Wahamiaji wanne wa kiafrika wamejeruhiwa baada ya
makaazi yao kuteketezwa na watu wanaoaminika kuwa wenyeji mjini
Jerusalem, Israel.
Hapo Jumapili sheria mpya ilipitishwa kuwapa mamlaka maafisa wa uhamiaji kuwazuilia korokoroni wahamiaji haramu kwa miaka mitatu.Waathiriwa wa shambulio la sasa ni raia wa Eriterea ambapo walipata majeraha ya moto mikononi.
Msemaji wa polisi nchini Israel Micky Rosenfeld ameambia BBC kwamba kumekuwa na matukio mengi ambapo waafrika weusi wamekuwa wakilengwa na wenyeji.
Katika majuma ya karibuni ghasia zilitokea miji kadhaa ya Israel wanakopatikana wahamiaji wa kiafrika. Kusini mwa jiji kuu Tel Aviv biashara za waafrika zilishambuliwa huku waafrika wenyewe wakikejeliwa hadharani.
Polisi wanasema takriban wahamiaji elfu 60 wa kiafrika wanaishi Israel ambapo 35,000 wakikaa Tel Aviv na 5,000 wakiwa mjini Jerusalem.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment