Thursday, May 6, 2010

Best Blogger Tips
Rais Yar'Adua wa Nigeria afariki Dunia


Rais Umaru Yar'Adua wa Nigeria amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kaimu rais, Goodluck Johnathan ameapishwa rasmi kuwa kiongozi wa taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

Umaru Musa Yar'Adua aliapishwa kushika hatamu za uongozi mwezi wa Aprili mwaka 2007 na kuwa kiongozi wa 13 wa Nigeria. Kabla ya hapo marehemu alikuwa ametangazwa mshindi kwenye uchaguzi uliozua ubishi mkubwa kutoka upinzani, kutokana na hali ya kutatanisha iliyotangulia kutangazwa matokeo hayo.

Bw Yar'Adua alikuwa chaguo la mtangulizi wake Olusegun Obasanjo kuwa mgombea wa chama tawala cha Peoples Democratic Party, na wadadisi wengi waliona hilo kama jaribio la Bw Obasanjo kuendelea kuhodhi mambo hata baada ya kustaafu.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza nchini Ngeria kwa kiongozi aliyechaguliwa na raia kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine wa kuchaguliwa na raia, baada ya kukumbwa na miongo mitatu ya utawala wa kijeshi.
Endelea kusoma habari hii..........

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits