Rais wa kwanza wa kiraia wa Misri, na kutoka chama cha Kiislamu,
Mohammed Morsi, ameapishwa, na ametoa wito kuwa bunge la nchi lirejeshwe
haraka - bunge lilofutwa hivi karibuni.
Katika sherehe kwenye eneo la jeshi nje ya Cairo, kiongozi wa wakuu
wa jeshi wanaoongoza nchi, Field Marshal Mohammed Tantawi, alikabidhi
madaraka rasmi kwa Rais Morsi.
Hapo awali, akitoa hotuba yake ya kwanza
iliyogusia mambo mengi, katika Chuo Kikuu cha Cairo, Bwana Morsi alisema
atalilinda jeshi kama taasisi, lakini piya alionya jeshi halifai kuwa
mbadala wa matakwa ya wananchi.
Bwana Morsi aliahidi ukurasa mpya utaong'ara katika historia ya nchi, kufwatilia ule aliosema ni ukurasa wa kuchusha.
Alipokuwa akizungumza, akina mama ambao watoto
wao waliuliwa chini ya utawala wa Rais Mubarak, walibeba juu picha za
watoto wao hao wa kiume.
Bwana Morsi piya alisema Misri haitotapakaza mapinduzi nchi za nje.
Rais mpya aliapishwa kwenye sherehe iliyofanywa katika mahakama ya katiba mjini Cairo.
Chanzo: BBC
Saturday, June 30, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment