Thursday, July 29, 2010

Best Blogger Tips
CCM kwawaka moto

Via Tanzania Daima

ZOMEAZOMEA kwa wagombea wanaowania nafasi ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye nafasi ya udiwani na ubunge, zimezidi kushamiri, safari hii zikiangukia kwa vigogo wa siasa, John Samwel Malecela na Mbunge wa Manyoni, John Chiligati.

Katika Kijiji cha Igungili, Kata ya Mtera, Malecela, alizomewa na wananchi kwa madai ya kukodi mamluki ili kuvuruga shughuli za kampeni kwa baadhi ya wagombea.

Inadaiwa kuwa kigogo huyo anawatumia mamluki kila kijiji, ambapo Kijiji cha Loje, wagombea wenzake walishtukia njama hiyo na kuhoji uhalali wa watu wale wale kuhudhuria kwenye mikutano tofauti tofauti.

Livingstone Lusinde, ambaye ni miongoni mwa wagombea waliojitokeza kuwania ubunge unaoshikiliwa na Malecela, alitishia kutoendelea na kampeni hizo mpaka mamluki hao waondolewe.

Alisema anashangazwa na hali hiyo, ambayo anaamini kwamba Malecela ni mwanasiasa wa siku nyingi, hivyo hakustahili kufanya kampeni chafu za namna hiyo.

“Hatuwezi kuendelea kujinadi hapa wakati watu hawa (mamluki), tuliwaona katika kijiji kingine ambapo waliuliza maswali hayahaya, iweje waruhusiwe mahali hapa?” alihoji Lusinde.

Akijibu tuhuma hizo, Malecela alidai tuhuma hizo hazina ukweli, kwani hawatambui mamluki hao na ndiyo mara yake ya kwanza kukutana nao.

Wagombea wakimbiwa

Wakazi wa Kijiji cha Matumbulu mkoani, Dodoma walisusia kwenda kwenye mikutano ya wagombea kujinadi, jambo lililowafanya wagombea kuwahutubia wanafunzi wa shule ya msingi.

Inadaiwa kwamba wagombea hao 19, walilazimika kufanya kioja hicho juzi, huku wakijinadi kwa wanafunzi ambao hawaruhusiwi kushiriki katika zoezi la kupiga kura kutokana na umri wao, wakiwataka wawaombee kura kwa wazazi wao.

“Wanafunzi mkaniombee kura kwa mama, mmesikia, mimi naweza kuwa mbunge na kuleta maendeleo ya kijiji na nyinyi wanafunzi pia…,” alisema mmoja wa wagombea hao.
Endelea kusoma habari hii.....................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits