Wednesday, August 18, 2010

Best Blogger Tips
Kibao chageukia aliyechukua nafasi ya Bashe Nzega

Via ippmedia

 Wakati msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga, akisema kuwa kwa mujibu wa nyaraka zilizoko, mgombea ubunge jimbo la Nzega aliyeenguliwa, Hussein Bashe, ni raia wa Tanzania, aliyepewa nafasi yake na Chama Cha Mapinduzi (CCM), naye ameibua mambo mapya juu ya uraia wake.

Taarifa kutoka jimboni humo zilieleza Dk. Hamis Andrew Kigwangala ambaye alipitishwa na chama hicho uraia wake unadaiwa kuwa na utata.

Kuna taarifa kwamba Dk. Kigwangala jana alihojiwa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji katika ofisi za Wilaya ya Nzega wakati akirudisha fomu ya kuwania ubunge kwa msimamizi wa uchaguzi.

Dk. Kigwangala aliteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kugombea nafasi hiyo baada ya Bashe aliyekuwa mshindi katika kura za maoni kuenguliwa baada ya kudaiwa kwamba sio raia wa Tanzania.

Habari hizo zilieleza kwamba, Dk. Kigwangala naye uraia wake una utata na kwamba jina alilotumia shuleni (Hamis Andrew) sio la kwake na kuwa mwenyewe yupo wilayani humo, lakini hivi sasa inadaiwa kwamba amefichwa.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba jina lake halisi ni Said Nassor Magaile.

Aidha, inadaiwa kwamba baada ya mgombea huyo kushtukia uraia wake, jana alikimbilia katika Mahakama ya Wilaya kukana jina lake halisi ambalo ni Said Nassor.
Endelea kusoma habari hii.........................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits