Friday, April 2, 2010

Best Blogger Tips
Wabunge wataka rais anunuliwe ndege nyingine

Via Mwananchi

WAKATI kelele kuhusu gharama za ndege ya rais zikiwa hazijapata majibu ya kuridhisha, Kamati ya Bunge ya Miundombinu sasa inataka mkuu huyo wa nchi anunuliwe ndege nyingine mpya kwa ajili yake na viongozi wengine.

Wabunge hao wanataka ndege hizo zitumike kwenye majanga ya kitaifa.Wabunge wa kamati hiyo walitoa ushauri huo licha ya kupewa taarifa fupi ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), iliyoeleza kuwa taasisi hiyo inaidai serikali deni linalofikia Sh6 bilioni.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Missanga alibainisha hayo jana mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam ambako vikao vya kamati mbalimbali za bunge vinaendelea.

"Labda niseme 'observation', yetu (tulichokiona), sijui nisemeje lakini, haya ni ya ndani. Kwa kifupi tumeridhishwa na ufanisi wa wakala hasa suala la usalama. Kwa upande wa ushauri tumeishauri TGFA kuwe na helkopta itakayotumika na viongozi wa kitaifa, kuwezesha kutua hata pasipo na uwanja wa ndege," alisema Misanga.

Alifafanua kuwa pamoja na helkopta, tunashauri serikali inunue ndege mbili ili ziwe mbadala wa ndege nyingine mbili aina ya Fokker 28 na Fokker 50 ambazo ni za siku nyingi.

“Kwa mujibu wa taarifa ya TGFA tumegundua kuna ndege mbili za siku nyingi, Fokker 28 na Fokker 50, ingawa bado zinafanya kazi vizuri, ushauri wa kamati ni kuwa serikali inunue ndege nyingine ‘kureplace’ (mbadala wa hizo) hizo kwani zimetimiza muda wa kubadilishwa," alisema Missanga.

"Tunatahadharisha katika ununuzi huo isitokee kama ilivyokuwa kwa ndege ya rais. Zinunuliwe zinazoweza kutua viwanja vingi kulingana na mazingira ya nchi."

Taarifa iliyowasilishwa na ofisa mtendaji wa TGFA , Keenan Mhaiki inaonyesha kuwa Fokker 28, iliyonunuliwa mwaka 1978, ina zaidi ya miaka 30 na kwamba imeruka asilimia 48 ya saa zilizotarajiwa kitaalamu.
Endelea kusoma habari hii.........

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits