WANASIASA nchini, wametakiwa kuacha kujihusishana suala la katiba na badala yake, suala hilo liachwe mikononi mwa wananchi.
Rai
hiyo ilitolewa jana na jijini Dar es Salaam na Kiongozi wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ,Askofu Dk Alex Malasusa,
alipokuwa akizungumz katia uzinduzi wa Usharika wa Kinyerezi.
Dk
Malasusa alisema katiba ya nchi si mali ya wanasiasa wanaotaka kuiteka
nyara na kwamba hiyo ni mali ya Watanzania, wanaopaswa kupewa uhuru wa
kujadili kwa kina.
Dk Malasusa alisema wananchi wanapaswa kuwa na
fursa kubwa ya kuboresha mchakato wa kuandika katiba hiyo, lakini
wanakwamishwa na asilimia kubwa ya wanasiasa, wanachangia.
“Sina
ugomvi na wanasiasa katika suala hili, ila naomba wawaachie wananchi,
kwanza ili wapate fursa ya kuchangia maoni yao,” alisema Dk
Malasusa.Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia maoni
yao ili kuboresha katiba inayotarajiwa kuandikwa kwa manufaa ya
wananchi wote.
“Wote mjitokeze na kutoa maoni yenu, msikae kimya
katika mchakato huu, alisema Dk Malasusa.Pia aliwataka waumini wa
kanisa hilo, kubadilika na kufanya mambo yasiyomchukiza Mungu.Alisema
lengi la kanisa hilo ni kujaribu kuwasaidia waumini wake, ili waweze
kubadilika na si vinginevyo.
Chanzo: mwananchi
Monday, June 11, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment