Dkt
Ulimboka anadaiwa kuvunjwa mbavu, miguu yote miwili, kung’olewa meno yote ya
mbele na kuumizwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio
hilo la kikatili na kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia leo jijini Dar es
Salaam, na linadaiwa kufanywa na watu wa sio julikana ambapo kabla ya kufanya
unyama huo walidaiwa kumteka na kumpiga kabla ya kumtelekeza katika eneo la
msitu wa Pande Mabwepande.
DKT.
ULIMBOKA ASIMULIA TUKIO
Akisumulia
tukio hilo Dkt Ulimboka alisema kuwa jana usiku alipigiwa simu na mtu
aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea
naye, na ndipo walipopanga kuonana katika eneo la Leaders Kinondoni.
Dk
Ulimboka aliyekuwa akiongea kwa tabu, aliendelea kusimulia kuwa wakati akiongea
na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa akifahamiana naye kabla, alikuwa na wasiwasi
kwani kila mara alikuwa akipokea simu na kuwasiliana na watu wengine ambao
hawakuwapo eneo hilo.
Alisema
baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa na
silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha Polisi na kumvuta na kumuangusha
barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.
Dkt
Ulimboka alisema kuwa wakiwa njiani walimpiga, na kumfikisha katika msitu huo
wa pande na kuendelea kumpiga paka alipoteza fahamu.
MADAKTARI
NAO WALONGA
Akisimulia
mkasa huo mmoja wa madaktari wenzie aliyefahamika kwa jina moja la Dkt Deo,
alisema kuwa alipigiwa simu na mtu hasiyemfahamu na kumfahamisha tukio hilo.
Alisema
alipofika katika kituo cha Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika hali mbaya
na ilikuwa ngumu kumtambua kwakuwa alikuwa na majeraha mengi eneo la usoni.
Aliongeza
kuwa akiwa na wenzie waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili kwaajili ya matibabu.
"Hali
yake kwakweli ni mbaya sana, amepigwa mno na ameumizwa kwakweli tumemleta hapa
hili aweze kupata matibabu, lakini mimi nilivyomkuta mara ya kwanza nilishindwa
hata kumtambua kwa jinsi alivyokuwa ameumizwa"alisema Dkt Deo
Alisema
kuwa alisimuliwa na Dkt Ulimboka kwamba watu hao waliomteka na kumpiga walikuwa
na silaha na kwamba alishindwa kuwatambua.
Aliongeza
kuwa Dkt Ulimboka alidai kuwa wakati akiwa katika halimbaya alikuwa akisikia
mazungumzo yao, wakibishana juu ya kumuua wengine wakisisitiza achomwe sindano,
na wengine wakitaka kumpiga risasi.
Alisema
wakati mabishano yakiendelea kati yao, Dkt Ulimboka aliinuka akiwa na lengo la
kukimbia lakini watu hao walipiga risasi hewani iliyomshtua na kuangua chini.
Kwa
upande wake Dkt Cathbeth Mcharo ambaye ndiye aliyempokea Dkt Ulimboka Hospitalini
hapo, alisema kuwa hali yake ni mbaya na kwamba wanajitahidi kumpatia huduma za
haraka.
Alisema
kuwa kwa hatua za awali amefanyiwa vipimo mbalimbali, hili iweze kufahamika
aina ya matibabu anayotakiwa kupatiwa.
POLISI
Kamanda
wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova amezungumza na
waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la utekaji nyara na kujeruhi lililompata
kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano
wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda
Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina
lake kiusalama na kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema huyo alimuokota
Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha
Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven
Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda
Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya
uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza
kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio
hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha
matukio mengine kama hayo
MUHIMBILI
Wakati
hayo yakitokea inadaiwa kuwa Askari Kanzu mmoja alikumbana na kipigo kikali
kutoka kwa madaktari hapo Muhimbili kwa kile kilochodaiwa kutambuliwa na Dkt
Ulimboka kuwa mmoja wa watu walio mjeruhi.
Pia
inadaiwa kuwa Askari huyo aliingia chooni na kufanya mawasiliano na wenzake
huku Madaktari hao wakimsikiliza na kutokana na alichokua akiongea chooni humo
ndipo alipotoka aliambulia kichapo kikali.
Pia
baadhi ya madkatari na wauguzi walikuwa wakisukuma gari alilokuwa amepanda Dkt
Ulimboka huku wakiimba nyimbo za Umoja na Mshikamano Daima miongoni mwao.
Hali
ya ulinzi ilikuwa kali Hospitalini hapo kwani Picha zilikuwa haziruhusiwi
kupigwa.
Chanzo: Father Kidevu
Chanzo: Father Kidevu
No comments:
Post a Comment