Friday, April 2, 2010

Best Blogger Tips
'Serikali hii kiziwi'

Via Raia mwema

UAMUZI wa Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe, kutangaza nia ya kujiuzulu ubunge na uanachama wa CCM na kujiunga na Chama Cha Jamii (CCJ) kama ilivyoandikwa kwa mara ya kwanza na Raia Mwema kwamba nyuma ya chama hicho kuna vigogo wa CCM, kimezidi kukitikisa chama hicho kikongwe nchini kinachozongwa na baadhi ya viongozi wenye tuhuma za ufisadi, ikielezwa orodha ya watakaohama ni ndefu na vigezo vinavyosubiriwa ni muda na ‘jukwaa’ muafaka.

Katika hatua yake ya kutangaza nia hiyo jana Jumanne, Mpendazoe aliita Serikali ya sasa kuwa ni kiziwi kwa kilio cha wananchi, ikibaki kusikiliza zaidi wafanyabiashara na matajiri haramu na wakati huo huo, akisema Kamati ya Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi ya kusuluhisha wabunge wa CCM ni upotezaji muda.

Lakini wakati hayo yakiendelea kwa upande wa Mpendazoe, Makamu Mwenyekiti wa CCM – Tanzania Bara, Pius Msekwa, katika hali isiyokuwa ya kawaida, amelazimika kuweka bayana kuwa kikao cha Kamati Kuu ya chama chake, kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii, hakikujadili kumfukuza mwanachama yeyote, kwa sababu yoyote.

Mpendazoe alitangaza jana Jumanne, jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), mbele ya waandishi wa habari, uamuzi wake huo wa kujivua uanachama wa CCM na ubunge. Miongoni mwa sababu za kujiengua alizozitaja ni pamoja na CCM kupoteza dira, sababu ambazo ziliwahi kuzungumzwa na aliyepata kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba.

Kolimba alitoa kauli hiyo akiwa bado ndani ya CCM, kauli ambayo ilimgharimu kiasi cha kuitwa kujieleza katika Kamati Kuu ya CCM, ambako kutokana na sababu za kiafya, alianguka na kukimbizwa hospitalini na baadaye kupoteza maisha.
Endelea kusoma habari hii.........

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits