Monday, January 23, 2012

Best Blogger Tips
 
Uamuzi huu metolewa  leo katika mfulilizo wa Mikutano waliyoianza toka jumatano ya wiki iliyopita (18/01/2012) katika  kujaribu kutafuta suluhu ya matatizo yao na ya Sekta ya Afya kwa Ujumla,Juhudi hizo hazikuzaa matunda kutoka kwa Serikali kuanzia ngazi ya Wizara ya Afya mpaka ofisi ya Waziri Mkuu ambapo kutozaa matunda.

Madaktari/watumishi wa afya hao wana madai kadhaa ikiwemo

*Kuboresha Huduma za Afya nchini (hospitali na vitanda kwa kila mgonjwa inawezekana)

*Maslahi Duni kwa watumishi wa sekta ya afya

*Malipo kwa kazi za ziada kwani   Madktari wanalipwa shilingi 10,000/=  kwa kukesha na kufanya kazi masaa 36 tofauti na taratibu za serikali ambapo ilitakiwa walipwe  shilingi 40,000(half pediem) kama taratibu za serikali zinavyoonesha lakini viongozi wa Wizara hasa Mama Blandina Nyoni wamekuwa wakikwamisha hili.

*Haki ya kupewa nyumba  au posho ya Nyumbai kama muongozo wa utumishi wa umma  wa serikali ya Tanzania unavyoelekeza ule wa mwka 1994 na wa mwaka 2009..

*Kulipwa posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi(Risk allowance)

*Lingine ni Kuondolewa kwa Katibu mkuu wa wizara ya afya Bi.Blandina Nyoni ambaye anaonekana kuwa ni kikwazo katika juhudi za msingi katika kuboresha sekta ya afya Tanzania.


*Bi Blandina Nyoni anatuhumiwa kutoa kauli ya kejeli  kwa watumishi wa afya kuwa anamshukuru baba yake kwa kumkataza kusomea mambo ya afya kwani sekta ya ya afya haifai na ndio maana licha ya kufaulu masomo ya sayansi baba yake alimshauri asomee uhasibu.

Maamuzi hayo magumu yamefikiwa katika Mkutano wa leo uliofanyika Don Bosco Upanga DSM ikiwa ni mwendelezo wa Mikutano isiyokoma iliyoanza Toka jumatano ya Wiki iliyopita.No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits