Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amejibu pendekezo la
Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba la kutaka wapinzani
waombewe, akisema hakuna kanuni yoyote ya uchumi inayosema Serikali
ikiendesha mambo isivyo yanafanyika maombi.
Badala yake, alisema
yeye ambaye ni mchungaji huwa wanaombea wazinzi na watu waotembea na
wake za watu, na si matatizo ya kiuchumi.
“Inashangaza sana kuona
watu wanaunga mkono bajeti…, kila mwaka deni la taifa linaongezeka na
sasa limefika Sh20 trilioni, fedha ambazo ukizigawanya kila Mtanzania
atakuwa anadaiwa Sh400,000” alisema Msigwa.
“Nilivyokuwa naona
wabunge wamevaa suti na wanachangia hoja bungeni nilipenda jambo hilo na
kutamani siku moja niwe mbunge, lakini baada ya kuingia bungeni
nimegundua kuwa hakuna kitu.”
Alisema bunge hilo hivi sasa
halieleweki na kwamba mbunge mwenye elimu ya kutosha akisimama kuchangia
hoja huwezi kumtofautisha na mtoto wa darasa la pili.
“Yaani
mbunge profesa akisimama kuchangia hoja huwezi kumtofautisha na mtoto wa
darasa la pili, watu wenye akili, akili zao wameziweka mfukoni na
kuweka ushabiki wa vyama mbele, tumekuja bungeni kumaliza matatizo sio
kuongeza matatizo” alisema Msigwa.
Huku akitumia mifano ya
wanasaikolojia mbalimbali Msigwa alisema ni aibu kuona Watanzania
wanazidi kuwa maskini harafu kila mwaka yanayozungumzwa ni tofauti na
yanayotendeka.
“Ufikie wakati wabunge tutambue kuwa tumekuja hapa
bungeni kuwatumikia wananchi, Watanzania waliotuchagua wanateseka na
wabunge hapa bungeni mnazungumza maneno ya khanga tu,” alisema Msigwa.
Chanzo: Mwananchi
Tuesday, June 19, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment