Wednesday, November 7, 2012

Obama wins second term in the White House

Best Blogger Tips
WASHINGTON — President Barack Obama says the American people have "picked ourselves up" and fought back during tough economic times, declaring after winning re-election that the "best is yet to come."

Obama says he wants to meet with Republican rival Mitt Romney to discuss how they can work together. He says they may have "battled fiercely, but it's only because we love this country deeply."

The president rolled to a second term over Romney, winning more than 300 electoral votes. Only one state's electoral votes hadn't been called by The Associated Press as of early Wednesday morning. In Florida, Obama has a 46,000-vote lead, with 100 percent of precincts reporting. But Florida historically has left as many as 5 percent of its votes uncounted until after Election Day, making the race too close to call until state officials complete their count, the AP said.

In victory, Obama spoke to thousands of cheering supporters, praising Romney and promising that better days are ahead. "While our road has been hard, though our journey has been long, we have picked ourselves up. We have fought our way back and we know in our hearts that for the United States of America, the best is yet to come," he said.

Romney made a graceful concession speech before a disappointed crowd in Boston. He summoned all Americans to pray for Obama and urged the night's political winners to put partisan bickering aside and "reach across the aisle" to tackle the nation's problems. Romney said earlier he called Obama to congratulate him on his victory, adding that he prays "the president will be successful in guiding our nation."

Obama triumphed despite a weak economy that plagued his first term and put a crimp in the middle class dreams of millions.

After the costliest - and arguably the nastiest - campaign in history, divided government seemed alive and well. Democrats retained control of the Senate with surprising ease. Republicans did the same in the House, making it likely that Speaker John Boehner of Ohio, Obama's partner in unsuccessful deficit talks, would reclaim his seat at the bargaining table.

At Obama headquarters in Chicago, a huge crowd gathered waving small American flags and cheering. Supporters hugged each other, danced and pumped their fists in the air. Excited crowds also gathered in New York's Times Square, at Faneuil Hall in Boston and near the White House in Washington, drivers joyfully honking as they passed by.

With votes counted in 75 percent of the nation's precincts, Obama held a narrow advantage in the popular vote, leading by about 25,000 out of more than 99 million cast.

But the president's laserlike focus on the battleground states allowed him to run up a 303-206 margin in the competition for electoral votes, where the White House is won or lost. It took 270 to win.

Obama captured Ohio, Wisconsin, Iowa, New Hampshire, Colorado and Nevada, seven of the nine states where the rivals and their allies poured nearly $1 billion into dueling television commercials.
Romney won only North Carolina among the battleground states. Four years ago, Obama had carried the state.

Florida remained too close to call, a state where long lines of voters kept the polls open in some areas well past the appointed poll close time.

Here’s how it shaped up for the candidates.

Barack Obama won:Virginia, Nevada, Wisconsin, Oregon, Colorado, Iowa, New Mexico, California, Hawaii, Washington, Minnesota, New Hampshire, Pennsylvania, New Jersey, New York, Michigan, Vermont, Delaware, District of Columbia, Maine, Maryland, Massachusetts, Connecticut, Rhode Island, and Illinois .

Mitt Romney won:Missouri, Idaho, North Carolina, Arizona, Utah, Arkansas, Mississippi, Louisiana, North Dakota, South Dakota, Texas, Wyoming, Kansas, Nebraska, Kentucky, West Virginia, South Carolina, Indiana, Oklahoma, Tennessee and Georgia.

The election emerged as a choice between two very different visions of government - whether it occupies a major, front-row place in American lives or is in the background as a less-obtrusive facilitator for private enterprise and entrepreneurship.

The economy was rated the top issue by about 60 percent of voters surveyed as they left their polling places. But more said former President George W. Bush bore responsibility for current circumstances than Obama did after nearly four years in office. That bode well for the president, who had worked to turn the election into a choice between his proposals and Romney's, rather than the simple referendum on the economy during his time in the White House.

Unemployment stood at 7.9 percent on election day, higher than when he took office. And despite signs of progress, the economy is still struggling after the worst recession in history.

About 4 in 10 said the economy is on the mend, but more than that said it was stagnant or getting worse more than four years after the near-collapse of 2008. The survey was conducted for The Associated Press and a group of television networks.

Thursday, October 25, 2012

Buriani Julius Kambarage Nyerere

Best Blogger Tips
Jenerali Ulimwengu
 MWALIMU Julius Kambarage Nyerere amefariki. Baba kaondoka. Jua limekuchwa. Mbuyu mkuu uliotanda katikati ya kijiji umenyauka. Zama zimefikia tamati. Watanzania ni yatima.

Ilani ilitolewa kwa muda wa kutosha. Wiki kadhaa za mateso ya maradhi ya Mwalimu katika Hospitali ya Mtakatifu Tomaso, mjini London, ingetakiwa iwe ni taarifa ya mapema ili watu wake wajiandae kwa lolote ambalo lingetokea. Kwa hakika taarifa za siku za mwisho zilionyesha wazi kwamba hakuwa mgonjwa wa kupona.

Hata hivyo, tangazo rasmi la kifo chake limeweza kuwashitua Watanzania, kama vile lilikuwa jambo lisilotarajiwa. Hali hii inaelezeka kwa utambuzi wa uhusiano maalumu kati ya Mwalimu na Watanzania, ambao walikataa kulizoea wazo la kifo chake.

Hadi jana asubuhi (Oktoba 14, 1999) wengi waliamini kwamba hata pale sayansi ya juu ilipokomea bado muujiza ungetokea na baba yao akainuka kitandani na kupanda ndege kurejea nchini.

Haiwezekani kuwalaumu hata wale walioshawishika kuegemea hisia za ushirikina. Watanzania walitaka mzee wao apone, na hawakukata tamaa hadi dakika ya mwisho. Ukweli ni kwamba hawakujua ni vipi wangeweza kuishi kama taifa bila Nyerere.

Haishangazi. Kwa muda wa nusu karne, nchi hii imetambulika na kujitambulisha kwa jina la Julius Kambarage Nyerere. Tangu alipojiunga na harakati za kudai uhuru mwanzoni mwa miaka ya 1950, Nyerere hajawahi kuondoka katika hisia za Watanzania.

Aliongoza kampeni ya uhuru kwa ujasiri mkubwa na kwa kufanya kazi bila kuchoka. Alitembelea kila kona ya nchi hii, akiwahamasisha wananchi kukataa ukoloni na kujiunga naye kudai uhuru. Kwa jinsi hii alijipatia fursa muhimu ya kuielewa nchi na watu wake, ujuzi ambao ulimfanya kuwa kiongozi aliyekuwa karibu na wananchi wake kuliko viongozi wengi wa Afrika na dunia.

Hata baada ya uhuru, alipokuwa kiongozi wa dola, hakuacha mtindo wake wa kwenda hadi vijijini, si katika sherehe na ngoma, bali kupiga kambi na kufanya kazi za sulubu bega kwa bega na wanavijiji, huku akiwafundisha alichokijua juu ya kilimo, au afya au ujenzi wa nyumba bora na huku akijifunza kutokana na uzoefu wa wananchi.

Baadhi yetu bado wanakumbuka kambi za Mwalimu katika mikoa ya Dodoma na Kigoma. Alikuwa mwalimu wa kweli, na alipenda kulifundisha taifa lake. Alijua kueleza dhana ngumu na tata kwa lugha nyepesi. Aidha alikuwa na kipaji cha ucheshi kilichomrahisishia mawasiliano.

Pia alikuwa ni msikilizaji makini aliyeweza kuhifadhi taarifa za maelezo marefu na misururu ya takwimu. Watanzania walimjua Nyerere kama kiongozi shupavu aliyeweza kukemea uovu, hasa dhidi ya wanyonge.

Alikuwa mtetezi asiyechoka wa watu wasiokuwa na uwezo na alipingana na kila aina ya unyanyasaji uliofanywa na watu wenye utajiri au vyeo. Alichukia rushwa na alipigana nayo hadi mwisho wa maisha yake.

Alikuwa safu ya mbele katika kupambana na ukoloni, ubeberu na ubaguzi na hakusita kuwakemea wakubwa wa dunia hii kila walipoonyesha dalili za kuwaonea au kuwapuuza wanyonge.

Mwalimu alikuwa miongoni mwa miamba wachache waliotetea haki za nchi ndogo na masikini katika mahafali yote ya kimataifa.

Alikuwa kiongozi asiyetetereka katika misimamo yake na uthabiti huo ulimwezesha kuwaongoza vyema Watanzania katika raha na katika taabu, katika amani na katika vita, Idi Amin alipovamia nchi yetu mwaka 1978 Nyerere alionyesha maana halisi ya cheo cha Amiri-Jeshi Mkuu kwa kusimamia mwenyewe maandalizi ya kivita ya kumwadhibu Amin na kujenga mawasiliano ya mara kwa mara na wananchi ili kuwaeleza kuhusu maendeleo ya vita. Kwa kumwondoa Amin madarakani, Nyerere alikuwa amesaidia dunia kuondokana na mwendawazimu hatari.

Mwalimu aliishi maisha ya kawaida, akakataa mbwembwe na ukwasi unaowatambulisha viongozi wengi wa nchi masikini. Alikwepa anasa na akajijengea mazingira yaliyowasuta wapenda makuu hapa nchini na nje ya nchi. Watu wa nchi nyingine walimstaajabu kwa mwenendo wake wa kujinyima katika mavazi na itifaki, tofauti kabisa na wenzake.

Katika mambo ambayo tungeweza kujifunza kutoka kwa Mwalimu Julius Nyerere ni ari yake ya kutaka kujua na kujiendeleza kila wakati. Wasomi wengi wameziacha bongo zao zikaota magugu kwa sababu ya kutojisomea. Mwalimu alisoma wakati wote, hata wakati akionekana kachoka. Jinsi hii aliweza kujipatia ujuzi na taarifa ambavyo vilimfanya awe na uwezo wa hali ya juu wa kuelewa masuala mbalimbali ya dunia.

Fursa ya kukaa na Mwalimu kwa muda wa saa moja wakati wowote ilikuwa ni fursa ya kunywa maji kutoka kisima cha elimu. Si bure kwamba Mwalimu Nyerere aliendelea kuenziwa na wananchi wa Tanzania, hata miaka mingi baada ya kuwa ameondoka madarakani. Kila wakati Mwalimu alipoitisha mkutano na waandishi wa habari, waandishi na wahariri waliingiwa na shauku kubwa ya kujua anataka kusema nini. Na kila alilosema lilichukuliwa kwa uzito mkubwa.

Si rahisi kufikiria mtu yeyote mwingine ambaye angeweza, kama Mwalimu, kufuta azimio la Bunge la kutaka iwepo serikali ya Tanganyika, mwaka 1993. Wala si rahisi kumfikiria mtu ambaye angeweza, kama Nyerere, kusema fulani hafai kugombea urais, na huyo fulani asigombee. Watu waliokuwa na bahati mbaya ya kukemewa na Nyerere hadharani walijikuta wanatembea na aibu muda mrefu.

Nguvu zake hazikuishia nchini. Kila alikokwenda Mwalimu Nyerere aliwavuta waandishi wa habari, wasomi na viongozi wakuu. Walimsikiliza kwa sababu walitambua kwamba ni mtu makini, mwenye akili na anayetetea maslahi ya watu wake na watu wa dunia ya tatu walio wanyonge na kwamba hakutafuta kujitajirisha binafsi.

Kwamba Rais wa Marekani, Bill Clinton na Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair walitaka wamlipie gharama za matibabu ni ishara ya jinsi alivyokuwa akithaminiwa na viongozi wa nchi za nje.

Heshima yote hii alipewa kwa sababu alitambulika kama mmoja wa Waafrika wachache walioweza kuongoza nchi zao kwa misingi ya ubinadamu na bila kuwaibia watu wao katika Bara lililojaa majambazi wanaojiita wakuu wa nchi, hii si sifa ndogo.

Hakuwa mtu wa kawaida. Sikuwahi kufanya kazi naye kwa muda mrefu, lakini mara chache nilipopata nafasi ya kuwa naye niligundua kwamba watu walioishi naye kwa muda mrefu halafu wakashindwa kujifunza kufikiri walikuwa na matatizo makubwa.

Ukali wa ubongo wake ulikuwa wa kusisimua na wenye uwezo wa kutekenya ubongo wako nao ufanye kazi. Mwalimu Nyerere ameliongoza taifa hili tangu mwaka 1954 na kwa muda wote huo, Watanzania wamemjua kwamba ndiye kiongozi namba moja.

Wako watu waliojaribu kubeza jina la “Baba wa Taifa” katika miaka ya karibuni, lakini sasa wametulia. Kwa karibu kila mtu, hilo ndilo jina lake na hiyo ndiyo hadhi yake.

Haishangazi, basi, kwamba wapo watu wenye wasiwasi kutokana na kifo chake. Wako wanaodhani kwamba baada ya kuondoka kwake, nchi itaingia kipindi cha mashaka makubwa, hata kuvurugika kwa amani.

Wako wanaodhani kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utavunjika kwa sababu mwasisi wake ametoweka. Hii inatokana na ukweli kwamba, Mwalimu hakusita kumkemea mtu yeyote, wa Bara au Visiwani, aliyemwona kama anataka kuuvunja Muungano.

Sasa ni dhahiri kwamba hakuna mtu atakayekuwa na uzito wa kuweza kuwakemea wachafuzi, na hawa ni wengi. Aidha yako makundi ya watu nchini yanayodhani kwamba kifo cha Mwalimu kinawaacha katika hali inayoweza kuwaletea matatizo, wakaonewa, kunyanyaswa au kudhuriwa kwa namna nyingine.

Watanzania wenye asili ya nje wanao wasiwasi wa aina hiyo. Baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani kadhalika wanaamini kwamba katika uhai wake, Mwalimu alikuwa ni kinga dhidi ya matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani.

Inawezekana hisia zote hizi hazina msingi na kwamba watu wanahofu zinazotokana na kukojua mustakabali wa taifa hili utakuwaje. Kila taifa hupata mashaka kama haya linapoondokewa na kiongozi wake mwasisi. Waasisi ni watu adimu. Hutokea mara moja katika maisha ya taifa. Mwalimu ni miongoni mwa hao. Anachangia nafasi na George Washington, Simon Bolivar, Jose Marti, Mahtma Gandhi/Jawaharlal Nehru na wengine kama hao.

Kwa sababu kufa ni lazima, waasisi nao hufa. Wanapokufa huacha majonzi na hofu, lakini wanaobaki baada yao wanatakiwa kuwa na moyo mkuu, kuelewa kwamba kifo cha mwasisi, kiwe na majonzi kiasi gani, si mwisho wa dunia.

Maisha lazima yaendelee. Njia moja muhimu ya kumuenzi Nyerere kama Baba wa Taifa na mwalimu wetu ni kudhihirisha kwa vitendo kwamba ni kweli alikuwa baba mwema aliyelea vizuri, na mwalimu mahiri aliyetufundisha tukaelimika na tukawa na busara. Tujitahidi kuepuka chokochoko na ukorofi unaoweza kuleta mfarakano katika jamii.

Tukifanya hivyo tutakuwa tumeheshimu wasia wake. Vinginevyo, tutaruhusu migawanyiko isiyo na maana. Au tukianza kuwaonea wanyonge na kuruhusu mambo ya hovyo katika jamii yetu tutakuwa tunamtukana baba yetu na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunajitukana wenyewe.

Taifa hili sasa linahitaji moyo mkuu na mshikamano wa hali ya juu, pamoja na ukomavu unaotakiwa kwa kila mwana ampotezaye mzazi wakati amekwishakukomaa.

Mola ailaze roho ya Mwalimu mahali pema peponi. Amina.

Makala hii ya tanzia iliyoandikwa na Jenerali Ulimwengu ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa gazetyi hili la Raia Mwema, ilichapishwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la Mtanzania, Oktoba 15, mwaka 1999, siku moja baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Tumeichapisha hapa kutokana ujumbe wake mzito kwa Watanzania-Mhariri Mkuu.
Chanzo: Raia Mwema

Wednesday, October 17, 2012

Vurugu kubwa Dar, Zanzibar

Best Blogger Tips
 POLISI mkoani Dar es Salaam na wale wa Kisiwani Zanzibar, jana walitumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kusambaratisha makundi ya watu wanaodaiwa kuwa waumini wa Dini ya Kiislamu, waliopanga maandamano kushinikiza kuachiwa kwa viongozi wao.

Kisiwani Zanzibar vurugu kubwa ziliibuka baada ya kusambaa taarifa kuwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed alitekwa nyara juzi saa 3 usiku akiwa kwenye gari lake na dereva wake.

Vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa mali kadhaa ikiwamo Maskani Kaka ya Kisonge inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo ilichomwa moto na waandamanaji.


Waandamanaji hao pia walichoma moto baa za Darajani na Mbawala eneo la Mikunguni na baadhi ya nyumba za kulala wageni, kabla Vikosi vya Kutuliza Ghasia (FFU) na Kikosi cha Zima Moto kudhibiti vurugu hizo kwa mabomu ya kutoa machozi.

Pia magari kadhaa yalichomwa moto na kuharibiwa vibaya yakiwa yameegeshwa katika maeneo mbalimbali, huku mipira na matairi vikichomwa katika barabara kadhaa.

Katika maeneo ya Mjini baadhi ya njia zilifungwa na watu waliokuwa wakitoka kazini walishindwa kwenda nyumbani. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni yale ya Malindi, Darajani hadi Michenzani ambako njia zilifungwa na mabomu yalisikika yakipigwa mfululizo.

Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheik Abdallah Said alisema,
“Taarifa tulizonazo ni kwamba Sheikh Farid ametoweka katika mazingira ya kutatanisha…Alitoka kwake Mbuyuni katika gari yeye na kijana wake wa hapo nyumbani, lakini baadaye kuna gari ikamfuata na kusimama na ndipo alipoingia katika hilo gari jingine na hakuonekana tena. Hatujui ni kina nani waliomchukua na hatujui ilikuwaje akaingia katika hilo gari ...”

Polisi waliimarisha ulinzi katika baadhi ya maeneo hasa Msikiti wa Mbuyuni ambao uko jirani na makazi ya Sheikh Farid. Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema polisi halihusiki na kukamatwa kwa Farid, lakini wao wanaamini kwamba ‘amejipoteza’ mwenyewe na kujificha.

Kamishna Mussa alisema polisi watawasaka wote waliosababisha vurugu hizo, na kwamba hadi sasa hawafahamu chanzo chake bado.

“Tunafanya uchunguzi zaidi kujua chanzo cha fujo hizo ingawa mimi sijui habari za kutekwa Farid, sasa tunasema tunachunguza chanzo cha vurugu hizo na tukishapata uthibitisho na waliosababisha tutawafikisha mahakamani kujibu mashtaka,” alisema kamishna huyo.

Ilivyokuwa Zanzibar
Vurugu hizo zilianza katika maeneo mbalimbali muda mfupi baada ya vijana kadhaa kukusanyika katika eneo la Darajani kando ya Soko Kuu majira ya asubuhi, kutokana na kuzagaa kwa taarifa kwamba Sheikh Farid alikuwa haonekani.

Idadi ya vijana hao ilikuwa ikiongezeka kadiri muda ulivyosonga, huku wengi wao wakiwa na silaha za aina mbalimbali zikiwamo magongo na mawe, hali iliyoibua hofu kwa wafanyabiashara wa eneo hilo, hivyo baadhi yao waliamua kufunga maduka.

Maeneo yalioharibiwa ni pamoja na baadhi ya nyumba za kulala wageni ambazo zimechomwa moto katika eneo la Amani, huku baadhi ya vijana wakionekana wakikimbia na kreti za pombe.

Katika eneo la Darajani, vijana kadhaa wakishirikiana na Wamachinga, walionekana wakivunja kisha kuingia katika moja ya maghala ya kuhifadhia bia, ambako walipora bidhaa zote zikiwamo kreti kadhaa za bia zilizokuwa zimehifadhiwa humo.

Baadhi ya wenye maduka walifunga na kutoweka, lakini waporaji waliiba baadhi ya bidhaa vikiwamo vyakula, kisha  kutokomea navyo kusikojulikana.

Katika maeneo ya Ng’ambo ambayo ni Amani, Mikunguni, Kwerekwe na Daraja Bovu vijana walioonekana kuwa na hamasa, waliingia kwenye makazi ya watu na kuiba vitu kadhaa, na kila mabomu yalipopigwa walikimbilia vichochoroni na baada ya muda walirejea tena.

Maeneo ya Malindi, Michenzani na  Rahaleo, kulikuwa na vurugu za urushaji mawe na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu katika maeneo hayo.

Matawi ya miti ilikatwa na kuunganishwa na magari mabovu kuwekwa barabarani kisha kuchomwa moto. Hali hiyo ilisabababisha uharibifu mkubwa katika baadhi ya barabara, na katika fujo hizo baadhi ya vijana walikamatwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohammed alithibitisha kutokea kwa fujo hizo na kusema Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kujua chanzo chake na taarifa kamili zitatolewa baada ya kukamilika uchunguzi huo.

Ponda Dar
Jijini Dar es Salaam, baadhi ya watu walipanga kufanya maandamano hadi Makao Makuu ya Polisi, kupinga kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekamatwa juzi usiku na kushikiliwa kutwa nzima ya jana katika Kituo Kikuu cha Polisi.

Ponda alitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani jijini Dar es Salaam, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisisitiza kuwa polisi wamechoka kuvumilia harakati zake za kutaka “nchi isitawalike”.

“Kuanzia leo uvumilivu kwa Jeshi la Polisi dhidi ya watu wasiofuata sheria za nchi umekwisha. Kwa kuwa Ponda ni mtu anayepotosha watu waliopo chini yake wanaotaka kuandamana bila utaratibu wasitulaumu kwa lolote lile litakalotokea,” alisema Kova.

Kova alisema hadi jana Ponda alikuwa bado anahojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Mkoa wa Dar es Salaam na kwamba ushahidi ukijitosheleza, atafikishwa mahakamani wakati wowote.

Alisema taasisi anayoingoza Sheikh Ponda haijasajiliwa kwa mujibu wa sheria kufanya shughuli za dini. Hivyo basi shughuli zote zinazoendesha na taasisi hiyo si halali.

"Natoa wito pia kwa wafuasi wa kiongozi huyo, walioshiriki katika vurugu mbalimbali za hivi karibuni, wajisalimishe haraka kwa kuwa sasa tupo katika mchakato wa kuwasaka, kuwakamata na baadaye kuwafikisha mbele ya sheria," alisema.

Tuhuma za Ponda
Kamanda Kova alidai kuwa Sheikh Ponda amekuwa akichochea vurugu na kuwashawishi wafuasi wake kuidharau Serikali na vyombo vya usalama.

“Ponda amekuwa ni mtu ambaye amefanya nchi hii, hasa katika Jiji la Dar es Salaam kukaa katika hali ya wasiwasi. Ijumaa imekuwa siku ya fujo badala ya kuwa siku ya amani,” alisema Kova.

Alisema vurugu hizo zinazoongozwa na Sheikh Ponda zimekuwa zikisababisha baadhi ya watu kushindwa kwenda kazini siku za Ijumaa na hali hiyo haivumiliki tena.

Kamanda Kova alitaja tuhuma nyingine dhidi ya Sheikh Ponda kuwa ni kuongoza kundi la watu kwenda kuvamia kiwanja namba 311/3/4 eneo la Chang’ombe ambacho kinamilikiwa  na kampuni Agritanza.

"Kiwanja alichokwenda kukivamia kilikuwa mali ya Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) na kiliuzwa kihalali kwa kampuni hiyo," alisena.

Alitaja tuhuma nyingine kuwa ni kufanya maandamano kinyume cha sheria, ikiwamo kuweka kambi Makao Makuu ya Polisi bila kibali cha jeshi hilo wiki kadhaa zilizopita.

Kamanda huyo alisema Ponda anashikiliwa pia kwa kuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola  na Serikali, ikiwa ni pamoja na kushawishi wafuasi wake kumdharau Rais wa nchi.

“Vilevile amekuwa akiendesha maandamano na kukusanyika Kiwanja cha Kidongo Chekundu, huku wakijitapa kuwa wana nguvu zaidi ya Jeshi la Polisi,” alieleza Kova.

Polisi pia wanamtuhumu Ponda kwa kuanzisha vurugu na vitisho dhidi ya Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mufti Shaaban Bin Simba na kutaka kumtoa madarakani kwa nguvu pamoja na kutaka kuvamia ofisi yake.

Alikamatwaje?
Kamanda Kova alisema Ponda alikamatwa na askari waliomuwekea mtego kutokana na yeye kuwa bingwa wa kutoroka kila akifanya matukio.

“Askari waliowekwa maalumu kwa ajili ya kumkamata walifanikiwa kumtia nguvuni saa 4:00 usiku karibu na eneo la maficho yake ambako alipelekwa na pikipiki,” alisema Kova.

“Hivi Ponda ni nani mpaka awe na uwezo wa kumpa Rais aliyechaguliwa na wananchi siku saba kuwaachia watu waliopo mahakamani yeye amechaguliwa na nani kuongoza taasisi aliyonayo na anatoa wapi nguvu za kufanya mambo yote hayo?,” alihoji Kova.

Alisema kulingana na matukio anayoyaongoza Ponda, wananchi wameanza kuona kama anaogopwa na vyombo vya dola, jambo ambalo siyo kweli.

Aliongeza kuwa polisi wana uwezo wa kumdhibiti, isipokuwa walikuwa wanatumia busara tangu alipoanza vurugu na kwa sasa uvumilivu umewashinda, hivyo wataanza kumshughulikia.

Vurugu zazuka
Kukamatwa kwa Sheikh Ponda kulizua vurugu jijini Dar es Salaam na kufanya baadhi ya wakazi wake hasa maeneo ya Mnazi Mmoja na Kariakoo, kuingiwa kiwewe baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha ili kuwasambaratisha watu waliokuwa wanataka kuandamana kwa lengo la kushinikiza kiongozi huyo aachiwe.

Hali hiyo ilisababisha watu kukimbia ovyo katikati ya iji na kuongezeka kwa misongamano ya magari, jambo lililofanya usafiri wa daladala kuwa mgumu kwenda na kutoka katikati ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyabiashara walifunga maduka yao wakihofia kuporwa mali wakati wa vurugu hizo, baada ya vibaka kujichanganya wakijaribu kufanya uhalifu huo.

Katika eneo la Mnazi Mmoja, polisi walirusha maji ya kuwasha kusambaratisha kundi la watu hao, huku wengine wakiwa wanadhibitiwa walipokuwa wakienda Makao Makuu ya Polisi ili kumtoa kiongozi huyo.

Baadhi ya mashuhuda walisema, mbali na Ponda watu hao walikuwa wanataka kwenda polisi kuwatoa watu waliokuwa wanashikiliwa kituoni hapo kwa tuhuma za kufanya vurugu na kuharibu makanisa katika Kata ya Mbagala wilayani Temeke.
Chanzo: Mwananchi

Saturday, October 13, 2012

Mshtuko mauaji ya RPC Mwanza

Best Blogger Tips
 SIMANZI imegubika Jiji la Mwanza na vitongoji vyake baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (55),  kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa  manane wa kuamkia jana.Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Said Mwema alithibitisha tukio hilo akieleza kuwa amemwagiza Kamishna wa Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba kwenda kuchunguza mauaji hayo.

“Tunasikitishwa kwa mauaji hayo na ninawaomba Watanzania wawe watulivu wakati tukishughulikia kuwakamata watu waliohusika katika tukio hilo,” alisema IGP Mwema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Mbali ya kumuua Kamanda Barlow, wauaji hao waliokuwa wamevalia makoti yanayovaliwa na watu wa ulinzi shirikishi (Polisi Jamii), walichukua na bastola ya kamanda huyo, simu mbili za mkononi pamoja na ‘radio call’ ya Jeshi la Polisi.

Hili ni tukio la tatu kwa Ofisa wa juu wa Polisi kuuawa mkoani Mwanza. Tukio la awali lilitokea mwaka 2007, ambapo aliyekuwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi Mwanza, ASP Mahende aliuawa kwa kupiga risasi eneo la Bugando saa 4:00 usiku wakati akifuatilia majambazi waliokuwa wakijitayarisha kuvamia.

Mwaka 1987, Inspekta Gamba aliuawa na majambazi katikati ya Jiji la Mwanza.
Kamanda Barlow aliuawa wakati akiendesha gari lake binafsi, aina ya Toyota Hilux Double Cabin na wakati wa tukio hilo hakuwa na mlinzi wake kwa kuwa kamanda huyo alikuwa katika shughuli binafsi.

Hata hivyo, mauaji hayo yamezua hisia tofauti huku wengine wakieleza kuwa ni kifo cha bahati mbaya na kwamba, wauaji walidhani ni mwananchi wa kawaida na wengine wakisema huenda ulikuwa mpango maalumu uliolenga kumwangamiza kwa kulipiza kisasi.

Taarifa ya Mkuu wa Mkoa
Akizungumza na waandishi wa habari jana saa 2:57 asubuhi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema kuwa kifo cha Kamanda Barlow kimetokea saa 8:00 usiku katika eneo la Kitangiri, Barabara ya Kona ya Bwiru karibu na Hoteli ya Tai Five.

Alisema kuwa kamanda huyo aliuawa alipokuwa akimrejesha mmoja wa wanawake waliokuwa nao katika kikao cha maandalizi ya harusi ya ndugu yake.

Mkuu huyo wa mkoa alimtaja mwanamke huyo aliyekuwa na marehemu kuwa ni Doroth Asasia Moses ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyamagana B.

 “Marehemu alikuwa katika kikao cha harusi ya anayedaiwa kwamba ni mtoto wa dada yake, Semburi Moleto kilichofanyika katika Hoteli ya Florida, Mtaa wa Rufiji. Kikao kilipomalizika tunaambiwa majira ya kati ya saa 4 hadi 5 usiku, alimchukua mwanamke huyo kama ‘lift’ ili kumsaidia kufika nyumbani kwake,”alieleza.

Alisema kuwa alipofika nyumbani kwa mwanamke huyo aliona watu waliokuwa wakimulika tochi  waliokuwa wakilalamika kuwa wameumizwa na mwanga wa taa za gari lake.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema walipofika katika gari, aliwauliza iwapo wanamfahamu na waliposhindwa kumjibu Kamanda Barlow alichukua radio ya mawasiliano ya kipolisi ili kuwasiliana na askari wake, ndipo wauaji hao walimpiga risasi eneo la shingo na kufariki papohapo.

“Kamanda wetu inaonekana amefariki kutokana risasi hiyo, ambayo imemvunja shingo yake na imepigwa kutokea upande wa kiti cha abiria na kumpitia begani na kuingia shingoni,” alisema Ndikilo na kufafanua:

“Baada ya kumuua, watu hao walipora bastola yake, ‘radio call’ hiyo pamoja na simu zake mbili za mkononi na mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na kusaidia upelelezi.”

Kilichomponza RPC
Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinamkariri shuhuda wa tukio hilo (Dorah) akieleza  kwamba, kilichomponza Kamanda Barlow ni kuwadharau wauaji hao baada ya kuona wamevalia vikoti vyenye rangi ya kijani vilivyokuwa na maandishi ya Polisi Jamii, alidhani kuwa na watu wa ulinzi shirikishi.

Baadhi ya maofisa wa polisi wameeleza kuamini kuwa watu hao walikuwa ni Polisi Jamii ndiko kulikomponza marehemu Barlow kwa kuwa aliamini kuwa alikuwa katika mikono salama, hali ambayo ilimfanya kutojiandaa kupambana nao.

Mwalimu Doroth
Mwalimu Doroth aliyekuwa na marehemu wakati wa tukio hilo, ambaye kwa sasa anashikiliwa kuhusiana na mauaji hayo ni mjane wa marehemu Modest Lyimo ambaye zamani alikuwa ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), aliyefariki mwaka 1997 wakati huo Kamanda Barlow akiwa na OCD wa Kituo cha Kati.

Lyimo alifariki na kumwacha Doroth akiwa na mtoto mmoja, lakini baadaye mwalimu huyo alizaa watoto wawili na mwanamume mwingine hivyo kuwa na watoto watatu (majina yanahifadhiwa kwa sasa).

Eneo la mauaji
Mwandishi wa gazeti hili alipofika nyumbani kwa Mwalimu Moses alikuta askari watatu wa jeshi la polisi wakilinda na kumkagua kila mtu aliyekuwa akiingia katika nyumba hiyo  na kutoka.

Mauaji yalivyotokea
Mmoja wa watoto wa mwalimu huyo, Kenrogers Edwin, ambaye alishuhudia tukio hilo la kuuawa kwa Kamanda Barlow, aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa siku hiyo usiku kabla ya tukio, alipigiwa simu na mama yake aliyemwarifu kuwa alikuwa amefika na kumtaka amfungulie mlango.
Edwin alisema kuwa anakumbuka pia katika maongezi ya simu mama yake alimweleza kwamba alikuwa akija na mgeni kwa ajili ya kutambua nyumbani anapoishi.

Alisema kuwa wakati akifungua geti ili gari alilokuwamo mama yake (Doroth), pamoja na mgeni wao (Kamanda Barlow) liingie ndani, aliona watu wakiwa wamezunguka gari hilo.

“Ilikuwa saa 8 usiku, nilipofungua geti ili aingie, niliona watu watatu wakiwa upande wa dereva wa gari na wawili upande mwingine aliokaa,” alisema na kuongeza:
“Niliona wakimnyang’anya mama mkoba na simu na nilisikia wakibishana, lakini baadaye nilisikia mlio wa risasi.”

Alieleza kwamba anakumbuka kuwa baada ya mlio huo wa risasi alilazimika kulala chini kwa kuogopa na kwamba baada ya Kamanda Barlow kupigwa risasi, wauaji hao walikimbia walipoona pikipiki ikija eneo hilo kwa kasi.

Aliyemhudumia  Baa
Mhudumu wa baa, Benard Kanyabukala, ambaye alimhudumia Kamanda Barlow katika kikao hicho alisema kuwa baada ya kikao hicho kumalizika, kamanda huyo aliagiza sanduku moja la bia kwa ajili ya wajumbe waliokuwapo katika kikao hicho na yeye (mhudumu) alinunuliwa kinywaji aina ya Alivaro.

“Aliomba bili na nilipompa alinifokea akidai nimemzidishia bei. Awali nilimweleza kuwa bei ya kreti ni Sh36,000, lakini kutokana na baadhi ya watu kutokunywa bia na kubadilisha vinywaji bei ilizidi na kuwa Sh40,700, ingawa baada ya kumwelewesha alilipa na kuongeza bia nyingine kwa raundi ya mwisho zenye thamani ya Sh 30,800,” alisema Kanyabukala.

Alieleza kwamba, wakati wa kikao hicho Kamanda Barlow alikuwa akinywa bia aina ya Serengeti, lakini mara ya mwisho alipoagiza vinywaji alikunywa maji ya Kilimanjaro na waliondoka hapo saa 8:30 usiku akiwa na mwanamke mmoja.

Mmiliki wa baa
Mmiliki wa baa ya Florida, kilipofanyika kikao hicho, Ritha Mosha alielezea kuwa, Kamanda Barlow alifika katika baa hiyo kwa mwaliko wa Semburi Moleto, ambaye yeye na Kamanda Barlow wote ni Wachaga waliozaliwa Kijiji cha Kiyou, Tarafa ya Vunjo Marangu, mkoani Kilimanjaro.

“Mimi ilikuwa ni mara yangu ya pili kuonana naye siku hiyo.  Kijana anayetarajia kuoa alinieleza kuwa, alimwomba Kamanda Barlow amsimamie kama mzazi wake katika arusi yake na ndiye aliyesimamia kikao hicho,  ndiyo aliyeongoza sala ya kufungua kikao hicho,” alieleza Ritha.

Alisema kuwa kikao hicho kilichelewa kuanza kutokana na wajumbe kuchelewa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini hapo.

Alifahamisha kuwa kikao hicho kilianza saa 2:21 usiku na kwamba kamanda huyo alikuwa msemaji wa familia.

Idadi ya wanawake
Ritha alifahamisha kuwa, kikao hicho kilitarajiwa kuwa na  wajumbe 100, lakini walifika kati ya 55 hadi 60 na kati ya hao kulikuwa na wanawake wawili ambao  aliwataja kwa majina ya Christina Mosha, mkazi wa Nyakato na Doroth ambaye alisindikizwa na kamanda huyo.
Chanzo: Mwananchi

Serikali yafikishwa mahakama ya The Hague

Best Blogger Tips
 KITUO  cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeipeleka Serikali ya Tanzania katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), kutokana na matukio 24 ya mauaji yanayokiuka haki za binadamu yaliyotokea nchini kati ya Januari na Septemba mwaka huu.

Mbali na hilo, LHRC kimepeleka taarifa hizo kwa Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Kimataifa, anayeshughulika na masuala ya mauaji ya raia yanayofanywa na vyombo vya dola.

Hatua hiyo ya LHRC inatokana na ripoti tatu zilizotolewa  hivi karibuni kuchunguza kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi kilichotokea katika Kijiji cha Nyololo, Mkoa wa Iringa, Septemba 2 mwaka huu.

Ripoti hizo ni ile ya Kamati ya Kuchunguza Mauaji hayo iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi iliyokuwa chini ya Jaji Steven Ihema; Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyokuwa chini ya Jaji Kiongozi Mstaafu, Amir Manento na ile ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tef), iliyoongozwa na John Mirenyi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Helen Kijo-Bisimba alisema kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, jumla ya watu 24 wameuawa na watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama.

“Tumepeleka mashtaka 24 ICC tangu Septemba 28 mwaka huu, ambayo yanahitajika kufanyiwa uchunguzi na kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali ya Tanzania ambayo imekuwa ikiwalinda viongozi wake wanaokiuka haki za binadamu,” alisema Dk Bisimba.

Alisema taarifa hizo pia wamezipeleka kwenye Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu katika kikao kinachoendelea huko Ivory Coast, lengo likiwa ni kuchunguza na kuchukua hatua katika Mahakama ya Afrika.

“Tunatarajia kuona uwajibikaji wa viongozi wote wa Serikali na vyombo vya dola waliohusika kwa njia yoyote ile. Hatua hizo au uwajibikaji huo ni pamoja na kujiuzulu, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani, ” alisema.

Aliitaka Serikali kuacha propaganda zinazotaka kuchochea vurugu katika taifa huku akisema inapaswa itambue kuwa hivi sasa nchi iko katika zama za vyama vingi vya siasa na kuacha kutumia vyombo vya dola kuleta chuki na mafarakano.

Dk Bisimba alisema baada ya kupitia taarifa zote tatu, LHRC kimesikitishwa na taarifa ya Kamati ya Dk Nchimbi... “LHRC hakijashangazwa sana pale taarifa hiyo ilipoonyesha wazi nia ya kuwalinda watuhumiwa kwa kuwa Serikali yetu bado haijajenga mfumo wa kujichunguza na kujiwajibisha yenyewe.”

“Serikali imeudhihirishia umma kuwa haikuwa na nia ya dhati ya kuchunguza suala la mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi, bali ilikuwa na lengo la kulisafisha Jeshi la Polisi na kuwalinda maofisa wake.”

Dk Bisimba alisema tangu mwaka 2001 hadi sasa, kituo hicho kimekuwa kikifuatilia kwa karibu matukio mbalimbali ya mauaji yanayoendelea kufanywa na vyombo vya dola na hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika.

Werema ashangaa, mawakili watofautiana
Akizungumzia suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema alisema hana taarifa za Serikali kushtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya The Hague.

“Kwa nini wameamua kutushtaki katika Mahakama ya The Hague? Kwani hapa nchini hakuna mahakama au wameona ni bora wavuke mipaka... Kwa sasa siwezi kulizungumzia zaidi suala hilo.”

Wakili wa Kujitegemea, Gaudioz Ishengoma alipotakiwa kuzungumzia hilo alisema anaunga mkono uamuzi wa kituo hicho kuipeleka Serikali kwenye Mahakama ya Kimataifa.

Alisema hilo ndilo eneo sahihi ambalo Serikali inatakiwa kupelekwa kwa sababu ya ukiukaji wa haki za binadamu na kwamba huko ndiko ambako haki inaweza kupatikana.

Hata hivyo, Wakili mwingine wa Kujitegemea, Majura Magafu alipinga hatua hiyo akisema kituo hicho kimekosea kuipeleka Serikali The Hague kwa kuwa imekuwa ikichukua hatua za kisheria dhidi ya makosa mbalimbali ya mauaji ambayo yamekuwa yakitokea.

“Kwa mawazo yangu, hawa LHRC wamekosea nadhani wamefanya hivyo kwa masilahi yao binafsi hasa ili kuonyesha kwamba wanafanya kazi,” alisema.

Alisema hata kama Serikali itakuwa imeshindwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wauaji, kituo hicho kilitakiwa kuishtaki Serikali katika mahakama za hapa nchini.

“Hawa sijui wanataka kutupeleka wapi kwa sababu wananchi wengi wa Afrika wakiwemo wa Kenya wamekuwa wakitaka mashtaka yasipelekwe nje ya nchi, hivi kila kitu tunawategemea Wazungu kwa sababu gani hasa?”

Utaratibu wa mashtaka
Kwa mujibu wa Mahakama hiyo, nchi mwanachama au Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndiyo wanaoweza kuelezea hali ya uhalifu ndani ya mipaka ya Mahakama hiyo na maelezo hayo hupelekwa kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC.
 
Mwendesha mashtaka mkuu atayapitia na kuanza uchunguzi isipokuwa pale tu atakapoona kuwa hakuna haja ya uchunguzi kwa maana ya kuwa kuna ushahidi wa kutosha juu ya uhalifu husika.

Uchunguzi wa mwendesha mashtaka utahusisha taarifa zote na ushahidi unaotakiwa kutathmini uhalifu unaotajwa huku ukizingatia haki zote za anayetuhumiwa.

Katika kipindi chote cha uchunguzi, mwendesha mashtaka atakuwa akitoa taarifa anazopata kwa Baraza la Awali la Mahakama (Pre-Trial Chamber) ambalo litakuwa na wajibu kwa maelekezo ya mwendesha mashtaka mkuu kutoa hati ya kukamatwa kwa wahusika au hati ya kuitwa mahakamani hapo. Mtuhumiwa anapofika mahakamani hapo, husomewa mashtaka yake ambayo yatakuwa msingi wa kesi nzima.

Baada ya kuthibitishwa kwa mashtaka, kesi hiyo itasikilizwa na Baraza la Awali la Mahakama chini ya majaji watatu na kutoa uamuzi wake wa ama kuwaachia au kuwatia hatiani watuhumiwa.

Tayari ICC imeshawapandisha kizimbani wanasiasa maarufu wa Kenya kutokana na kutuhumiwa kuhusika kuchochea vurugu za uchaguzi nchini Kenya mwaka 2008 ambazo zilisababisha vifo vya watu 1,133.

Wanasiasa hao ni Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, Mbunge wa Eldoret Kaskazini, William Ruto, aliyekuwa Mkuu wa utumishi, Francis Muthaura na Mtangazaji wa Redio ya Kass FM, Joshua Sang.
Chanzo:Mwananchi

Thursday, October 11, 2012

Lowassa hashikiki

Best Blogger Tips
 WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amezidi kuwatimulia vumbi wapinzani wake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutokana na wajumbe wanaounga mkono kambi yake kuzidi kupeta katika uchaguzi.

Katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha uliomalizika jana, kambi mbili zinazowaunga mkono Lowassa na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe katika mbio za urais 2015, zilionekana kutifuana vikali.

Msuguano huo ulianza kujitokeza tangu juzi kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa huo, ambapo juhudi za Katibu wa Mkoa, Mary Chatanda kutaka kuihujumu kambi ya Lowassa, ziligonga mwamba na kunusurika kipigo.

Chatanda ambaye alikuwa akifanya juhudi za kuhakikisha mshindi anakuwa Dk. Harold Adamson, aliambulia patupu baada ya Robinson Meitinyiku anayedaiwa kuungwa mkono na Lowassa, kushinda kwa kura 247 dhidi ya 188 za mpinzani wake.

Katika mwendelezo huo huo wa msuguano wa kambi hizo mbil, jana Katibu huyo CCM Mkoa wa Arusha, Chatanda, alijikuta akiaibishwa na wajumbe wa mkutano Mkuu wa chama baada ya kujifanya amesahau kumtambulisha Lowassa.

Chatanda aliufanya ukumbi mzima kupiga kelele kubwa wakisema bado! bado! Bado Eddo! Eddo! Eddo! Na ndipo kwa aibu kubwa, katibu huyo akameza mate na kumtambulisha Lowassa.

Hata hivyo, hatua hiyo ilitafsiriwa tofauti na baadhi ya wajumbe ambapo wengine walisema ni tukio la bahati mbaya, lakini wengi wao wakidai kuwa Chatanda alifanya makusudi kutokana na kundi analoliunga mkono kuanguka kwenye uchaguzi wa UVCCM.

Katika mkutano huo mkuu wa mkoa uliohudhuriwa na wajumbe 833, nafasi ya Mwenyekiti ilirudi tena kwa Onesmo ole Nangole ambaye anadaiwa kuunga mkono na Lowassa, akiwaacha kwa mbali washindani wake wawili.

Nangole alijizolea kura 604 huku akifuatiwa kwa mbali na Adam Choro wakati Dk. Salash Toure aliyedondoshwa na Lowassa kwenye uchaguzi wa ujumbe wa NEC Taifa kupitia wilayani Monduli akiambulia kura 13.

Akitangaza matokeo hayo, msaimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, alisema kura zilizopigwa ni 833 ambapo kura halali zilikuwa 830 na tatu ziliharibika.
Mapema akifungua mkutano huo kabla ya uchaguzi, Prof. Maghembe, aliwataka wajumbe kuacha kuzomea au kushangilia wagombea pindi watakapofika mbele yao kujinadi.

Alisema lengo la uchaguzi huo ni kupata viongozi watakaojenga chama kwa kuhakikisha wanavunja makundi na kuwaunganisha wanachama wote ili kuvirejesha viti vya udiwani na ubunge walivyovipoteza mkoani humo.

“Msichague viongozi watakaobweteka na kutugawa, hawa hawatufai, tuepuke viongozi wa aina hii, tuchague watakaokisaidia chama,” alisema Maghembe.

Naye Lowassa, akizungumza baada ya kuchaguliwa na wajumbe kuwa mwenyekiti wa muda wa mkutano huo, aliwashukuru wote kwa imani waliyompa huku akishangiliwa kwa kishindo.

“Wajumbe nimewaelewa na sitawaangusha, nimewaelewa ndugu zangu sitawaangusha, nawashukuru kwa kunishangilia, ila sasa tusishangilie tusije kuharibu utaratibu,” alisema Lowassa.

Akijinadi kwa wajumbe hao, Nangole aliwaomba wamchague ili aweze kusimamia dosari zilizopo na kushughulika na watu wote wanaoleta makundi ndani ya chama kwa mgawanyiko kuanzia wilayani mpaka Mkoa.

Naye Dk. Toure, aliwaomba wajumbe hao kuwa akichaguliwa, atamaliza makundi yaliyopo ambayo yamekiathiri chama hicho kwani wanachama wamegawanyika kila ngazi na kuwasihi wawabwage wagombea waliotumia fedha kuomba kura kwenye uchaguzi huo.

Mgawanyiko ndani ya chama ulionekana kuzungumzwa na kila mtu kwani hata Chora, naye aliwaomba wajumbe wamchague ili tatizo hilo alilodai kuwa limewapotezea majimbo.
Chanzo: Tanzania Daima

Wednesday, October 10, 2012

Ripoti ya Mwangosi yazua mazito

Best Blogger Tips
KAMATI  iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi kuchunguza kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten, Daud Mwangosi imeweka hadharani ripoti yake inayoeleza madudu yaliyofanywa na pande zote; polisi na Chadema na kusababisha mauaji hayo.

Wakati hayo yakibainika katika ripoti ya Kamati ya Waziri Nchimbi, Baraza la Habari Tanzania (MCT) nalo limeanika ripoti yake kuhusu kifo hicho. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mauaji hayo, yalitokana na uhasama uliopo baina ya polisi mkoani Iringa na waandishi wa habari wa mkoa huo.

Kamati hizo ziliundwa kwa nyakati tofauti kutokana na vurugu zilizotokea Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakifungua tawi la chama hicho katika kijiji hicho.

Wajumbe katika kamati ya Nchimbi ni Mwenyekiti Jaji Steven Ihema, Makamu Mwenyekiti, Theophil Makunga na Ofisa wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike.

Wengine ni Ofisa aliyesomea masuala ya milipuko kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Wema W. Wapo pamoja na Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi, Isaya Ngulu.

Kamati ya MCT ilikuwa ikiongozwa na John Mirenyi kutoka MCT, Hawra Shamte kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, Simon Berege.

Ripoti ya Nchimbi

Pamoja na mambo mengine ripoti hiyo imesema nguvu iliyotumika na polisi kuwatawanya wafuasi wa Chadema siku ya tukio, ni kubwa na bomu lililomuua Mwangosi, lilipigwa kutoka umbali mdogo badala ya mita 80 zinazotakiwa kitaalamu, tena bila kumwelekezea mtu.

Imesema utaratibu wa matumizi ya bomu hilo unaelekeza kulenga juu usawa wa nyuzi 45 na umbali wa mita 80 mpaka mita 100.

"Hakukuwa na umuhimu wa kutumia bomu hilo kwa sababu hata ingekuwa kwa sababu ya kuwakamata watu, tayari askari polisi wapatao sita walikuwapo eneo la tukio walitosha kwani operesheni haikuwa kubwa," imesema ripoti hiyo iliyokuwa ikisomwa na Jaji Ihema.

Jaji Ihema alisema kamati imependekeza nafasi za wakuu wa wilaya na mikoa ziangaliwe upya kwa kuwa zinatumika kisiasa.

Hata hiyo, Jaji Ihema alisema kinachozungumzwa kuhusu ripoti hiyo ni muhtasari tu wa ripoti nzima na wamefanya hivyo kuepuka kugusa mambo mengine ambayo yataingilia mwenendo wa kesi iliyopo mahakamani.

Hata hivyo, akaeleza kuwa ripoti nzima inayoelezea kitu kilichotokea anaijua Dk Nchimbi ambaye ndiye aliyeunda kamati hiyo.

Jaji Ihema alieleza kuwa kamati yake ilipewa hadidu sita za rejea ambazo ni kuangalia kama mkusanyiko wa Chadema ulikuwa halali na kama kulikuwa hakuna uvunjifu wa amani.

“Pia kuangalia kama nguvu iliyotumiwa na polisi ilikuwa sawa, mazingira yaliyosababisha polisi kutumia nguvu na kusababisha mauaji ya Mwangosi, kama kuna uhasama kati ya polisi na waandishi Iringa,” alisema Jaji Ihema na kuongeza;

“Kuangalia kanuni na taratibu za polisi kuzuia mikutano ya siasa na uhusiano wa Jeshi la Polisi na vyama vya siasa.”

Chadema nao walikuwa tatizo

Jaji Ihema alisema Chadema ndiyo chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani kijijini Nyololo hasa kutokana na uamuzi wa kung’ang’ania kukusanyika isivyo halali eneo hilo.

"Ikizingatiwa kuwepo kwa ujumbe wa SMS kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dk Willibrod Slaa uliosema, “IGP nasubiri simu yako. Wajulishe Polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha. Mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya Hague. Ni afadhali tufe kuliko manyanyaso haya,” alisema Jaji Ihema na kuendelea.

“Ujumbe huu ukiashiria umwagaji wa damu ni ushaidi tosha kuwepo kwa uvunjifu wa amani.”

Polisi tatizo

Alisema kuhusu nguvu iliyotumika na polisi, kamati imebaini kuwa ilikuwa ni kubwa kutokana na maelezo ya viongozi wa kijijini hapo.

“Mwangosi aliuawa wakati amri ya askari kuondoka kwenye eneo la tukio ilishatolewa,” alisema Jaji Ihema na kuongeza;.

"Kamati imebaini kuwa ushirikiano wa polisi na waandishi wa habari mkoani Iringa si mzuri hivyo ikapendekeza uangaliwe." Pia uhusiano kati ya polisi na baadhi ya vyama vya siasa hauridhishi, hivyo ni muhimu kukawa na jukwaa la kushughilikia hali hiyo, alisema Jaji Ihema.

Mapendekezo

Alisema kamati imeshauri kuwa sheria zinazotoa mamlaka za kuchunguza matukio ya vifo kwenye mkusanyiko ziangaliwe kwa kuwa lililotokea Nyololo lina ushahidi wa kutosha.

Jaji Ihema alisema kwa kuwa Jeshi la Polisi litabaki kuwa mlinzi wa wananchi, siasa za ubabe na uhasama ziachwe.

Aliendelea kusema kuwa kamati inapendekeza utulivu uendelee kuwepo ili kuweza kuondoa purukushani na pia viongozi waelimishwe juu ya  umuhimu wa kutii sheria.

“Kuwepo na programu mahususi ya uzalendo na kukuza maadili, elimu ya uraia iimarishwe  na mafunzo ya JKT yarudishwe mapema,” alisema.

Mapendekezo mengine ni kuboresha ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa kuanzisha ofisi wilayani na mikoani kwa kuwa imelemewa

“Kwa upande wa vyama vya siasa viongozi wajifunze kuwa wavumilivu na kutii sheria,” alisema Jaji Ihema.

Polisi ambao walihusika katika kumpiga marehemu Daud Mwangosi kabla.

Ripoti ya MCT

Ripoti ya Timu Maalumu iliyoundwa na MCT na TEF, kuchunguza tukio hilo imesema mauaji hayo yalifanywa makusudi chini ya usimamizi wa Kamanda wa Polisi wa Iringa, Michael Kamuhanda.

“Matokeo ya uchunguzi ya mazingira yaliyopelekea mauaji ya Daudi Mwangosi, awali ya yote umethibitisha polisi kwa makusudi kabisa waliwashughulikia waandishi wa habari wa Iringa wakati wakikusanya habari za shughuli za Chadema katika Kijiji cha Nyololo,” inasema na kuongeza:

“Pia  Daudi Mwangosi aliuawa mikononi mwa polisi chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa RPC Michael Kamuhanda. Matokeo haya yanathibitishwa na maelezo pamoja na ushahidi uliokusanywa kwa kutumia picha za video na ushahidi mwingine muhimu wa taarifa za vyombo vya habari.”

Katibu wa MCT, Kajubi Mukajanga aliyesoma ripoti hiyo alisema kuwa utafiti huo ulibaini kuwa taarifa za mauaji wa Mwangosi zimekuwa zikikinzana kuanzia hatua za awali jitihada za kuficha ukweli zilipojidhihirisha.

Ikifafanua juu ya uhusiano mbaya kati ya viongozi wa Serikali ya  Mkoa huo na Jeshi la Polisi dhidi ya waandishi, ilisema  baadhi ya waandishi waliwahi kupigwa na kuharibiwa vyombo vyao vya kazi.

“Novemba 2011, mwandishi Laurent Mkumbata anayefanya kazi ITV, alipigwa vibaya na kamera yake ilivunjwa kwa makusudi na aliyekuwa Mkuu wa Polisi (OCD) wa Iringa Mohamed Semunyu wakati akiwa kazini,” ilisema:

“Waandishi wa habari wa Iringa pia, walitendewa vibaya na viongozi wa mkoa wakati wa ziara ya Makamu wa Rais mwishoni mwa Februari 2011. Waandishi katika ziara hiyo walilazimika kulala kwenye basi walilosafiria kutokana na viongozi kupuuza kuwapatia hoteli ya kulala.”

Kwa mujibu wa Mukajanga, Machi sita mwaka huu, polisi mkoani Iringa waliwapa Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (IPC), kibali cha kufanya maandamano ya amani kulalamikia kukua kwa uhusiano usio mzuri kati ya waandishi wa habari na viongozi wa mkoa.

Mukajanga alisema tukio hilo waliwalenga zaidi waandishi wa Iringa ambao walikuwa wanawafahamu zaidi na kuwaacha wale waliotoka  Dar es Salaam.

Kabla ya kusomwa kwa ripoti hiyo, Mukajanga alitahadharisha juu ya tabia aliyosema imeibuka ya watu kufungwa midomo kwa kisingizio cha kuwa kesi ipo mahakamani.

Alisema kwamba, ana imani kuwa mahakimu na majaji nchini, ni watu wenye sifa ambao wanaweza kufanya shughuli zao kwa kuzingatia ushahidi unaotolewa mahakamani bila ya kuathiriwa na maneno ya mitaani. 
Chanzo: Mwananchi

Tuesday, October 9, 2012

Mzee Mwinyi aibiwa sh milioni 37/-

Best Blogger Tips
 RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi, ameibiwa sh milioni 37.4 na hivyo kulazimika kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutoa ushahidi wake.

Kwa hatua hiyo, Mzee Mwinyi anafuata nyayo za Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliyepanda kizimbani hivi karibuni kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin.

Mzee Mwinyi ambaye alipanda kizimbani jana, anadai kuibiwa sh 37,440,000 na Abdallah Nassoro Mzombe (39) ambaye ni wakala wake.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Genivitus Dudu, mshtakiwa huyo, mkazi wa Kinondoni Mkwajuni, anashtakiwa kwa makosa ya kumuibia Mzee Mwinyi kiasi hicho cha kodi ya pango ya nyumba mbili zinazomilikiwa na Rais huyo mstaafu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ambayo Tanzania Daima Jumatano ina nakala yake, Mzombe anadaiwa kufanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 258 na 273 (b) (e) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Sura ya 16 ya mwaka 2002.

Siku hiyo ya Agosti 21, mwaka huu, ilidaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, mwaka 2011 na Julai 2012 huko Mikocheni, Mzombe akiwa wakala wa Rais huyo mstaafu, alimwibia sh 17,640,000 ambazo ni pato la kodi ya nyumba yake iliyoko eneo la Mikocheni, wilaya ya Kinondoni.

Iliendelea kudai kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho Mzombe alimwibia Rais Mwinyi kilikuwa ni kodi ya pango la nyumba namba 481, iliyoko kwenye ploti A huko Mikocheni ya mwaka 2011/2012 na 2012/2013.

Aidha anadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, mwaka 2011 na Julai 10, mwaka huu huko Msasani Village wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa huyo alimwibia tena Rais huyo mstaafu sh 19,800,000 ambazo zilikuwa ni kodi ya nyumba namba 55 iliyoko kwenye Kitalu C .

Kiasi hicho cha fedha kilikuwa ni kodi ya pango la nyumba hiyo la mwaka 2011/2012 na 2012/2013.
Hata hivyo mshtakiwa huyo alikana mashtaka yote na yuko rumande hadi Oktoba 22 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Rais Mwinyi jana alitua katika mahakama hiyo huku akiongozwa na maofisa Usalama wa Taifa (TISS) kuja kutoa ushahidi katika kesi hiyo ya jinai Na. 201/2012 iliyofunguliwa na serikali dhidi ya wakala wa Mwinyi, Abdallah Nassoro Mzombe (39).

Kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa, Mwinyi alihifadhiwa kwa muda kwenye chumba namba moja cha mahakama hiyo ili kutoa muda kwa wakili wa serikali, Charles Anindo, kumuandaa.

Waandishi wa habari waliokuwepo mahakamani hapo kwa ajili ya kuripoti kesi hiyo, walizuiliwa kuingia, jambo ambalo lililalamikiwa vikali na wana habari hao.

“Msiingie humu ndani haiwahusu,” alisema ofisa habari mmoja, akiwazuia waandishi kuingia ndani ya mahakama hiyo.
Mzee Mwinyi aliondoka katika viwanja vya mahakama hiyo majira ya saa 6:21 mchana na kisha kupanda gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 914 BJT.

Hati ya mashtaka ya kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo Agosti 21 mwaka huu.

Mei 7 mwaka huu Rais Mkapa alifika mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Elvin Mugeta, kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, na Grace Martin. Mahalu aliachiwa huru katika kesi hiyo.
Chanzo: Tanzania Daima

Sunday, October 7, 2012

Sumaye: Lowassa hawezi kunizuia kugombea urais

Best Blogger Tips
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema endapo ataamua kugombea urais, hata kama jina la Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa litakuwepo haitamsumbua kwa kuwa hatafanya hivyo kwa ajili ya mtu yeyote, bali Watanzania.

Vilevile, amesema kuanguka kwake katika nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kupitia Wilaya ya Hanang', kumempa nguvu zaidi na kwamba hakujamdhoofisha kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Sumaye aliangushwa katika nafasi hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Sumaye pia alikana kukutana na viongozi wa Chadema kujadili hatima yake ya kisiasa baada ya uchaguzi huo... “Kama ningekuwa nimekutana na viongozi wa chama hicho ningesema kwa kuwa hata wengine wanaoutafuta urais kwa udi na uvumba huwa wanakutana nao,” alisema Sumaye bila kufafanua.

Hivi karibuni, mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya Chadema, alikaririwa akidai kwamba Sumaye alikutana na viongozi wa chama hicho mara baada ya kuangushwa na Nagu.

Jana, Sumaye alisema kwamba atabaki kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na kwamba hayuko katika chama hicho kwa ajili ya cheo.

Hata hivyo alitoa angalizo kuhusu upinzani akisema: “Nadhani tufikie kwenye ustaarabu kuwa vyama vya upinzani siyo maadui wala viongozi wao siyo maadui wa viongozi wa CCM.”
Alisema kukosa kwake nafasi ya Nec hakumnyimi usingizi na wala hajawahi kufikiria kukihama chama hicho kwa sababu hiyo.

“Hakuninyimi usingizi na hakusababishi au kunizuia kugombea urais kama nikiamua. Sijatangaza kugombea urais, nikiamua kugombea nitapita humohumo CCM kwa kuwa kuangushwa Hanang’ hakujanisumbua kabisa.”

Alisema hana uhasama na Lowassa na kwamba hajawahi kusema kwamba atapambana naye wala kumtangazia vita. Alisisitiza kwamba endapo atachukua uamuzi wa kugombea nafasi hiyo kuu ya uongozi nchini, haitakuwa kwa ajili ya mtu yeyote, bali Watanzania.

“Kama nikiamua kugombea, hata kuwe na wagombea 20 au agombee Lowassa, nikiamua kugombea nitagombea,” alisema Sumaye.

Uchaguzi ulijaa rushwa
Akizungumzia uchaguzi huo wa ndani wa CCM, Sumaye alisema yaliyotokea Hanang’ yametokea maeneo mengi nchini na kwamba uchaguzi unaoendelea umegubikwa na rushwa.

Hata hivyo, alisema hatakata rufaa wala kupeleka malalamiko popote kwa kuwa yaliyokuwa yakitendeka yanafahamika.

Alisema uchaguzi huo licha ya kutawaliwa na rushwa ulijaa vitendo vingi viovu vikiwemo, vitisho na uharamia wa kuhamisha wapiga kura usiku.

Alisema pia kulikuwepo rushwa ya kimtandao na kwamba hajui fedha zilizokuwa zikitolewa kama rushwa kwa wajumbe ni nani aliyekuwa akizitoa.

“Uchaguzi ulikuwa kivumbi kwelikweli, hivi sasa hapa nchini inaonekana ni vigumu kushinda uchaguzi bila kutoa rushwa.”

Alisema watu wanatoa rushwa ya kimtandao kuhakikisha wapambe wao wanachaguliwa katika nafasi mbalimbali nchini ili kujiwekea wawakilishi kwa ajili ya faida yao ya baadaye.
“Viongozi wa aina hii hufanya kazi kwa manufaa ya wale waliowapa fedha na si kwa manufaa ya wananchi,” alisema Sumaye.

Alisema hazungumzii rushwa kwa kuwa ameshindwa nafasi ya Nec Hanang’, bali hayo ni mapambano yake ya muda mrefu katika kuhakikisha rushwa inatokomea.
Alisema tatizo la rushwa si la ndani ya CCM pekee, bali ni la nchi nzima akisema viongozi wanatoa rushwa ili wapate nafasi kitu ambacho si sawa.

“Kiongozi mtoa rushwa ni mali ya watu fulani na hawezi kutenda haki akiwa madarakani, kazi yake itakuwa ni kutafuta fedha kwa ajili ya kuwahonga tena wapiga kura ili arudi madarakani,” alisema Sumaye na kuongeza:
“Rushwa ni adui wa haki na ni tatizo kubwa nchini kwetu hivyo lazima tulikatae tatizo hilo.”
Huku akitanabahisha kwamba anayoyasema siyo mazuri kwa baadhi ya watu, Sumaye alisema ni muhimu amani ya nchi ikalindwa isichafuke kutokana na uroho wa madaraka.

Sumaye alisema ana imani na CCM, lakini kilichopo ni kwamba bado chama hicho hakijasimama vya kutosha kukabiliana na tatizo la rushwa.

“CCM kama chama hakina tatizo, bali kuna maeneo kadhaa ya kurekebisha ili kiweze kubadilika kwa kuwa kina uwezo huo,” alisema Sumaye.
Alisema endapo mtu ataona kuna tatizo katika chama jibu lake ni kujitoa, hiyo itakuwa ni tatizo la mtu kwa kuwa anakohamia anaweza kukuta nako kuna tatizo ikawa tatizo ni kuhama hama.

“Nitapigana na rushwa labda ifike sehemu nichoke niamue kutoka na kuwa mwananchi wa kawaida au kwenda sehemu nyingine kwani mapambano dhidi ya rushwa ni ya kudumu kwangu na nitaendelea nayo popote nitakapokuwepo,” alisema na kuongeza: “Kama mtu ana mambo mabaya katika chama ni lazima aadhibiwe na aadabishwe na ndiyo maana mwenyekiti wetu aliposema watu wajivue gamba nilifurahi. Ni bora CCM tukajirekebisha kabla watu hawajasema sasa basi.”
Chanzo: Mwananchi

Wednesday, September 26, 2012

Vita CCM

Best Blogger Tips
HALMASHAURI Kuu ya CCM (Nec), imetangaza majina ya wagombea walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho, huku ikionyesha kuwa uchaguzi huo utakuwa na mchuano mkali.

Katika orodha iliyotolewa jana, baadhi ya makada wake maarufu akiwamo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Salum Londa wametupwa.

Mchuano mkali unaonekana kuwapo kwenye nafasi ya ujumbe wa Nec Mkoa wa Manyara ambako Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye anachuana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu.

Mchuano huo unatarajiwa kuwa mkali katika nafasi ya uenyekiti kwenye baadhi ya mikoa kutokana na kupitishwa kwa majina ya makada wake maarufu. Mwanza ni miongoni mwa mikoa hiyo kwani Nec imepitisha jina la Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo ambaye atachuana na Clement Mabina anayetetea nafasi hiyo.

Makada hao watapata ushindani mkali kutoka kwa Zebedayo Athumani, Joseph Yaredi na Mashimba Hussein Mashimba.

Dar es Salaam nako kunatarajiwa kuwa na mchuano mkali kwani mwenyekiti wa sasa, John Guninita atachuana na Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi Makao Makuu ya CCM, Matson Chizzi na kada mwingine, Ramadhan Madabida. Godfrey Mwalusamba, Harold Adamson na Paul Laizer wanawania nafasi hiyo mkoani Arusha.

Vita nyingine kali ipo kwenye Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania (UWT), ambako Mwenyekiti wa sasa, Sofia Simba ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto anachuana na Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela na Mbunge wa Viti Maalumu, Mayrose Majige.

Katika Jumuiya ya Wazazi, Mkono ambaye alikuwa akiwania nafasi hiyo ametupwa na kuwaacha Abdallah Bulembo, Martha Mlata na kada wa siku nyingi, John Barongo kuchuana.

Awali, Mkono alikatwa jina lake na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo na kutangaza hali ya hatari akisema asipopitishwa patachimbika. Jina lake lilirejeshwa na Kamati ya Usalama na Maadili kabla ya kukatwa tena na Kamati Kuu.

Alipoulizwa jana kuhusu kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho, Mkono alisema: “Nimekubaliana na uamuzi wa chama na nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM. Nimelelewa na kukulia CCM na nitaendelea kubaki CCM nikiwa mwanachama mtiifu.”

Katika Jumuiya ya Vijana (UVCCM), mchuano mkali unaonekana kuwa katika nafasi ya makamu mwenyekiti kwani mmoja wa wagombea waliopitishwa, Paul Makonda anaaminika kuwa na nguvu kubwa kutoka katika kundi la wabunge na mawaziri wapambanaji wa ufisadi. Makonda anawania nafasi hiyo pamoja na Mboni Mhita na Ally Hapi.

Nafasi ya Mwenyekiti UVCCM inawaniwa na Sadifa Juma Khamis, Rashid Simai Msaraka na Lulu Mshamu Abdallah.

Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa atachuana na Dk Salash Toure na Nanai Kanina kwenye nafasi ya ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Monduli.

Wagombea wa ‘kundi la kifo’
Vigogo kadhaa wamepitishwa kuwania nafasi 10 za Nec, wakiwamo baadhi ya mawaziri na viongozi wa juu wa chama hicho.

Miongoni mwao ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo David, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama.

Wengine ni Katibu wa Fedha na Uchumi CCM, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano, Stephen Wassira, Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Vijana, Dk Fenela Mukangara na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela.

Kwa upande wa Zanzibar, nafasi 10 za Nec kupitia kapu zinawaniwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan.

Katika orodha hiyo wamo, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, Waziri wa zamani wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Mohamed Seif Khatib, Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Omar Yussuf Mzee na Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Abdisalami Issa Khatib.

Familia ya Kikwete
Katika uteuzi huo wa wagombea, majina matatu ya wagombea kutoka katika familia ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete yamepitishwa.

Waliopitishwa ni pamoja na mkewe Salma Kikwete ambaye anakuwa mgombea pekee katika nafasi ya ujumbe wa Nec Lindi Mjini na Ridhiwan Kikwete ambaye pia ni mgombea pekee wa nafasi hiyo katika Wilaya ya Bagamoyo.

Mbali ya hao, Nec pia imepitisha jina la Mohamed Mrisho Kikwete kuwania nafasi ya uenyekiti wa Wilaya ya Bagamoyo.

Vigogo watemwa
Nec imewatema vigogo kadhaa, baadhi yao ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Azim Premji na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo-Swai ambaye alikuwa anagombea ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Hai na kada wa siku nyingi, Salum Londa.

Pia wamo wabunge, Sarah Msafiri, Munde Tambwe, Deo Filikunjombe na Victor Mwambalaswa.Wengine waliotemwa ni Hussein Bashe na hasimu wake mkubwa kisiasa Dk Hamis Kigwangalla, Jamali Kassim, Anthony Mavunde na Emmanuel Nzungu, ambaye aliomba kugombea Uenyekiti Wilaya ya Ilemela, Mwanza.

Mgeja chupuchupu
Mwenyekiti wa sasa wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja aliponea chupuchupu kutemwa baada ya Nec kurejesha jina lake kwenye orodha ya wagombea lililokuwa limeondolewa na vikao vya awali.Taarifa za kuondolewa jina la Mgeja zilivuja tangu juzi wakati kikao cha Kamati Kuu kilipoketi ikidaiwa ni kutokana na malumbano kati yake na Mbunge wa Kahama, James Lembeli.

Inadaiwa wakati wa kujadiliwa Mgeja, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alitoka kwenye kikao na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na kumwachia kiti Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa.

Baada ya mjadala mrefu wa kumtetea Mgeja kwamba hakutendewa haki, Msekwa alifikia uamuzi wa kurejesha jina.

“Baadhi ya waliomtetea ninaokumbuka ni Dk Makongoro Mahanga na Peter Serukamba, lakini wakati wa mjadala wa Mgeja, Mwenyekiti (Kikwete) na Nape walikwenda chemba, kiti akaachiwa Msekwa,” kilisema chanzo chetu.

Awali, kada mkongwe wa chama hicho, Kingunge Ngombale - Mwiru aliituhumu Kamati Kuu kwamba imevunja kanuni za uchaguzi kwa kuteua majina zaidi ya matatu kwenye nafasi moja.

Hata hivyo, inadaiwa Msekwa alimsomea kanuni moja baada ya nyingine zinazohusu uteuzi hali iliyoonyesha kama kumweka darasani na hatimaye ikabainika hakuna kanuni iliyovunjwa.Hoja hiyo ilitokana na baadhi ya mikoa kwenye nafasi moja kusimamisha wagombea zaidi ya watatu kama nafasi ya mwenyekiti mkoa wa Mwanza.

Hatua hiyo inadaiwa inalenga kuondoa matokeo ya kupanga kwa baadhi ya wagombea na kwamba, kwa hali hiyo mshindi hawezi kupatikana kwa mzunguko wa kwanza.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba anadaiwa kushambulia mtandao uliokuwa umejipanga na kuweka wagombea wao hata kama hawana sifa.“Yule mzee (Makamba) amewachana-chana vibaya, anasema hapa tunasajili timu, kama majina hayafai yaondolewe,” kilidokeza chanzo na kuongeza kwamba hoja hiyo iliungwa mkono na kada mkongwe wa chama hicho, Mzee Peter Kisumo.
Chanzo: Mwananchi

Kikwete: Anayetaka kuondoka CCM ‘ruksa’

Best Blogger Tips
 MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amewatolea uvivu wagombea wa nafasi mbalimbali ambao majina yao yamekatwa, akisema wanaotaka kukihama chama hicho kwa sababu wametoswa, waondoke haraka.

Licha ya kuwatakia safari njema, Rais Kikwete aliwatupia lawama baadhi ya wanaCCM ambao wameripotiwa kuendesha malumbano na kugeuza uchaguzi huo kama uwanja wa vita.

Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) jana, Rais Kikwete alisema kumekuwapo na taarifa mbalimbali ambazo zimemfikia pia kwamba baadhi ya wanachama wanatishia kukihama chama hicho kama majina yao yatakatwa.

“Wako wenye ndimi mbili ambao wanasema kuwa wasipoteuliwa wanaweza kuondoka. Ah! Mimi nasema watangulie huko maana inaonyesha kuwa walishaandaa maeneo ya kwenda,” alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wajumbe wa Nec.

Alisema CCM kinayo taarifa kuhusu watu kugombana na hata kutoleana silaha, jambo alilosema linashangaza, huku akihoji kuna nini katika uongozi tena Nec?

“Uchaguzi usigeuzwe uwanja wa fujo. Wengine wanatoleana silaha kama majembe, ngumi na silaha nyingine, hivi wanagombana nini huko? Uchaguzi usigeuzwe kuwa ni uwanja wa vita.” alisema.

Hivi karibuni, baadhi ya makada wa chama hicho wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za kukitishia chama hicho akiwemo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ambaye alikaririwa akisema kama jina lake halitapitishwa, patachimbika.

Mbunge huyo alisema hayo siku chache baada ya jina lake kutupwa na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi iliyokuwa ikipitia na kuteua wagombea watatu kwa ajili ya kuwania nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

"Hapatatosha CCM," alisema Mkono alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kutoswa kwake katika mchujo wa awamu hiyo ya awali.

Ingawa Rais Kikwete hakutaja majina, Mbunge wa Nzega Dk Khamis Kigwangallah na Hussein Bashe nao waliripotiwa kutoleana maneno makali hata kuonyeshana bastola, huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na Mbunge wa Kahama, James Lembeli wakiendesha malumbano kwa muda mrefu.

Inadaiwa kuwa majina hayo yote na ya vigogo wengine yamekatwa na jana baadhi yao walikuwa wanadai kuwa CCM kinataka kuzalisha upinzani ambao utakisababishia kushindwa katika safari yake kisiasa hasa katika mfumo huu wa vyama vingi.

Licha ya makaripio hayo, Rais Kikwete alibainisha kuwa CCM kinasemwa na watu kuwa kinakithiri rushwa katika chaguzi zake hivyo akawataka wagombea kubadilika kabla ya kukamatwa na Takukuru.

“Zipo taarifa ingawa hatujazithibitisha kwamba wapo baadhi ya wagombea wanamwaga fedha sijawahi kuona…

Takukuru wapo wanaendelea na kazi. Chama chetu kinasemwa tujipe fursa ya kubadilika, tusisubiri kukamatwa na kuanza kuilaumu PCCB.”

Kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali, Rais Kikwete alisema katika uchaguzi huo, wamejitokeza watu wengi tena vijana wasomi na kwamba Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati Kuu, zimewapandisha na kuwakata waliotumikia chama muda mrefu.

“Kama hukuteuliwa kuna mawili, ama nafasi zimejaa au hufai una upungufu kidogo na huo ni utaratibu wa chama siyo kuoneana,” alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa.

Alisema katika uteuzi huo vijana watapewa nafasi zaidi kutokana na ukweli kuwa, chama bila ya vijana hakiwezi kuwa imara kwa sababu ndiyo nguvu ya ushindi.

“Hao watakaoachwa watambue kuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kutengeneza timu ya ushindi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa Bara na Visiwani, hivyo kuachwa jina lako isiwe nongwa,” alisema na kuongeza:

“Lazima tukipe chama chetu watu wa kushinda… Lazima tutambue sasa tunaunda timu ya ushindi wa chama siyo ushindi wa mtu.”

Hata hivyo, Rais Kikwete alitoa angalizo kuwa anajua kikao cha Halmashauri Kuu kingekuwa na mjadala mzito, lakini lazima wakipe chama watu wa kushinda.

Majina manne
Kamati Kuu ya CCM, inadaiwa kupendekeza majina ya wagombea wanne kwenye jumuiya zake, tofauti na kanuni ya chama hicho ya nafasi moja kuwaniwa na watu watatu.

Kikao chake kilichomalizika juzi usiku, kinadaiwa kubadili kanuni ya kupendekeza wagombea watatu kwa nafasi moja na kwamba, hivi sasa mapendekezo hasa kwenye jumuiya ni wagombea wanne.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa, hatua hiyo inalenga kutoa ushindani kwa wagombea.

Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipotakiwa kuzungumzia suala hilo hakukanusha wala kukubali zaidi ya kusema kwamba hata kama utaratibu huo umetumika siyo mara ya kwanza kwa chama hicho.

Alisema kama Jumuiya ya Vijana wanaojitokeza lengo lao linakuwa kupata uzoefu na kwamba, idadi ya majina inategemeana na busara za kikao kinavyoona ili kutoa nafasi kwa wagombea kujipima.
Chanzo: Mwananchi

Tuesday, September 18, 2012

Madaktari waliogoma waiangukia serikali

Best Blogger Tips
MADAKTARI waliokuwa kwenye mafunzo kwa vitendo ambao Serikali iliwafutia vibali vya kazi, wamesalimu amri na kuamua kumuangukia aliyekuwa mwajiri wao ili awarudishe kazini.

Serikali iliwafukuza kazi madaktari hao baada ya kutangaza mgomo usio na kikomo Juni mwaka huu, hadi madai yao yatakapofanyiwa kazi ambapo mgomo huo ulisababisha vifo kwa baadhi ya wagonjwa waliokosa huduma za matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari walioathirika na mgomo, Bw. Paul Swakala, alisema wameamua kuomba msamaha kwa Rais Jakaya Kikwete na Watanzania wote baada ya kubaini kuwa, wagonjwa wengi waliathirika na mgomo huo.

Alisema walishindwa kuuepuka mgomo huo kutokana na mazingira ya wao kufanya kazi na Madaktari Bingwa kwani mikataba yao, haikuwaruhusu kufanya kazi ya kutoa matibabu peke yao.

“Tunafahamu kuwa, Watanzania wengi waliathirika mgomo ule, tunawaomba radhi sana kwa usumbufu walioupata na tunakiri kuwa kila mmoja wao alichokizwa na uamuzi wetu.

“Japo nchini kwetu utamaduni wa kuomba radhi hadharani haupo, sisi tumeamua kufanya hivi kwa sababu tumekosa na hakuna binadamu aliye kamili wote tunakasoro,” alisema Bw. Swakala.

Aliongeza kuwa, wanatambua na kuunga mkono juhudi za Rais Kikwete katika kuboresha huduma za afya nchini licha ta changamoto nyingi zinazoikabili sekta hiyo.

“Tunamuomba radhi sana Rais Kikwete na Serikali yake kwa usumbufu uliosababishwa na mgomo, pia tunatambua jitihada zake za kutafuta suluhu ya mgomo uliopo,” alisema.

Aliwahakikishia Watanzania kuwa, kuanzia sasa hawako tayari kushiriki mgomo kwa namna yoyote kwabni kufanya hivyo ni kuweka rehani maisha ya wagonjwa.

Bw. Swakala alisema wanajutia kosa hilo na wako tayari kulejea kazini ili kuwahudumia Watanzania kwa moyo mweupe na wanayo dhamira ya kounana na Rais Kikwete ana kwa ana ili kumuomba radhi.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Bw. Swakala alisema madaktari ambao wamesaini fomu za kuomba radhi ni 200 kati ya 364 waliofutiwa vibali vya kazi.

“Mimi nimesoma kwa gharama za sh. milioni 35, sioni faida ya kukaa mtaani wakati Watanzania wakiendelea kupata  shida ya matibabu,” alisema Bw. Swakala.

Akizungumzia suala la vifaa ambalo ni moja ya sababu iliyowafanya wagome, Bw. Swakala, wao wanaamini Rais Kikwete na Serikali yake itaboresha mazingira ya huduma za afya.

“Chama cha Madaktari nchini (MAT) ni cha hiari, hatuungani na msimamo wao, wanachama walionao ni madaktari wenye usajili wa kudumu si kama sisi, hatulazimishwi kujiunga nao,” alisema.

Madaktari hao walifanya mgomo huo ili kuishawishi Serikali iboreshe mazingira ya kazi, nyongeza ya mishahara na marupurupu mengine.
Source: Tanzania Daima

Sunday, September 16, 2012

UWT kwawaka moto

Best Blogger Tips
MAPENDEKEZO ya Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) wa CCM ya majina ya wagombea nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo ngazi ya taifa, yameibua mlolongo wa tuhuma kuwa yalifikiwa kwa upendeleo, rushwa na woga.

Tuhuma hizo zimetolewa na baadhi ya walioomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo, ambao majina yao hayakupendekezwa na kamati wanayodai kuwa ilifanya kazi kwa woga na kuwapendelea baadhi ya wagombea baada ya kushawishiwa kwa rushwa.

Mbali ya malalamiko ya wagombea, taarifa kutoka ndani ya UWT zinaeleza kuwa, uteuzi wa majina yaliyopendekezwa na kamati ya utekelezaji na kupelekwa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM umeibua ufa baina ya wanajumuiya hiyo kwa kile kinachoelezwa baadhi yao kujiona wanatengwa kwa sababu hawana watu wa kuwapigania dhidi ya wake wa vigogo wanaodaiwa kuogopwa na kutetewa na waume zao.

Mmoja wa wagombea ambaye jina lake halikupendekezwa, Hamida Thabit, katika mahojiano yake na gazeti hili kuhusu mwenendo wa mchakato wa uteuzi alisema ulikuwa wa hovyo kwa sababu haukuzingatia sifa na uwezo wa waombaji.

Alisema waombaji wenye sifa majina yao hayakupendekezwa kwa sababu hawakuwa na pesa za kuwafurahisha wajumbe, na majina ya waombaji ambao waume zao wana sauti ndani ya chama yalipitishwa kwa woga.

“Sijaridhika na mapendekezo ya kamati. Siyo kwamba nina uchu wa madaraka, lakini wakati mwingine ukiona mambo yanakwenda kombo kiasi cha kutisha ni lazima kusema. Na ninasema ili NEC ilione hili, itende haki kwa sababu UWT ni waoga.

“Baadhi yetu majina yetu hayakupendekezwa kwa sababu hatuna pesa, hatuna watu wa kututetea, hatuna wanaume wenye nyadhifa au sauti ndani ya chama. Ni aibu kwa jumuiya iliyokomaa kama UWT kuchagua watu kwa kuwaogopa, eti wasipochaguliwa watapiga kelele.

“Wabunge wenye majimbo, wana kazi za kila siku za kusimamia majimbo yao, bado wanataka na kazi ngumu ya kuongoza umoja huu na majina yao yanapitishwa, hiyo maana yake nini? Wanaachwa watu wenye sifa, wanaoijua UWT,” alisema Hamida.

Alisema mwenendo wa sasa wa CCM unaonekana kuwa wa kifamilia zaidi kwa sababu licha ya kuwa na wanachama wengi wenye sifa na uwezo wa kushika nafasi za uongozi, bado nafasi hizo zinatolewa kwa kujuana na hasa kwa kuangalia wake wa vigogo.

Alitolea mfano wa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, kuwa ni mbunge wa jimbo ambaye ana jukumu la kuwatumikia wapiga kura wake, hivyo hapaswi kukabidhiwa jukumu lingine la kuongoza UWT kwa sababu majukumu yote ni mazito.

Pia alisema Maryrose Majinge hakupaswa kupendekezwa kwa sababu hana sifa zinazostahili kuwa kiongozi wa juu wa umoja huo.

“Anne Kilango ni mbunge wa jimbo, anawajibika kwa karibu sana kwa wananchi wa jimbo lake, lakini bado anataka uenyekiti wa jumuiya. Majukumu yote ni mazito, kwanini yeye tu majukumu hayo?

“Sophia Simba ni sawa kwa sababu yeye ni mwenyekiti hivyo anatetea kiti chake na anao uzoefu wa uongozi ndani ya jumuiya, lakini hata huyu Maryrose, ametokea umoja wa vijana moja kwa moja amerushwa hadi kwenye uenyekiti, aanzie chini ajifunze na kupata uzoefu.

“Huu ni upendeleo wa wazi kabisa, unajua ukiwa na watoto watatu halafu ukawa unampendelea mmoja tu, wengine lazima watalalamika na itafika mahali watapachukia nyumbani, huko ndiko tunakokwenda.

“Kwa sababu lazima ieleweke kuwa kujua kupiga kelele siyo ujuzi wa kiutendaji, kupiga kelele bungeni siyo kigezo cha kuwa kiongozi bora,” alisema.

Alipoulizwa kama ana mpango wa kukata rufaa kupinga mapendekezo hayo, alisema hana mpango huo kwa sababu anaamini hakuna kitakachofanyika isipokuwa anabaki na matumaini NEC itatenda haki.

Mgombea mwingine aliyelalamikia mapendekezo ya kamati ya utekelezaji ya UWT ni Hilder Kitana, ambaye alisema ingawa anayaheshimu maamuzi ya kamati hiyo, amesikitishwa na kitendo chake cha woga.

Kitana alisema kamati hiyo imewaacha baadhi ya waombaji wenye sifa na kuchukua majina ya watu ambao hawana rekodi ya uongozi ndani ya jumuiya, lakini pia wenye majukumu ya kila siku kwa nafasi ambazo tayari wanazo.

“Wameamua wamependekeza majina hayo sawa, nayaheshimu. Lakini nimesikitishwa na woga wa kamati hii. Tukienda kwa kuogopana kama walivyokuwa wanasema ndani ya kamati hiyo hatutafika, tunaiua jumuiya.

“Mimi nimekuwa Mjumbe Kamati Kuu ya UWT, nimekuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, ninaijua jumuiya, sina jukumu kwa sasa linalonibana moja kwa moja zaidi ya biashara zangu, halafu jina langu linakatwa kwa sababu wanasema wakimuacha Kilango, anaongea sana na mke wa mtu mkubwa itakuwa matatizo, atapiga kelele hadi kwenye vyombo vya habari, huu ni udhaifu mkubwa,” alisema Kitana.

Kwa upande wake, Maryrose Majinge, alisema licha ya jina lake kupendekezwa, anasubiri maamuzi ya NEC.
Alisema nafasi za uongozi ndani ya CCM zinapaswa kuzingatia uwezo wa utendaji badala ya kuchagua watu kwa sifa ya kuzungumza au kwa majina ya wenzi wao.

Wiki iliyopita, kamati ya utekelezaji ya UWT iliyoketi mjini Dodoma ilipendekeza majina ya wanachama wake watatu kwenda NEC ya CCM kwa ajili ya kuwania uenyekiti wa jumuiya hiyo. Waliopendekezwa ni Mwenyekiti wa sasa, Sophia Simba, Anne Kilango na Maryrose Majinge.
Chanzo: Tanzania Daima

Wednesday, September 12, 2012

Balozi wa Marekani auawa Libya

Best Blogger Tips
 Balozi wa Marekani nchini Libya ameuawa baada ya kushambuliwa na watu waliokuwa wamejihami na kuvamia ubalozi wa Marekani Mashariki mwa mji wa Benghazi.

Balozi J Christopher Stevens, ni miongoni mwa maafisa wengine wa ubalozi waliouawa kufuatia maandamano kuhusu filamu iliyotolewa nchini humo ikimkejeli Mtume Muhammad.

Idara ya mambo ya ndani nchini Marekani, imethibitisha tu kifo cha afisaa mmoja wa ubalozi huo ingawa bado haijataja jina lake.

Maandamano ya kupinga filamu hiyo pia yalifanyika mjini Cairo dhidi ya ubalozi wa Marekani.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton, amelaani mashambulizi hayo.

Serikali ya Libya imetaja shambulio hilo kama kitendo cha uoga.
Ubalozi huo uliteketezwa na watu waliojihami kwa bunduki kulalamikia filamu moja iliyotengenezewa nchini Marekani ambayo wanasema inamdhihaki Mtume Mohammed.

Wanamgambo hao wanaoripotiwa kuwa na ufungamano na kundi la waislamu wenye msimamo mkali walitumia maguruneti ya kurushwa kwa roketi kuvamia ubalozi huo kabla ya kuiteketeza. Maafisa wa Libya wameiambia BBC kwamba hali imetulia kwa sasa.

Machafuko hayo ya Libya yalijiri saa kadhaa baada ya maelfu ya waandamanaji kukusanyika nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo kuelezea hasira zao kuhusu filamu hiyo kumhusu Mtume Mohammed.

Kwa wakati mmoja waandamanaji hao waliingia ndani ya ubalozi huo na kuichana bendera ya Marekani na kurejesha yao.
Chanzo: BBC

Wednesday, September 5, 2012

Al-Senussi akabidhiwa kwa watawala wa Libya

Best Blogger Tips
 Serikali ya Mauritania imewakabidhi maafisa wa utawala wa Libya aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini humo, Abdullah al-Senussi.

Libya inataka kumfungulia mashtaka bwana Senussi kwa makosa aliyoyafanya chini ya utawala wa hayati Muamar Gaddafi.

Mapema mwezi huu rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz alisema kuwa bwana Sanusi aliyekuwa amekimbilia nchini humo, sharti kwanza akabiliwe na sheria kwa makosa ya kuingia Mauritania kinyume na sheria.

Senussi alitoroka Libya baada ya mapinduzi ya mwaka jana ambayo yalimng'oa mamlakani Muammar Gaddafi.

Pia anatakiwa na Ufaransa pamoja na mahakama ya kimataifa kuhusu haki za bianadamu ICC kwa makosa ya kukiuka haki za binadamu.

Ripoti za kukabidhiwa kwake kwa watawala wa Libya, zilitolewa na televisheni ya taifa pamoja na shirika rasmi la habari la Mauritania.

Kulingana na ripoti, bwana Senussi alikabidhiwa kwa wajumbe wa Libya walioongozwa na waziri wa sheria na haki wa nchi hiyo. Lakini hadi sasa bwana Senussi hajulikani aliko.
Chanzo: BBC

Monday, September 3, 2012

Mauaji Iringa yamtesa IGP

Best Blogger Tips
 TUKIO la kuuawa kwa mwandishi wa habari wakati polisi wakipambana na wafuasi wa Chadema mkoani Iringa, limelitikisa jeshi hilo na jana Mkuu wake (IGP), Said Mwema alilazimika kujifungia na vigogo wa polisi Mkoa wa Iringa kujadili suala hilo.

Wakati IGP Mwema akifanya mkutano huo, uliodumu kwa zaidi ya saa mbili na nusu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi amelazimika kukatisha ziara yake ya kikazi Afrika Kusini na kurejea nchini kushughulikia suala hilo.

Mwema alienda Iringa jana na kuitisha mkutano huo uliowahusisha pia viongozi wa Chadema, akiwamo Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa katika mazingira yaliyoelezwa kuwa na ulinzi mkali.
Hii ni mara ya kwanza IGP Mwema kwenda mwenyewe kwenye mikoa kunakotokea vurugu kati na vyama vya siasa na baadaye mauaji ya raia.

Julai 15, mwaka huu vurugu za aina hiyo zilitokea mkoani Singida ambako Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Ndago wilayani Iramba, Yohana Mpinga aliuawa kwa kupigwa na silaha za jadi.

Pia mkoani Morogoro, Ally Zona aliuawa katika vurugu zilizoibuka baina ya polisi na wafuasi wa Chadema katika haraka za jeshi hilo kuwasambaratisha wafuasi hao kwa kile ilichoeleza kuwa maandamano yao yalipigwa marufuku.
Katika vurugu zote hizo, IGP amekuwa akituma wawakilishi au kutumia polisi kwenye mkoa husika kushughulikia matatizo hayo.

Makubaliano ya kikao
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zimeeleza kuwa polisi imekubaliana na Chadema na Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kusitisha majadiliano yote yanayohusu kifo cha mwandishi huyo hadi mazishi yake yatakapokamilika.

Mwenyekiti wa UTPC, Kenneth Simbaya alisema baada ya mkutano huo kuwa wamekubaliana kuwa na mkutano mwingine baada ya shughuli za mazishi kukamilika.

“Tulichoomba kifanyike ni kwamba, tumzike mwenzetu halafu majadiliano mengine juu ya ilikuwaje kwa nini na nini kifanyike kwa siku za usoni yatakuja,” alisema Simbaya.
Alisema sasa wanasubiri mwili wa Mwangosi ufanyiwe uchunguzi na wataalamu kutoka Dar es Salaam kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Francis Godwin alisema uchunguzi wa awali wa IPC unapingana kwa asilimia zote na taarifa ya jeshi hilo kwa kuzingatia taarifa zilizotolewa na baadhi ya waandishi waliokuwapo katika tukio hilo.

“Taarifa kutoka katika vyanzo vyetu zinaonyesha kwamba Mwangosi alipigwa kwa virungu kabla ya kulipuliwa na bomu hilo ambalo kwa vyovyote vile mhusika wake mkuu anaweza kuwa jeshi hilo na ili taarifa hiyo potofu isiendelee kuugubika umma, IPC imeamua kutoa tamko linalolenga kuviarifu vyombo huru viingilie kati uchunguzi,” alisema Godwin.

Nchimbi akatisha ziara
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi jana alilazimika kukatisha ziara yake ya kikazi, Afrika Kusini na kurudi nchini ambako pamoja na mambo mengine, atazungumza na waandishi wa habari leo kuhusu tukio hilo.

Nchimbi anarejea nchini wakati Naibu wake, Pereira Ame Silima akikataa kulizungumzia akisema uchunguzi umeshaanza.

Silima alisema tukio hilo linachunguzwa kwa pamoja kati ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba na IGP Mwema... “Mwema na Manumba wanaelekea Iringa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa tukio hilo na baadaye ndipo jeshi la polisi litaweza kueleza ni kitu gani hasa kimetokea.”

Alisema kwa sasa lolote litakalozungumzwa juu ya tukio hilo litakuwa ni hisia tu na ukweli utajulikana baada ya uchunguzi huo kukamilika.

Channel Ten yanena
Uongozi wa kampuni ya Africa Media Group ambao wanamiliki Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, umeitaka Serikali kuanzisha uchunguzi huru ili kubaini sababu na mazingira ya kuuawa kwa mwandishi huyo ambaye alijiunga na kampuni hiyo mwaka 2006.

Taarifa iliyotolewa na kampuni na kusainiwa na Mhariri Mkuu wa Channel Ten, Dina Chahali imetaka uchunguzi huru kufanyika na kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Tunalaani vikali tukio hili ambalo halikubaliki kwa jinsi yoyote ile, tunataka kuanzishwa uchunguzi huru na hatimaye nguvu za kisheria zitumike,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Chanzo: Mwananchi

Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits