Thursday, December 2, 2010

Best Blogger Tips
Chadema chamlima barua Zitto, wabunge tisa

SAKATA la wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akihutubia, limechukua sura mpya baada ya chama hicho kuwaandikia barua wabunge ambao hawakushiriki akiwemo Zitto Kabwe, kuwataka waeleze sababu za kutoonekana.

Uamuzi huo umetolewa takribani siku 20, baada ya Chadema kudhihirisha msimamo wa kutotambua matokeo ya uchaguzi ya urais kwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge na kususia sherehe za kuapishwa kwa Mizengo Pinda kuwa Waziri Mkuu, katika hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.

Akizungunza na Mwananchi jana, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu alisema wabunge 10 kati ya 13 ndio wanaotakiwa kujieleza na kwamba, hatua hiyo imefikiwa baada ya kwenda kinyume na maamuzi ya pamoja ya chama na kutotoa taarifa yoyote ya kutokuwepo kwao bungeni.

“Tunachotaka kujua kwa wabunge hawa kumi ni kwamba, kwa nini hawakuja katika kikao cha Bunge siku hiyo,’’ alifahamisha Lissu na kuongeza:
“ Hatua hii imefikiwa baada ya wabunge hao kwenda kinyume na maamuzi ya chama pamoja na kutotoa taarifa ya kutohudhuria kwao’’.Hata hivyo, Lissu alisema bado hawajawakabidhi rasmi barua hizo, lakini zipo katika hatua ya mwisho na kwamba watakabidhiwa wakati wowote kuanzia sasa.

Aliwataja wabunge hao kuwa ni Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Said Arfi (Mpanda Mjini) ambaye ni Naibu Mwenyekiti Taifa wa chama hicho, Mhonga Luhwanya (Viti Maalum), Jonh Shibuda (Maswa Magharibi), Maulida Komu (Viti Maalum).

Wengine ni Profesa Kulikoyele Kahingi,(Bukombe),  Rachel Mashishanga(Viti Maalum), Raya Ibrahimu(Viti Maalum), Lucy Owenya (Viti Maalum) na Suzan Lyimo(Viti Maalum).

“Lakini wabunge John Mnyika (Ubungo) na Halima Mdee (Kawe), walitoa udhuru kwamba walikuwa wanaumwa na Philemon Ndesamburo (Moshi Vijijini) alikuwa safarini. Hawa hawatapewa barua ya kujieleza, ’’ alisema Lissu.

Lissu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chadema, alifahamisha kuwa kitendo hicho kikiachwa bila kukemewa, ingeondoa umuhimu wa vikao vya chama na maamuzi.
Endelea kusoma habari hii.................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits