Monday, May 17, 2010

Best Blogger Tips
Vijana CCM wamtisha Makamba, MWENYEWE AWABEZA, ASEMA NI WAJINGA

Via Mwananchi

HALI ya umoja na mshikamano ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM imezidi kuwa mbaya kutokana na makundi mawili yanayosigana kusambaza taarifa zinazomuonya katibu mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba kutojihusisha na upande wowote wakati wa kikao cha leo cha baraza kuu.

Tayari semina ya jana ya vijana hao, ambao ni moja ya nguzo za ushindi wa CCM, imefanyika katika wakati mgumu kutokana na makundi hayo kuvutana mara kwa mara ndani ya ukumbi huku kukiwa na hali ya wasiwasi ya kung'oloewa ama mwenyekiti Hamad Yusuph Masauni au Nassoro Moyo, ambaye ni naibu katibu mkuu wa jumuiya hiyo kwa Zanzibar.

Huku cheche hizo zikionekana mapema, wajumbe 357 wa baraza kuu, akiwemo Makamba, leo watakutana huku kukiwa na taarifa kuwa mtendaji huyo mkuu wa chama ameonywa asithubutu kushinikiza Masauni kujiuzulu.

Sehemu ya taarifa inasomeka: "Usiku wa kuamkia jana (juzi), tumekaa (wenyeviti wa wilaya 20 na wajumbe 19 wa baraza kuu). Tumeweka msimamo kuwa kama Makamba atajaribu kuingilia kati na kumlazimisha Masauni ajiuzulu, tutamwachia UVCCM."

Hata hivyo, haijulikani kama wajumbe waliosalia kwenye baraza hilo, ambalo lina wajumbe 357, wanamuunga mkono Masauni.

Majira ya saa 11:30 jioni, Makamba alipatikana na kusema: "Mimi niko Iringa ndiyo nimeingia kutoka Tabora... nimekuja kushiriki mkutano wa baraza kuu kwa kuwa mimi ni mjumbe.

"Nimepata taarifa nyingi ikiwemo ya 'meseji', lakini wanaosema naweza kuamua Masauni au fulani ajiuzulu ni wajinga."

Makamba atakuwa kigogo pekee wa chama atakayeshiriki kikao hicho baada ya taarifa kuwa mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete ametoa udhuru.
Endelea kusoma habari hii.............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits