Tuesday, April 20, 2010

Best Blogger Tips
Jela miaka 30 kwa kumbaka Bi kizee


MKAZI wa Kijiji cha Kitowo Olele wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, Priscus Peter Kimario amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka bibi kizee mwenye umri wa miaka 87.

Hukumu ya kesi hiyo iliyovuta hisia za wananchi wengi wa wilayani hapa ilisomwa jana na hakimu mfawidhi wa wilaya ya Rombo, Aziza Temu ambaye aliamuru pia mshitakiwa kuchapwa viko 12 na kulipa faini ya Sh100,000.

Bibi kizee huyo, Lucia Lokela alifariki dunia Oktoba 17, 2007 hata kabla ya kutoa ushahidi wake lakini mahakama ikachukua maelezo yake ya awali kuwa ushahidi, kwa mujibu wa kifungu namba 34(D) cha sheria ya ushahidi.

Upande wa mashitaka ukiongozwa na Inspekta Richard Busimba ulidai kuwa Julai 2,2007 mshitakiwa huyo alimbaka bibi kizee huyo, kitu ambacho ni kinyume na sheria ya makosa ya kujamiiana.

Tangu mwanzo wa usikilizwaji wa kesi hiyo hadi hatua ya utetezi, mshitakiwa huyo alikuwa akikanusha kutenda kosa hilo ingawa alikuwa akikiri kwamba siku hiyo na muda huo alikuwa katika kijiji hicho kwenye sherehe ya kijadi.

Hata hivyo, Hakimu Temu alisema mashahidi wanne wa upande wa mashitaka katika kesi hiyo wameithibitishia mahakama bila shaka yoyote kwamba mshitakiwa huyo ndiye mshiriki mkuu wa tukio hilo.

“Mahakama inatupilia mbali utetezi wa mshitakiwa kwa sababu upo ushahidi kuwa alikamatwa red handed (alifumaniwa) akiwa amemlalia bibi kizee huyo ambaye kwa bahati mbaya sana sasa ni marehemu,” alisema Temu.

Kwa mujibu wa hakimu huyo, mahakama ilikubaliana na hoja ya upande wa mashitaka ya kutaka kutolewa kwa adhabu kali kwa kuwa vitendo vya ubakaji na udhalilishaji wanawake na watoto ambavyo vinazidi kuongezeka kwenye jamii.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits