Wednesday, March 30, 2011

Best Blogger Tips
Rushwa Loliondo

Via Newhabari

MDUDU rushwa tayari ameingia kwenye utaratibu wa kuruhusu magari yenye watu wanaokwenda kunywa dawa kwa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, katika Kijiji cha Samunge, Loliondo mkoani Arusha.


Mamia ya magari yaliyokuwa yamezuiwa juzi katika maeneo ya Meserani, Makuyuni na Mto wa Mbu, yaliruhusiwa kwenda Samunge baada ya madereva kutoa rushwa. Polisi walio kwenye vizuizi ndio watuhumiwa wakuu wa vitendo hivyo.

Kuzuiwa kwa magari hayo hadi Aprili Mosi ilikuwa ni utekelezaji wa ombi la Mchungaji Masapila kwa Serikali la kuzuia magari zaidi kuingia Samunge hadi wale waliopo watakapokuwa wameshapata dawa na kuondoka.

Mamia ya magari juzi yalizuiwa katika vituo vya Mesereni, Makuyuni na Mto wa Mbu wilayani Monduli. Yote yalikuwa na idadi kubwa ya watu.

Baadhi ya watu waliozungumza na MTANZANIA wamesema kuwa magari hayo yalianza kuruhusiwa baada ya wahusika kutoa rushwa.

Vitendo hivyo vilianza muda mfupi baada ya Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, kuondoka katika Kijiji cha Mto wa Mbu.

“Baada ya Makamu wa Rais kupita, polisi na viongozi waliyokuwa wakidhibiti magari walifungua mradi wa kukusanya pesa na kuyaruhusu yote kwenda Loliondo, hawakuwa na wasiwasi katika kukusanya pesa hizo,” alisema mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo.

Jana kwenye vituo vyote vitatu hapakuwapo askari wala magari yaliyozuiwa kwenda Samunge.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, hakupatikana kuzungumzia suala hilo baada ya simu yake kutopokewa.
Endelea kusoma habari hii...................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits