Thursday, December 16, 2010

Best Blogger Tips
Buriani Dr. Remmy Ongala


Mwanamuziki maarufu nchini Tanzania Ramadhan Mtoro Ongala, amezikwa leo katika makaburi ya sinza, jirani kabisa na nyumbani kwake alikokuwa anaishi yeye na familia yake.


Bendi mbalimbali zilipiga muziki, zikiwemo za muziki wa injili , bendi ya wasiojiweza, na kadhalika. Muungano wa Bendi za injili ulipiga wimbo ambao waliutunga na kuurekodi maalumu kumuaga Dr. Remmy Ongala.

Wimbo wake maarufu ujulikanao kama Siku ya kufa, ulipigwa wakati  wakati wa  kumuaga, kitu ambacho kiliwatoa machozi waombelezaji wengi.

Serikali iliwakilishwa na Waziri wa Habari na Utamaduni Dr. Emmanuel Nchimbi katika mazishi hayo.

Mwenye- ezi- Mungu Umuweke Mahala Pema Peponi  Dr. Remmy Ongala.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits