Friday, December 3, 2010

Best Blogger Tips
Urusi Kuandaa Kombe la Dunia 2018


Urusi itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018, wakati  michuano ya mwaka 2022 itaandaliwa na  Qatar.

Shirikisho la kandanda duniani- FIFA,  lilitangaza maamuzi yake ya nafasi hizo  mbili kwenye  sherehe iliyofanyika  Zurich Alhamisi. Rais wa FIFA, Sepp Blatter alitoa tangazo hilo kwa wajumbe kutoka mataifa yote yaliyowasilisha maombi.

Urusi ilichaguliwa kuwa mwenyeji michuano ya  mwaka 2018 dhidi ya Uingereza na maombi ya pamoja  kutoka Spain na Ureno na ubelgiji  na uholanzi. Qatar ilichaguliwa dhidi ya Japan, Korea kusini, Australia na Marekani kuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka 2022.

Qatar itakuwa nchi ya kwanza ya  mashariki ya kati,  kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa urusi  kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits