Friday, September 3, 2010

Best Blogger Tips
Dk.Slaa amtega Makamba

Via ippmedia

.Amtaka atoboe kilichomfukuzisha ualimu
.Vinginevyo atayaanika yote aliyoyatenda
.Kingunge naye atumbukia hoja ya ndoa

Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, amesema Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, hana ubavu wa kuhoji masuala ya uadilifu wa ndoa.

Alisema badala yake, Makamba anapaswa kuuelezea umma sababu zilizomfanya afukuzwe katika kazi ya ualimu akiwa Mkuu wa shule ya msingi.

Dk. Slaa alivunja ukimya jana alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni katika uwanja wa Kwaraha mjini Babati.

Dk. Slaa alisema ndoa yake kamwe haijamshinda na kwamba hakuna mwenye uwezo wa kumchagulia mke na kwamba kufunga ndoa ni makubaliano ya watu wawili.

Alitumia fursa hiyo kumtambulisha mke wake, Josephine na kuhoji, “kipi bora kuwa na mke mmoja hadharani au kuwa na nyumba ndogo nyingi?”

Pia alivunja ukimya na kuamua kujibu tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake na wapinzani wake wa kisiasa hasa masuala ya Ukatoliki, kuacha upadre na maisha yake ya ndoa.

Aidha, Dk. Slaa alieleza kusikitishwa kwake na kitendo cha polisi kusimamisha magari ya msafara wake juzi, na kuwataka kutenda haki na kusimamia kile walichokubaliana katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.
Endelea kusoma habari hii..............................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits