Friday, April 2, 2010

Best Blogger Tips
JK awapoza hasira wafanyakazi nchini

Via Tanzania Daima

RAIS Jakaya Kikwete amelisihi Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) lisiitishe mgomo wa wafanyakazi kwa nchi nzima kama lilivyotangaza, bali wakae kwenye meza ya mazungumzo na serikali kwa lengo la kumaliza tofauti zao na kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Katika hotuba yake ya kila mwezi kwa taifa iliyotolewa jana, Rais Kikwete alisema ametishwa na kauli za viongozi wa TUCTA kuhusu mgomo ulioitishwa unaotarajiwa kuanza Mei 5, akisema iwapo utafanyika, unaweza kuwa na athari kubwa kwa taifa.

Aliongeza kuwa miongoni mwa mambo yaliyomshtua ni kauli za jazba na kejeli za baadhi ya viongozi wa TUCTA, jambo lililomfanya achelee kulizungumzia kwa hofu ya kuingizwa katika zogo la kutupiana maneno.

Hata hivyo, alionya kuwa iwapo mgomo huo utafanyika, shughuli zote nchini zinazofanywa na watu walioajiriwa zitasimama kwa muda usiojulikana kuanzia siku hiyo, jambo ambalo limemfanya awasihi wasitishe mgomo wao.

“Nawasihi viongozi wa TUCTA kuufikiria upya uamuzi wao, waachane na mgomo na wakubali kufanya mazungumzo na serikali na waajiri wengine kwa kutumia mfumo uliopo kisheria.

“Nawasihi tuchague kuzungumza sasa kuliko kuzungumza baada ya mgomo kwani kuna hatari ya mahusiano yetu kuchafuliwa na misuguano inayotokana na mgomo,” alisema.

Rais Kikwete alidokeza kwamba serikali inawajali na kuwathamini wafanyakazi wa sekta ya umma au binafsi na mara kadhaa kumekuwa na hatua za kuboresha maslahi yao.

Alisema tangu iingie madarakani, serikali imeongeza mshahara wa kima chini mara tatu kuanzia mwaka 2006 kutoka shilingi 65,000 hadi 104,000 sasa, na hivi sasa inajiandaa kuongeza tena katika bajeti ijayo.
Endelea kusoma habari hii..........

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits