Thursday, August 19, 2010

Best Blogger Tips
Mwanamume akutwa amefia chumbani Dar

MWANAMUME Omari Disomba, maarufu kwa jina la Kitimutimu (54), ambaye kazi yake ilikuwa ni dereva teksi, amekutwa amekufa chumbani kwake huku maiti yake ikiwa kitandani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, amesema tukio hilo limetokea jana saa 12 jioni, Ubungo Kibo.

Amesema mwili wa marehemu huyo umekutwa hauna jeraha lolote na chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika.

Kwa mujibu wa Athuman Amri (34), mkazi wa Ukonga Magereza, enzi za uhai wake marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

Maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi na upelelezi unaendelea.

Wakati huo huo, polisi inawashikiliwa wakazi wanane kwa tuhuma za kukutwa na bangi puli 47, miskoto 60 na pombe haramu ya gongo lita 20.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, amesema watuhumiwa hao walikamatwa jana saa 3 asubuhi, Magomeni Mapipa, Bonde la Madaba.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Scola Mambo (43), Ramadhani Saidi (24), Hawa Adamu (18), JUlieth JOhn (34) na wenzao wanne.
Source: Darleo

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits