Saturday, May 1, 2010

Best Blogger Tips
Mwanaume asimulia mkewe alivyoua watoto

SIKU moja baada ya mwanamke mmoja, ambaye anadhaniwa kuwa mgonjwa wa akili, kuua watoto wake watatu kwa shoka, mambo makubwa zaidi yaliyojificha yameibuka, huku ikidaiwa kuwa awali watoto hao walikuwa wauawe kwa panga.

Katika tukio la kikatili lililotikisa mji wa Moshi, mwanamke huyo, Benadicta Thadei, 44, mkazi wa Kariwa, Kata ya Longuo aliwaua kwa kuwakata na shoka watoto wake watatu na kumjeruhi vibaya mmoja usiku wa kuamkia juzi.

Wakati mauaji hayo yakifanyika, mume wa mwanamke huyo, Thadei Aloyce Kihanda, ambaye ni mlinzi wa Hospitali ya KCMC, alikuwa zamu ya usiku na aligundua mauaji hayo mara alipofika nyumbani kwake asubuhi.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kihanda alisema Jumatano jioni kabla ya kwenda kazini, mkewe alimuomba amwachie panga, ombi ambalo alisema lilimshitua sana.

Kihanda alimuomba mkewe amueleze analitaka kwa kazi gani na kwa kuwa ilikuwa inakaribia saa 1:00 usiku na kulikuwa hakuna kazi ya kufanya na mkewe alimjibu kuwa alikuwa analihitaji kwa ajili ya kukabiliana na maadui zake.

“Nakumbuka kabla sijaenda kazini aliniambia nimwachie panga na nilipomuuliza kuwa anataka la kufanyia nini aliniambia kuwa anataka kulitumia kupambana na maadui zake,” alisema Kihanda katika mahojiano hayo.

“Baada ya kuona hivyo, niliamua kuficha vifaa vyote ambavyo vinaweza kuwa silaha kwa kuwa nilijua hali ya mke wangu wakati mwingine huwa hana akili timamu kwa hiyo niliona nichukue tahadhari.

“Baada ya kuhakikisha nimeficha vifaa vyote vinavyoweza kutumika kama silaha niliamua kwenda kazini, lakini kwa bahati mbaya sana bila kujua nilisahau shoka kwenye gogo na ndilo alilotumia kuwaua watoto wetu,” alisema.
Kwa habari zaidi ingia hapa............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits