INAKADIRIWA kuwa Jiji la Dar es Salaam, linazalisha tani 4,252 za
taka kwa siku na kwamba ni kati ya asilimia 26 na 37 tu, zinazozolewa na
kutupwa dampo.Hayo yalisemwajana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk
Didas Masaburi, katika hotuba yake katika warsha kuhusu kubuni mikakati
ya kusimamia usafi wa mazingira ya jiji.
Warsha hiyo
inawashirikisha wadau mbalimbali wa mazingira.Meya huyo alisema majiji
mengi katika nchi zinazoendelea, yana mazingira machafu ikilinganishwa
nay ale ya nchi zilizoendelea na kwamba hali hiyo inatokana na
changamoto nyingi ukiwemo ukomo wa bajeti.
Hali kadhalika wingi
wa watu wanaohamia mjini na mipangilio mibovu ya miji.Dk Masaburi
alisema kwa assa Jiji la Dar es Salaam, linakadiriwa kuwa na wakazi
milioni nne na nusu huku ongezeko la wahamiaji likiwa limefikia
asilimia 4.3.
Alisema ongezeko hilo la watu, limesababisha Jiji hilo kukua kwa kasi kubwa.
“Asilimia 70 ya watu hao wanaishi katika maeneo yasiyopimwa na mimi ni miongoni mwao,” alisema Dk Masaburi.
Alisema
ongezeko hilo la watu, limesababisha mamlaka za halmashauri,
kushindwa kumudu kutoa kwa ufanisi, huduma za miundombinu ya barabara,
afya, majisafi, maji taka na mipango miji .
Alibainisha kuwa Jiji la Dar es Salaam, linakadiriwa kuzalisha wastani wa tani 4,252 za taka kwa siku.
Alisema
kwa kuzingatia changamoto hizo, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa
kushirikiana na wadau wengine, imeanzisha sehemu ya kutengeneza mbolea
ya mboji kwa kutumia takarejea, zinazotokana na mabaki ya vyakula
mbalimbali.
Kwa mujibub wa meya, mbolea hiyo ya mboji inahitajika
kwa kiwango kikubwa na wakulima wadogo wadogo na itasaidia kuwa sehemu
ya vyanzo kwa vikundi vya kijamii vinavyojishulisha na udhibiti wa taka
jijini. “Lakini pia itasaidia kupunguza hewa ya Carbon inayotokana na
taka zenye kemikali zinazosababisha madhara kwa binadamu ukiwemo ugonjwa
wa kansa,” alisema.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Taka katika
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Membe Protus, alisema Jiji hilo
ni la tatu barani Afrika linalokua kwa haraka.
Alisema pia ni
moja ya majiji 12 machafu duniani.Alisema halmashauri zinafanya kazi ya
kukusanya uchafu kwa shida kutokana na upungufu wa vifaa, ikiwemo vya
kuteketeza taka hatarishi husasani zile za hospitali na zenye
kemikali.
Chanzo: Mwananchi
Friday, July 27, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment