Sunday, August 1, 2010

Best Blogger Tips
Vituko Vya Uchaguzi - TZ

AONYWA KUJIITA OBAMA
KATIKA jimbo la Bunda, kulikuwa na habari kuwa mgombea Ginche Kisase, ameonywa akitakiwa kuacha kujinadi kwa kutumia jina la Rais Barack Obama wa Marekani, kwa kuwa hawafanani. Onyo hilo lilitolewa na wanachama wa CCM kata za Kunzugu na Mcharo, wakati mgombea huyo akijinadi kuomba kura. Hilo liliibuka baada ya Kisase kusimama kujinadi na kudai anafahamika zaidi kama Obama, jina ambalo alidai amepewa na wananchi. Baada ya kujinadi hivyo, baadhi ya wanachama waliguna, huku wengine wakizomea na kupaza sauti kuashiria kutokubaliana naye. Kwa upande wake, Kisase alisema mtu akitaka kumuita Obama yuko huru na asipotaka anaweza kumuita vingine.

AJINADI KWA KUOGESHA WAZEE
MGOMBEA ubunge, Peter Msuya, aliwavunja mbavu wanachama wa CCM wakati akinadi sera zake, kwa kusema akichaguliwa atajenga kituo cha kuwaosha vikongwe. Msuya anayewania jimbo la Ubungo, alisema kuanzishwa kituo hicho kutaleta ajira kwa vijana, kwani hata Ulaya watu wanafanya kazi hizo na kujipatia fedha na kununua magari ya kifahari na kuahidi kuwa, fedha za mfuko wa jimbo zitatumika kutatua kero jimboni humo. Naye mgombea Alfred Nchimbi, akijinadi alisema anatakiwa kiongozi atakayeleta maendeleo na si kupiga kelele.
Source: Uhuru

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits