Wednesday, April 14, 2010

Best Blogger Tips
Wabunge wauasa Ubalozi kuajiri wa Tanzania

Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje ya bunge la Tanzania Wilson Massilingi amezitaka balozi za Tanzania kutoa nafasi za ajira kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi hiyo na wenye vibali vya kuwawezesha kuishi na kufanyakazi katika nchi hizo.

Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Amerika VOA mjini Washington, Masilingi anasema itakuwa si busara kwa balozi za Tanzania kutoa ajira kwa wageni katika kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania wanaoishi katika nchi hizo.

Amewataka Watanzania kujitokeza pale inapotokea fursa ya nafasi ya kazi katika balozi za Tanzania zilizoko nje ya nchi hiyo.

Akiwa na wajumbe wenzake wa kamati ya bunge ya mambo ya nje Juma Kilimba na Khalifa Khalifa inayotembelea Marekani kukagua miundo mbinu ya balozi za Tanzania mjini Washington DC na New York mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa Muleba mashariki amesema itakuwa ni kichekesho kwa wageni kuajiriwa hata katika kazi kama za uhudumu wa ofisi au udereva wakati wapo Watanzania wanaofanya kazi kama hizo katika nchi hizo.

  Aidha Masilingi ameitaka wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kuangalia uwezekano wa kuongeza watumishi katika ubalozi wa Tanzania mjini Washington kutokana na ofisi hiyo kukabiliwa na uchache wa watumishi ukilinganisha na kazi zilizopo.
Source: VOA

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits