WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amewapiga vijembe aliowaita
maadui zake kisiasa wanaomchafua katika majukwaa mbalimbali akisema
kuwa, hawamuwezi na hawamnyimi usingizi.
Lowassa akitambia
maadui zake, kambi yake nayo imezidi kujizatiti baada ya mshirika wake
kisiasa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amefanikiwa
kukalia kiti cha Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi hivyo kuzidi
kuongeza nguvu kwenye bungeni.
Jana, akiwa mkoani Arusha katika
harambee ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika
wa Elaira, Lowassa alitumia sehemu ya muda wake kuwapiga vijembe maadui
zake pasipo kuwataja majina akisema kamwe hawamnyimi usingizi.
Lowassa
ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, alitoa kauli hiyo, baada ya Askofu wa
Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer kumtaka aendelee kufanya
kazi ya Mungu licha ya baadhi ya watu kumkatisha tamaa.
Akizungumzia
kauli ya Askofu Laizer, Lowasa alisema mahasimu wake kisiasa wamekuwa
wakimsema kupitia vyombo mbalimbali vya habari, lakini akatamba kwamba
juhudi hizo hazitaweza kufua dafu kwake kwani kelele zao hazimnyimi
usingizi.
“Wanaonisema kwenye magazeti wala hawanisumbui, nasema
hawaninyimi usingizi kwa kuwa mimi namtegemea yule anitiaye nguvu
daima,” alisema Lowasa, kitendo kilichosababisha kushangiliwa na
waumini waliohudhuria kanisani hapo.
Aliongeza kuwa yeye daima
humtegemea Mungu amtiaye nguvu na kamwe hawezi kushindwa kulala
usingizi kwa kusikiliza kelele zao za mara kwa mara.
“Nakushukuru
Baba Askofu kwa kunijibia, wale wote wanaonisemasema kwenye magazeti
wala hawanisumbui na wala hawaninyimi usingizi,” alisema Lowasa.
Alisema
kwamba yeye ataendelea kumtumikia Mwenyezi Mungu ambaye amtiaye nguvu
siku zote bila kujali maneno ya mahasimu wake wa kisiasa.
Kabla
ya kuendesha harambee hiyo, Lowasa aliwaongoza waumini wa kanisa hilo
kwa nyimbo zilizopo kwenye Kitabu cha Tenzi za Rohoni na kuibua shangwe
kanisani hapo.
Kambi yake yajizatiti
Chenge ambaye ni mshirika mkubwa wa Lowassa kisiasa amechaguliwa katika
kamati nyeti ya Bunge ya Fedha na Uchumi, akizidi kuongeza nguvu kwenye
mhimili wa kambi hiyo.
Lowassa mwenyewe anaongoza Kamati ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama huku mshirika wake mwingine,
Peter Serukamba akiongoza Kamati ya Miundombinu.
Katika
uchaguzi wa juzi wa kamati hiyo uliotawaliwa na malalamiko ya vitendo
vya rushwa bila kuelezwa ilikuwa ikitolewa na kambi ipi, aliyechaguliwa
kuwa Makamu Mwenyekiti ni Dunstan Kitandula ambaye ni mbunge wa
Mkinga.
Uchaguzi huo ulikuwa wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk Abdallah Kigoda aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda hivi karibuni.
Akizungumzia uchaguzi huo jana, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah
alisema, Chenge alipata nafasi hiyo baada ya kumshinda Mbunge wa Lupa,
Victor Mwambalaswa.
“Mwambalaswa alikuwa Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Fedha na Uchumi kabla ya uchaguzi, hivyo aliamua
kujiuzulu ili kugombea nafasi ya uenyekiti na Chenge, lakini
akashindwa," alifafanua Dk Kashillilah.
Alipotakiwa kuzungumzia
mizengwe na rushwa iliyotawala kwenye uchaguzi huo, Dk Kashililah
alisema hawezi kuzungumzia hilo kwa sababu hakuwepo kwenye mchakato wa
upigaji kura.
“Wanaoweza kuzungumzia hilo ni wale waliopiga
kura ndiyo wanaweza kuelewa kama kulikuwa na mazingira ya rushwa lakini
mimi sikuwapo,” alisema.
Tayari kambi ya Lowassa pia
inaonekana kuwa na nguvu katika baadhi ya kamati kutokana na k
uwa na
washirika wenye msimamo wa wastani akiwemo Agustine Mrema wa Kamati ya
Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali Kuu (PAC) inayoongozwa na John Cheyo, Kamati ya Hesabu za
Mashirika ya Umma (POAC) inayoongozwa na Zitto Kabwe na hata Kamati ya
Bunge ya Katiba ya Sheria na Utawala inayoongozwa na Pindi Chana.
Chanzo: Mwananchi
Sunday, June 3, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment