Sunday, April 15, 2012

Msani Lulu atendewe haki na haki ionekane inatendeka

Best Blogger Tips
Lula wa Ndali Mwananzela

Msiba wa Msanii maarufu zaidi wa filamu Tanzania Stephen Kanumba umekuja na kutuachia mshtuko kupita kiasi. Kutokea kwake katikati ya Ijumaa Kuu na Pasaka kwa kweli umefanya sikuu ya Pasaka (yenye kuadhimisha ufufuko) kuwa na maana ya pekee kwa baadhi yetu. Sisi wengine tayari tulikuwa tunaomboleza kuondokewa kwa aliyekuwa Inspekta Generali wa Polisi Mzee Harun G. Mahundi hatukutarajia mioyo yetu kuchomwa na msiba mwingine ndani ya muda huo. Lakini Mungu ni Mungu kwani nina uhakika wapo watu wengine wengi tu ambao walikuwa kwenye misiba mingine wakati huo huo na msiba wa Kanumba ukaja kama kidonda kingine.

Kilichoshtua wengi zaidi na hasa tuliopata habari mapema zaidi ni nini kilitokea. Taarifa za mwanzo kama ilivyotarajiwa zilikuwa na utata sana maana wengine walianza kusema ilikuwa ni ajali ya gari huko Mbagala wakati wengine wakitaja vyanzo mbalimbali. Lakini baada ya muda taarifa zikawa wazi zaidi kwamba kifo cha Kanumba kimesababishwa kwa namna moja au nyingine katika mazingira ya ugomvi wa kwenye nyumba (domestic conflict) ambao matokeo yake ni mmoja kufariki. Na kilichokuwa wazi mapema hiyo ni kuwa msanii mwingine maarufu Elizabeth Michael a.k.a Lulu alikuwa anahusika.

Mara moja hata hivyo baadhi ya watu walianza kueneza habari kuwa “Lulu kamuua Kanumba” na wengine kwenda mbali na kumuita “muuaji”. Niliwasoma wengine wakielezea kifo cha Kanumba kama “mauaji” bila ya shaka wengine wakishindwa kujua kuwa baadhi ya lugha wanayotumia ina maana ya kisheria zaidi. Kwamba Kanumba ametutoka hilo halina ubishi lakini ni mazingira gani yalisababisha hilo hilo ni suala la kitaalamu na la kisheria. Hapa ndio hoja ya Lulu kutendewa haki inapokuja kwa sababu tusipoangalia kutokana na maumivu tuliyonayo ya kupotelewa na mtu tuliyempenda mno basi tunapoteza macho yetu ya haki na tunajenda macho ya kisasi ambayo hayataki kuutafuta wala kuujali ukweli.

Niwashirikishe maneno yenye hisia hizo yaliyoandikwa na mmoja wa wanaForum wa JamiiForums.com akijaribu kuturudisha kwenye fikra za kujali haki bila kumuangalia nani atanufaika na haki hiyo. Yaani, badala ya kuangalia ni “Lulu” anahusika basi tumweke huyo “Lulu” kama ni mdogo wetu, binti yetu, rafiki yetu n.k na amefanya kitu ambacho pia kimemsababishia mauti ndugu, rafiki au jamaa yetu mwingine; je tungependa atendewe vipi? Ni wazi wengi tungependa atendewe haki; asionewe, asidhulumiwe au kupendelewa. Yaani, isije kuwa watu ambao walikuwa na chuki na Lulu kabla ya tukio hili ndio wanakuwa wa kwanza kupiga debe la “muuaji muuaji” kumbe wanathibitisha tu midomoni mwao kile wanachokiamini moyoni kutokana na chuki.

Mwanachama huyo aitwaye WomanofSubstance aliandika hivi katika mtandao huo na nimebandika hapa ili kutupa fikra na sisi wengine:

Naanza na kutoa Pole kwa watanzania wote, hasa ndugu jamaa na marafiki wa karibu wa Kanumba The Great (R.I.P) kabla sijatoa mchango wangu kuhusu hili jambo zito na nyeti ambalo limetawala maongezi katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka. Mengi yamesemwa na pia kuna mengi pia hayajasemwa, moja wapo likiwa "ujinai" wa Lulu katika kifo cha Kanumba.

Katika mukatadha wa sheria, tunaona kwamba Tanzania ni moja ya nchi zenye kuuweka uwajibikaji kijinai kuwa chini ya UMRI wa miaka 18 kwa kuweka miaka 10 kama umri ambapo mtu anaweza kushtakiwa kwa kosa la jinai. (Linganisha na Kenya miaka 8, Zimbabwe -7,Zambia 8,Africa Kusini 10) n.k. Ina maana kwamba mtu (mtoto) aliye chini ya umri huu hawezi kushtakiwa labda ithibitishwe kuwa alikua anajua kabisa anachokifanya. Lulu hafit kwenye kundi hili hata kama ana umri wa miaka 17 kama ambavyo Mh Halima Mdee ame tweet leo baada ya kumtembelea LuLU Oysterbay Polisi.

Tukiacha sheria na matakwa yake, kwa kuzingatia yale yanayosemwa kuhusu mkasa huu wa kifo cha Kanumba (R.I.P), inatupasa tuone kuwa kila hadithi ina pande mbili. Hadithi ya Kanumba ambaye kwa sasa hayupo kuelezea, na hadithi ya Lulu aliye mahabusu. Inasikitisha sana kwamba kifo kimetokea katika mazingira ya kutatanisha. Kifo hiki kimesikitisha watu wengi na kufanya udadisi wa kutaka kujua ukweli ulio objective iwe vigumu. Watu wamebakia kushusha lawama ZOTE kwa Lulu tu bila kutaka kujua haswa ilitokea nini hadi kifo hicho kikatokea.
Endelea kusoma habari hii..............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits