Monday, August 29, 2011

Familia ya Gaddafi yatorokea Algeria

Best Blogger Tips
Mke wa Kanali Gaddafi wanawe wa kiume na binti yake
Mke na watoto watatu wa kiongozi wa Libya aliye mafichoni Muammar Gaddafi wako nchini Algeria, maafisa wa Algerian wamesema.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema mke wa kanali Gaddafi, Safia, binti yake Ayesha na watoto wa kiume Muhammad na Hannibal waliondoka Libya mapema Jumatatu.

Balozi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa amesema walipokelewa kwa misingi ya kibinadamu.

Waasi wa Libya wamesema kuwapa hifadhi familia ya Gaddafi ni kitendo cha uchokozi, na wametaka warejeshwe nchini Libya.

Haijulikani mahali alipo Kanali Gaddafi.

Wakati huo huo waasi wamesema mtoto mwingine wa kiume wa Kanali Gaddafi, Khamis, huenda aliuawa katika mapigano karibu na Bani Walid.

Taarifa hizo zimetolewa wakati waasi wa Libya wakijaribu kumaliza upinzani uliopo katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo yanayomtii Gaddafi, na kujiandaa kuendelea kwenda katika mji aliozaliwa kanali Gaddafi wa Sirte ili kumalizia upinzani unaonekana kuwa ngome yake ya mwisho.

Kuwasili kwa mke wa kanali Gaddafi na watoto watatu nchini Algeria kuliripotiwa Umoja wa Mataifa na kwa viongozi wa waasi wa Libya, wizara ya mambo ya nje ya algeria imesema katika taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la Algeria, APS.

Taarifa hiyo imesema familia ya Gaddafi walivuka mpaka kati ya Libya na Algeria Jumatatu, saa Mbili na dakika arobaini na tano za huko.

Algeria ni mahali dhahiri pa kukimbilia familia ya Gaddafi kutokana na nchi mbili hizo kuwa na mpaka mrefu na serikali ya Algeria bado halijalitambua Baraza la Mpito la Taifa la Libya.
Source: BBC

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits