Tuesday, August 3, 2010

Best Blogger Tips
Kikwete aomboleza kifo cha Jidulamabambasi

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kutokana na kifo cha Amani Jidulamabambasi kilichotokea juzi.

Jidulamabambasi alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM waliokuwa wamejitokeza kuwania kuteuliwa na kugombea Ubunge Maswa Magharibi.

“Ninakutumia salamu za rambirambi wewe Katibu Mkuu wa CCM na wana– CCM kote nchini kwa kumpoteza mmoja wa makada katika chama chetu”, alisema Kikwete.

Aliongeza, “aidha kupitia kwako, natuma salamu za rambirambi na pole nyingi kwa familia ya marehemu Amani kwa kuondokewa na kiongozi muhimu wa familia yao.”

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Kikwete amemwelezea Amani kuwa miongoni mwa makada jasiri wa CCM wasiokata tamaa katika medani za siasa na mpambanaji hodari aliyekuwa na dhamira ya dhati ya kulitumikia taifa na umma wa Watanzania.
Source: HabariLeo

1 comment:

Anonymous said...

We all love you but God loves you more. Rest in Peace Amani.


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits