasema kuwa ni mkataba wa kudumu wa misimu yote miwili.
Kwa mujibu wa Oklahoman, Thabeet atalipwa mshahara wa dola 880,000 (Sh1.3 Bilioni) katika mwaka wake wa kwanza wa mkataba.
Gazeti
hilo limeeleza kwamba, mshahara huyo ni mdogo zaidi kulipwa kwenye
ligi.Thabeet mwenye urefu wa futi 7.3, anajiunga na timu hiyo mpya,
ikiwa ni ya nne kwake katika misimu minne ya kucheza tangu mwaka 2009.
James
Harden, Tyreke Evans, Stephen Curry, Jrue Holiday, Brandon Jennings na
Ricky Rubio ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa toka kwenye
mashindano ya vyuo baada ya Thabeet mwaka 2009.Akiwa amecheza michezo
135 ya Ligi Kuu ya Kipapu Marekani (NBA), Thabeet ana wastani wa pointi
2.2 ya kucheza mipira inayorudi na pointi 0.9 ya kuzuia.
Wastani
huo ni sawa pointi 1.8 na 2.1 kwa mipira inayorudi katika mechi 20,
lakini kwa zile tano ya mwisho akiwa na timu ya Houston, na michezo 15
akiwa na timu ya Portland.
Chanzo: Mwananchi
Saturday, July 7, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment