Saturday, August 7, 2010

Best Blogger Tips
Dk. Slaa ateka Moshi, Tanga

Leo kunguruma jijini Dar

Via ippmedia

Umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Moshi na wilaya za jirani juzi walijitokeza kwa wingi kumlaki mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Willbroad Slaa.

Wananchi hao ambao walijitokeza kwa maandamano ya magari, pikipiki na baiskeli walitembea maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na baadaye majira ya saa tisa alasiri walikwenda kumlaki Dk. Slaa katika uwanja mdogo wa ndege mjini hapa.

Vifijo na nderemo zilizidi pale Dk. Slaa na msafara wake ulipoingia kwenye eneo la mkutano katika viwanja vya Manyema kata ya Bondeni majira ya saa 11:30, huku wananchi wakionyesha ishara ya Chadema na kila aina ya shauku ya kumuona.
Endelea kusoma habari hii......................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits