Sunday, March 27, 2011

Best Blogger Tips
Adaiwa kumbaka mtoto wa mkewe

Via HabariLeo

POLISI mkoani Tabora wamemkamata mkazi wa Kijiji cha Mtakuja, Amos Gambo kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kike wa mkewe mwenye umri wa miaka minane.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow, alisema, Gambo ambaye alitoweka tangu mwezi uliopita baada ya kudaiwa kufanya kitendo hicho, alitiwa mbaroni jana jioni.

Barlow alisema, mtuhumiwa alikamatwa kijijini hapo baada ya kumpigia simu mkewe (jina limehifadhiwa) akimlalamikia kuwa anakunywa pombe.

Kwa mujibu wa Kamanda Barlow, ndugu waliokuwepo walibaini kwamba mtuhumiwa huyo alipiga simu hiyo akiwa kijijini hapo na si nje ya Kijiji cha Mtakuja, kilichopo Manispaa ya Tabora.

Kamanda alisema, baada ya polisi kupata taarifa hiyo kutoka kwa mama wa mtoto aliyebakwa, walijaribu kumpigia simu na hatimaye kumtia mbaroni na kumfikisha kituoni.

Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya mahojiano ya wapelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kitendo hicho mwezi uliopita baada ya mama wa mtoto huyo kuondoka nyumbani kwenda kulala msibani kwa majirani.

Mama aliporejea alimkuta binti yake akiwa katika hali mbaya na alipomchunguza, alibaini kwamba alikuwa amebakwa .

 

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits