Monday, October 25, 2010

Best Blogger Tips
Mauaji Maswa: Shibuda aachiwa huru JESHI la Polisi limemwachia huru mgombea ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Shibuda, kwa madai hakuhusika na mauaji yaliyosababishwa na vurugu zilizotokea katika Kijiji cha Kizungu, wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Maswa jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba, alisema wameamua kumwachia huru mgombea huyo kutokana na upelelezi wa awali kuonyesha kuwa hakuhusika na tukio hilo.

Alisema upelelezi huo umeonyesha wazi kuwa hakuwepo katika eneo la tukio ambapo mauaji hayo yalipotokea baada ya wafuasi wa vyama vya CHADEMA na CCM waliposhambuliana na kusababisha kifo cha Stephen Kwilasa.

“Unajua linapotokea tukio kama hilo la mauaji ni lazima tufanye upelelezi kwa makini, ili kuweza kutenda haki kwa pande zote na sisi kama polisi tupo hapa kwa ajili ya kulinda usalama wa raia, hasa katika matukio haya ya kampeni za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu, ni lazima tufanye kazi kwa umakini mkubwa,” alisema.

Alisema bado wanaendelea na upelelezi na iwapo itabainika kwa namna moja au nyingine alihusika na tukio hilo, atafikishwa mahakamani na kuongeza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Aidha, alisema Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Kata ya Nyalikungu, Abel Jombo, amelalamika katika Kituo cha Polisi Maswa dhidi ya Shibuda akidai kuwa alimpiga mateke alipopelekwa katika eneo la mkutano, ambapo alikuwa akihutubia mgombea huyo na kusisitiza kuwa upelelezi wa tukio hilo haujakamilika.
Endelea kusoma habari hii..............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits