Thursday, September 2, 2010

Best Blogger Tips
Slaa amvaa mke wa Kikwete

Via Mwananchi

KAMPENI za uchaguzi mkuu zimezidi kunoga baada ya mgombea urais wa Chadema, Dk Slaa kumgeukia mke wa Rais Jakaya Kikwete akieleza kuwa anatumia vibaya rasilimali za nchi kumpigia kampeni mumewe huku akimtaka katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba aeleze kisa cha kufukuzwa ualimu mkuu wa shule ya msingi.

Kwa muda mrefu Salma Kikwete, mke wa Rais Kikwete na ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), amekuwa katika ziara kwenye mikoa mbalimbali, jambo ambalo limekuwa likitafsiriwa kuwa anafanya ziara za kampeni kwa ajili ya mumewe. Kwa sasa yuko mkoani Manyara.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni, Dk Slaa ambaye ameripotiwa kuwa na makombora 20 kwa ajili ya kuimaliza CCM, alisema kitendo cha mke huyo wa rais kumpigia kampeni kwa kutumia rasilimali za umma ni ufisadi.

“Mke wa rais si rais," alisema Dk Slaa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Kwara ulio Babati Mjini.

"Mama Salma anatembea na askari wa serikali; magari ya serikali na wakuu wa mikoa na wilaya. Anatumia fedha za Ikulu kwa sababu walinzi wake wanalipwa na Ikulu. Huu ni ufisadi.”
Endelea kusoma habari hii......................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits