Monday, July 12, 2010

Best Blogger Tips
Bilal aweka hadharani ya moyoni mwake

Via Mwananchi

MGOMBEA mwenza wa urais wa Muungano kwa tiketi ya CCM, Dk Mohamed Gharib Bilal jana alitia fora wakati CCM ilipotambulisha wagombea wake mjini Dodoma.

Dk Bilal aliteuliwa na mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kuwa mgombea mwenza kwenye kinyang'anyiro cha urais wa Jamhuri ya Muungano, ikiwa ni siku moja baada ya kuangushwa kwenye mbio za urais wa Zanzibar.

Hafla hiyo, ambayo iliandaliwa na CCM mkoani Dodoma na kufanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa, ilikuwa ni sehemu ya utamaduni wa CCM kutambulisha wagombea wake baada ya kuteuliwa na kupitishwa na chama.

Dk Bilal alikuwa wa kwanza kutambulishwa na Kikwete na alikuwa kivutio katika hotuba yake iliyojaa maneno ya hekima, busara na wosia, na hivyo kusisimua wananchi waliofurika.

Mara kwa mara hotuba yake ilikatishwa na kelele za furaha kutoka kwa mamia ya wana CCM na wananchi waliohudhuria tukio hilo lililosindikizwa na burudani za wasanii tofauti.

Dk Bilali alisema: “Naahidi nitafanya kazi ya kumsaidia kwa moyo, uwezo na ujasiri wangu wote, nitatembea kusini, mashariki, kaskazini, magharibi visiwani na bara kutetea na kuinua ilani ya CCM ya mwaka 2010.”

“Nitafanya yote kwa mujibu wa katiba na maelekezo ya rais ili kuleta ushindi wa CCM pia nitamsaidia rais mtarajiwa wa Zanzibar kuleta ushindi wa CCM Zanzibar na kuweka nguvu, upendo na mshikamano Zanzibar na Bara," alisema Dk Bilal.

Bilal alisema kuwa kwa pamoja kwa kushirikiana na mgombea huyo atahakikisha CCM inashinda visiwani Zanzibar na kuvunja makundi.

“Nitafanya kazi ya kumsaidia kuimarisha CCM kuipa sura mpya Zanzibar ili kuboresha maisha ya wananchi wake. Tutafanya kazi pamoja kuinua imani na nyoyo za Wazanzibar na Tanzania kwa jumla na kuendelea kujenga na kulinda imani ya chama,” alisema.
Endelea kusoma habari hii................

1 comment:

Anonymous said...

Hii kweli inaonyesha kwamba Kikwete kafanya hekima kumchagua huyo Bilal maanake kulikuwa hakuna jinsi angeleta mgogoro mkubwa.


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits