Friday, April 16, 2010

Best Blogger Tips
Sophia:Nimejifungua watoto watatu sina cha kuwapa

 Via Mwananchi

"Hivi kama msaada upo ni ufahari gani kujitangaza kuomba wakati najua kwamba watu wengi kwanza watanicheka na wengine hata kunidharau lakini yote hayo mimi sijali, muhimu ninachoona ni kuinusuru familia yangu. Najua wenye moyo safi watanisaidia."

KAMA kuna jambo ambalo wanawake wengi duniani wanalitamani ni kupata watoto na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Sophia Salum (28) mkazi wa Ukonga Mombasa, Dar es Salaam.

 Lakini baada ya kujifungua watoto watatu kwa mara moja, Sabra, Sabri na Swabri mnamo Februari 5, mwaka huu, maisha ya Sophia yamebadilika. Hivi sasa anaishi kwa mashaka makubwa, akipata chochote mchana, hana uhakika wa kupata kingine usiku au kesho yake.

 Licha ya kutokuwa na uhakika wa kupata lishe lakini hilo halimwondolei jukumu la kuwanyonyesha malaika hao na hilo ndilo lililomfanya kujitokeza na kupaza sauti akilia.

Nimeamua kuomba msaada kwa jamii, inisaidie kulea watoto wangu. Wanangu hawa watatu niliojifungua wana afya njema lakini sina maziwa ya kutosha kuwanyonyesha wakashiba hii inanipa simamzi nzito. Sina uwezo wa kuwanunulia maziwa ya makopo.
Endelea kusoma habari hii..............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits