Tuesday, August 31, 2010

Best Blogger Tips
Shule iliyokumbwa na mashetani

Via darleo

BAADA ya zaidi ya wanafunzi 26 wa Shule ya Msingi Tumaini kuanguka jana na maruhani leo shule hiyo ilionekana kupwaya baada ya wanafunzi kutofika shuleni wakihofia kukumbwa na masaibu hayo.

Gazeti hili leo asubuhi lilishuhudia shule hiyo ikiwa na idadi ndogo ya walimu na wanafunzi, hali ambayo ilizidi kuifanya shule hiyo kuzizima kutokana na ukimya uliokuwapo.

Imebadinika kuwa baadhi ya wazazi wamelazimika kuwakataza watoto wao kwenda shule kwa kuhofia kukumbwa na balaa hilo.

Akizungumza na gazeti hili leo asubuhi, mwalimu mmoja wa shule hiyo ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini kwa madai kuwa si msemaji, alidai kuwa tukio hilo si la kwanza na kwamba kuna uwezekano kukawa na tatizo.

“Kuna taarifa kuwa eneo hili lilikuwa ni la makaburi, hivyo kuna maruerue yanayojitokeza,” alidai mwalimu huyo.
Jana mwalimu mmoja wa shule hiyo, Godfrey Wilbard, wakati akifundisha darasani, ghafla alisikia wmanafunzi mmoja akipiga mayowe akidai kuwa anaona watu walioko uchi na huku wakimwita.
Baada ya muda mwanafunzi huyo alizirai huku akifuatiwa na wanafunzi wenzake wadarasa la saba.

Kutokana na hali hiyo kuendelea idadi ya wanafunzi ilizidi kuongezeka kuanguka jambo lililozua utata kwa wazazi wa wanafunzi hao kulazimika kukimbilia shuleni hapo.

Imedaiwa kuwa wakati wanafunzi hao walikuwa wakizungumza maneno ya yasiyoeleweka ambapo walimu na wazazi walilazimika kuwakimbiza kwenye kanisa la Assembles of God lililopo jirani kwa ajili ya kuombewa.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni saa 4.30, bado idadi ya wanafunzi shuleni hapo ilikuwa ndogo na hata waliokuwepo walionekana kuwa na woga.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits