Kaimu balozi wa Venezuela nchini Kenya Olga Fonseca ameuawa na watu
wasiojulikana.
Kitengo cha polisi wanaoshughulikia usalama wa maafisa wa
kibalozi nchini Kenya kimeupata mwili wa balozi huyo mwenye umri wa
miaka 57 nyumbani kwake katika mtaa wa Runda.
Balozi huyo amewasili
nchini Julai 15 kuchukuwa mahala pa mtangulizi wake Gerardo Carrillo
ambaye aliondoka Kenya baada ya wafanyakazi wa kike kwenye ubalozi wa
Venezuela kumtuhumu kwa dhuluma za kimapenzi.
Afisa mkuu wa polisi
Nairobi Area Antony Kibuchi amesema kuwa ishara zote zinaonyesha kuwa
balozi huyo alinyongwa nyumbani kwake alfajiri.
Amesema kwamba polisi
wanachunguza masuala mbali mbali kuhusiana na kifo hicho ikiwemo habari
kuwa huenda wafanyakazi aliowafuta kazi wamekuwa na kisasi naye.
Balozi
huyo aliwafuta kazi baadhi ya wafanyakazi waliodai mtangulizi wake
alikuwa akiwadhulumu kimapenzi. Tayari wafanyakazi wawili wa ubalozi huo
wametiwa nguvuni.
Chanzo: Radio Maisha
Friday, July 27, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment